Mkulima anufaike vipi na wewe, mkulima kauza bei ya hasara kwa mlanguzi (mlanguzi kayahifadhi) huyo ndo atakayenufaika.
Chain ya biashara iliharibiwa baada ya serikali kuzuia kuuzwa mahindi nje, hapo ndo mahindi mengi yakawa ndani ya nchi kupelekea kushuka bei kutoka mashambani kwenda kwa mnunuaji (mchuuzi).
Sasa kinachofanyika hapa wafanyabiashara wameweka stock , uhaba ukitokea wanayatoa kuuza kwa walaji kwa bei kubwa huku mkulima akiwa keshakula hasara kitambo tu (nieleweke wengine wanakopa benk kugharamia shughuli za kilimo).
Mwisho wa siku serikali isifanye vitu bila kufikiria maana mkulima akipa hasara mwakani akashindwa kulima tegemea uhaba mkubwa wa mahindi baadae ambao watumiaji pia wataumia, wakulima hali mbaya na wafanyabiashara hawatafanya trade..
Uchumi! Uchumi ! Uchumi ! Wa viwanda (kati).