Mawakala wa Mabasi Kituo Kikuu cha Mabasi Mkoani Dodoma wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa Kituo hicho, wakikitaja kama Mkombozi wa Vijana wengi Mkoani humo ambao wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali Kituoni hapo ikiwemo ujasiriamali na biashara ndogondogo
Mawakala hao pia wamezungumzia uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 29, 2025 pamoja na maandalizi yao binafsi, wakiahidi kushiriki Kikamilifu kwa kumpigia kura kiongozi ambaye ni msikivu, mwenye kuzingatia changamoto zao na yule ambaye amekuwa akitanguliza maslahi na ustawi wa Jamii mbele katika kuhakikisha kuwa wanakuwa na mazingira bora ya ufanyaji kazi zao
"Sisi tuishukuru sana serikali, serikali ya Mama Samia na wasaidizi wake wote wanaomuunga mkono katika kuwaletea maendeleo wananchi, sisi wanufaika wa stendi hii tunasema ahsante, serikali imewekeza hapa mabilioni ya pesa kwaajili ya kutupa ustawi, changamoto zilizobaki hapa tunaamini kuwa maendeleo ni mchakato kwahiyo tutaendelea kuzungumza na serikali. Waliojitokeza na kuamua kubaki kwenye stendi ile ya zamani hatuungani nao mkono." Amesema Bw. Makoye Fredrick, Mmoja wa Wakala hao
Mawakala hao wamezungumza na wanahabari mara baada ya Kikao chao na Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Ndugu Geofrey Kiliba, Mwenyekiti huyo akiwaasa Mawakala hao kuendelea kutunza amani wakati wa uchaguzi Mkuu, kujitokeza kupiga kura pamoja na kuepukana na baadhi ya watu wanaotaka kuwatumia kutimiza maslahi yao binafsi ambayo ni kinyume na maslahi na Tunu za Tanzania