Mawakala wa kutafutia kazi watu nje ya nchi wa serikali na binafsi, fikirieni pia kutafutia watu kazi za msimu vijijini Ulaya, Marekani na Canada

Mawakala wa kutafutia kazi watu nje ya nchi wa serikali na binafsi, fikirieni pia kutafutia watu kazi za msimu vijijini Ulaya, Marekani na Canada

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Kama ilivyo kwenye mashamba makubwa ya miwa Tanzania ya viwanda vya sukari kama Mtibwa, Kilombero nk ambako hutoa ajira nyingi mno za msimu kwenye mashamba yao vivyo hivyo Ulaya, Marekani na Kanada

Ona kijiji hiki cha Thailand ambacho ambacho wanakijiji wake kila mwaka msimu wa kuvuna matunda pori sweden huenda kuvuna kwa kipindi cha miezi miwili mshahara wao kwa mwezi huwa ni Euro 2000 sawa na shilingi za kitanzania 5,600,000 kwa miezi miwili hupata shilingi 11,200,000

Mkoloni hizi kazi hizi za mshambani za msimu kwenye mashamba ya Tumbaku,katani nk alipenda kuwapa watu wa vijijini wachapa kazi kutoka Kigoma na Njombe. IIeweke hizi kazi sio za vi modal na za brother na ma sister du wa mijini watu wakachukuliwe vijijini sababu wakipelekwa wasioleweka kule image ya nchi ikichafuta hatuwezi pata fursa tena kama nchi .Hivyo kazi za mashambani wapelekwe wenyewe wanaoziweza

VIDEO HIYO HAPO

Mawakala wetu ni wapigaji na nature ya Ulaya ilivyo watakosa upigaji sababu pesa itaingia moja kwa moja kwa mfanyakazi. Hivyo hakuna upigaji na unyonyaji kama ilivyo kwa nchi za Kiarabu ambapo wanamamlaka mkubwa kwenye maslahi ya watumishi.
 
Sasa hapa tunaweza kuongea, hayo yote yangewezekana, kama usingemchukia huyo beberu, kumchukia umchukie, umeshindwa kutengeneza nafasi za kazi kwa watu wako nyumbani, sasa unawaza kujenga mazingira beberu atengeneze nafasi za kazi kwa watu wako.
 
Kwenye issues za kazi usiingize umasikini wako na njaa, fikiria upatikanaji wa kazi na jinsi utakavyo wajibika, hayo mambo ya ukata ndiyo yanafanya wengi waishie kwenye wizi.
Mimi nimekuelewa.
 
Ajira zinatengenezwa kote ndani na nje ya nchi mawazo yako ya ajira za ndani tu yamepitwa na wakati ndio maana hata hao wazungu wanakuja kufanya kazi kwetu kwenye maeneo ambayo sisi hatuna uwezo nayo na wao kule kwao kuna maeneo ambayo hayana watu wa kufanya hizo kazi ndio maana ukienda kanada misituni kuna wasambaa kule wanakata magogo ya miti ya mbao walibebwa toka LUSHOTO elimu zao darasa la saba!!!
 
Kwanini tusiwatengenezee kwenye viwanda vyetu,au mashamba,yetu ama misitu yetu.
 
Kwanini tusiwatengenezee kwenye viwanda vyetu,au mashamba,yetu ama misitu yetu.
Fursa hiyo wekeza wewe kiwanda chako kule hawaendi kwenye mashamba au misitu ya serikali fursa hiyo kazi kwako!! usiulize swali
 
Hatuna uthubutu wa kisiasa (political will).
sio uthubutu wa kisiasa wewe.Viwanda vingi Tanzania vinamilikiwa na wageni hao ndio wenye uthubutu mitanzania inalala inakoroma tu haina uthubutu kutwa kuimba siasa!!!! Eti uthubutu wa kisiasa .Kule wanakoenda ni uthubutu wa private sector sio siasa!!!
 
Najua tutabishana sana, lakini mwisho wa siku uongozi wa nchi usipoamua kitu kitendeke, hakitatendeka. NUKTA.
 
Najua tutabishana sana, lakini mwisho wa siku uongozi wa nchi usipoamua kitu kitendeke, hakitatendeka. NUKTA.
Uongozi wa nchi sio unaosema kanunue daladala au nenda kafanye kazi nje!!!!! hayo ya binafsi ya kwako!! utasubiri sana hilo serikali inashughulika na macro issues sio micro ya individual level!!
 
Kwenye issues za kazi usiingize umasikini wako na njaa, fikiria upatikanaji wa kazi na jinsi utakavyo wajibika, hayo mambo ya ukata ndiyo yanafanya wengi waishie kwenye wizi.
Ni kweli watu wengine hudhani ajira unapata sababu una shida nyingi una majukumu nk no watu wanataka mchapa kazi finish.Usianze ohh mimi yatima sijui nini? uliona tangazo ya kazi linatafuta yatima? uko sahihi
 
huu uzi umenipa wazo la kutafuta mawakala wa kazi za aboard huko. shukrani sana mtaalam YEHODAYA
Hawa mawakala wanasaidia sana mfano shule nyingi za marekani vijijini nyingi huwa zina upungufu wa walimu kitu ambacho hubidi wenye shule watafute walimu nje ya marekani lakini swali huwa watawapataje ? KUrahisha hutumia mawakala kama huyu mwalimu kwenye video alipata kazi ya kufundisha hesabu marekani kupitia wakala wa ajira

Mkuu kama unafahamu mawakala weka mawasiliano yao,Ila sio wale tapeli tapeli,Watanzania wachapa kazi wapo, passport sio tatizo!!
 
Mkuu kama unafahamu mawakala weka mawasiliano yao,Ila sio wale tapeli tapeli,Watanzania wachapa kazi wapo, passport sio tatizo!!
Jaribu Taesa ni mawakala wa serikali wa kutafutia ajira watanzania nje ya nchi wana website inaitwa Taesa Google andika Taesa .

Ofisi zao ziko Dar zinatazamana a chuo cha CBE nilienda muda mrefu sijui bado wapo pale au wamehama
Kwa private wako wengi andika google Tanzania recruitment agency watakuja kibao halafu angalia kazi walizonazo kwa sasa mara nyingi huwa wanapost lakini hata wasipopost kuuliza sio ujinga waweza wauliza kwa kwenda ofisini kuandika email au kuwapigia

Lakini pia sio vibaya kutafuta recruitment agency wa nchi nyingine hata za ulaya na marekani au canada kuangalia wao wamepata kazi ya ku recruit watu wa kazi zipi huwa wanaonyesha kabiisa kuwa wanatafuta foreigners Jaribu na wa kenya nao hupeleka nje wengi jaribu na wa Uganda na Rwanda pia.Usiridhike na wa Tanzania tu saka kuanzia kule unakotaka kwenda au nchi baada ya nchi ya ulaya na marekani na Canada .

Mtafutaji hachoki akichoka keshapata
Ni kitu inataka utulie mitandaoni hasa na u concentrate hasa

Good luck
 
Back
Top Bottom