Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mawakala 94 wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Edward Kinabo, bado hawajaapishwa na kulazimika kuweka kambi katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ya Kibamba na Ubungo.
Imeelezwa, zoezi la kuwaapisha mawakala lilifanyika Oktoba 22, 2025, lakini baadhi yao hawakuapishwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni dosari chache. Mawakala hao wameendelea kusubiri katika ofisi hizo wakisubiri maelekezo mapya kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi
Soma: Mawakala 27 wa mgombea udiwani wa ACT Wazalendo wakwama kuapishwa
Kinabo amesema hizo ni hujuma kwa mgombea na Chama akisisitiza hataondoka ofisini hapo mpaka ahakikishe mawakala hao wameapishwa
Kinabo amesema baadhi ya mawakala hawakuapishwa kwa sababu ya kutokuwa na picha ya passport size kwenye fomu zao, licha ya kuwa na Vitambulisho vinavyokubalika na kanuni za uchaguzi. Aidha, alisema chama chake kimeomba uhakiki na haki ya kuapishwa wa mawakala hao kutokana na changamoto zilizojitokeza siku ya awali ya kuapishwa.
“Tumeomba haki ya kuapishwa kwa siku ya leo kutokana na changamoto zilizotokea tarehe iliyopangwa awali. Tumekuja kwa ibadi kubwa kuapishwa, lakini tumekuta ofisi zimefungwa.
Nae Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi jimbo la Ubungo na Kibamba Rose Mpeleta, alipotafutwa na mwandishi wa JamboTV kuhusiana na malalamiko hayo, alisema, "jukumu la kuapisha mawakala liliisha tarehe 22 Oktoba 2025, na mawakala wote waliowasilishwa kupitia ofisi za vyama vyao walipewa barua inayowaambia siku ya kuapishwa".
Kuhusu masuala ya kuapishwa, ameeleza kuwa siku ya kuapishwa alikuwa ofisini na alipokea changamoto kama hizo kutoka vyama vingine, lakini wote waliopelekwa na vyama vyao waliapishwa.
Kuhusu hatma ya mawakala wa CHAUMMA, amesema kuwa mengine ni ya ofisi. Sababu za kutoapishwa mawakala hao zipo kwenye kata, ila yeye hana majibu.
Aliongeza kuwa wote waliotakiwa kuapishwa waliapishwa kulingana na taarifa alizo nazo, labda kama kulikuwa na hoja nyingine.