KERO Mawakala wa NMB tuna changamoto ya commission na kusumbuliwa na Mtandao

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni wakala wa huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu na benki kwa takribani miaka mitano sasa. Kero yangu ni kuhusu huduma za Benki ya NMB. Takribani miezi miwili iliyopita, benki ilitangaza kufanya maboresho ya huduma zake na kuzisitisha kwa siku tatu hadi nne, lakini tangu huduma ziliporejea, hali imekuwa ngumu kwetu mawakala.

Kwanza, tumepunguziwa malipo ya commission. Pili, mtandao umekuwa ukisumbua mara kwa mara kuliko ilivyokuwa awali, hali inayofanya utoaji wa huduma kwa wateja kuwa mgumu. Wakati mwingine asubuhi huduma zinakuwa vizuri, mchana mtandao unasumbua, jioni unakaa sawa, kisha tatizo linajirudia.

Changamoto nyingine ni miamala kuonyesha kuwa imefeli wakati fedha tayari zimetoka, na risiti haitoki. Hali hii inatupa usumbufu sisi mawakala na wateja wetu. Tunaomba wahusika wa NMB walifuatilie tatizo hili na kuboresha huduma zao.
 
Poleni sana, sasa itakuwaje?
 
Kamisheni ya NMB ni upumbavu mtupu. Wanaofanya biashara ya miamala mnastahili pongezi. Mimi niliona bora tu kula mtaji.
 
Back
Top Bottom