Mawakili msipojitathimini taaluma yenu inakwenda kufa kifo cha kisiasa

Mawakili msipojitathimini taaluma yenu inakwenda kufa kifo cha kisiasa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Duniani wanaitwa wasomi, Afrika wanaitwa wasomi ila Tanzania nachelea kuwaita wasomi.

Endapo Mawakili mtashindwa kuungana nakupigania Uhuru wenu basi kitambo kidogo mtapigania kutoka gereza la fikra. Mkwamo wenu ni mkwamo wa jamii, nimkwamo wa Taifa. Natambua mna familia ila nawakumbusha kuwa mna kiapo ndani yenu pia. Mnayo nafasi yakulisimamia taifa kwenye milango ya mahakama na kuakikisha tunapata haki.

Alianza Fatma na sasa ni zamu ya Jebra, je Nani atafuata? Bado tunao watu wa kariba hii miongoni mwenu? Wangapi?
 
Kwa jebra, Sina swali. Niliwahi kujiuliza wakili gani ana akili za kitoto vile? Sijajua ni kuwafurahisha watu ambao hata yeye mwenyewe pengine hawajui au basi tu ndio alivyo. Utoto ni mwingi Sana, mbona akina majura magafu, ishabakaki, Peter kibatala hawapo vile?
 
Ktk utawala huu, jiwe ameiteka mihimili yote ukiwemo mhimili wake. Nchi inaongozwa na maagizo ya mtu (jiwe) na tunafuata anachokitaka.

Kinachowapata akina Jebra na wengineo ni mwendelezo wa ukandamizaji wa haki za wananchi.
 
Jebra amekuwa mwanasiasa na mwanaharakati siyo mwanasheria tena!
Hivyo vitu ulivyovitaja hapo,havitenganishiki,sheria inaongoza siasa na mwanasheria atakaye paza sauti kukemea siasa zinazokiuka sheria za nchi ataonekana ni mwanaharakati tu....

Hayo mengine ni maneno ya siasa tu kuwanyamazisha watu wasikemee maovu.
 
Hongera Mh.Wakili kusema ukweli mchungu, Kiukweli tunawategemea walau nyie Wabobezi kada ya kati kuliongoza taifa kujitambua.
 
Jiwe muda wote amekuwa na mbinu ya kutaka kudhoofisha mihimili ya Bunge na Mahakama . Ameweza kuwathibiti mahakama kiasi kwamba anawateua majaji anaowapenda kwenye mikutano ya hadhara bila kufuata utaratibu; Bunge ndio kabisa analielekeza kila kitu cha kufanya ikiwemo hata miswada ya kujadili licha ya kutumia fedha za serikali bila idhini ya bunge!!!

Tanzania Law Society imekuwa mwiba sana kwa jiwe na jitihada zake kutaka kuwadhoofisha zilianza toka Mwakyembe alipokuwa waziri wa sheria lakini akashindwa. Angalia tu nani wamekuwa viongozi wa TLS; kuanza na Tundu Lissu, akafuatiwa na Fatma Karume . Wote hawa wamekuwa hawakubaliani na jinsi Jiwe anavyoendesha nchi.

Jiwe anatumia sana ofisi za Jaji kiongozi na Attornet General kuwathibiti wanasheria ambao hawakubaliani na ukiukaji wake wa sheria kwa kuwaamuru watumie kamati yao ya maadili kuwasimamisha uwakili wale anaoona ni kikwazo kutimiza nia yake ya kuwa dikteta kamili nchini.

Tumeshuhudia Fatma Karume akisimamishwa kuwa wakili na sasa mawakili wengine wakina Kambole na mwenzie wanaosimamia kesi za wanachama wa upinzani nao wakiwa katika mchakato wa kusimamishwa kufanya shuhuli za uwakili!!! Huo ndio utawala wa Jiwe anaejiita mtetezi wa wanyonge!
 
Tanzania Law Society imekuwa mwiba sana kwa jiwe na jitihada zake kutaka kuwadhoofisha zilianza toka Mwakyembe alipokuwa waziri wa sheria lakini akashindwa. Angalia tu nani wamekuwa viongozi wa TLS; kuanza na Tundu Lissu, akafuatiwa na Fatma Karume . Wote haha wamekuwa hawakubaliani na jinsi Jiwe anavyoendesha nchi.
Kwa hiyo kazi ya viongozi wa TLS ni kupingana na serikali? basi ni chama cha kijinga.Mimi nilifikiri TLS ni proffessional body kama chama cha madaktari Tanzania au bodi ya mainjinia au bodi ya wahasibu au chama cha wataalamu wa hisabati nk kumbe TLS ni kama Club tu ya wanasheria kisicho na malengo proffessional.
 
Kuna mhimili naskia umejichimbia chini chini zaidi ndio kikwazo ....
 
Alianza Fatma na sasa ni zamu ya Jebra, je Nani atafuata? Bado tunao watu wa kariba hii miongoni mwenu? Wangapi?
Mawakili ukitaka kujua ukali wao ni mahakamani na kwenye makaratasi
Hao karume na Jebra wamevamia fani ya siasa ndio maana ni wepesi Kama mlenda
 
Mawakili ukitaka kujua ukali wao ni mahakamani na kwenye makaratasi
Hao karume na Jebra wamevamia gani ya siasa ndio maana no wepesi Kama mlenda
Watanzania sijui tuko vipi katika masuala yetu na hata katika kutoa mawazo flani kuhusu ishu flani.
Mfano kuhusu wakili jebra, sijaona mtu yeyote kazungumzia ishu ya kwa nini kapelekwa advocate committee, kosa Lake, halafu ndo watu tuanze hapo kuona kama ana tatizo au la.
Advocate committee anaweza pelekwa wakili kwa misconduct yoyote kati yake yeye na mteja, au attorney general, au jaji kutokana na aina ya misconduct ambayo huainishwa na yeye hupewa siku 14, kujibu, sijaona hyo charge sheet, na hata yeye majibu yake, ila hapa anaonyesha tu kuwa kama kuna sympathy flani anaitaka toka kwa wananchi.
Pia kumbuka tu kuwa hayo makosa anayotuhumiwa nayo japokuwa hayajulikani, bado ni tuhuma na hivyo anapewa Muda wa ku-defende all allegations na hivyo ni suala la Muda tu.
Ila niseme, kama kafanya kosa lolote, atahukumiwa tu kama watu wengine. Sheria ni msumemo. Kama hajafanya ataachiwa tu
 
Duniani wanaitwa wasomi, Afrika wanaitwa wasomi ila Tanzania nachelea kuwaita wasomi.

Endapo mawakili mtashindwa kuungana nakupigania Uhuru wenu basi kitambo kidogo mtapigania kutoka gereza la fikra. Mkwamo wenu ni mkwamo wa jamii,nimkwamo wa Taifa. Natambua mna familia ila nawakumbusha kuwa mnakiapo ndani yenu pia. Mnayo nafasi yakulisimamia taifa kwenye milango ya mahakama na kuakikisha tunapata haki.

Alianza Fatma na sasa ni zamu ya Jebra, je Nani atafuata? Bado tunao watu wa kariba hii miongoni mwenu? Wangapi?
Watawafungia uwakili lakini hawatawafungia mawazo yao
 
Watanzania sijui tuko vipi katika masuala yetu na hata katika kutoa mawazo flani kuhusu ishu flani.
Mfano kuhusu wakili jebra, sijaona mtu yeyote kazungumzia ishu ya kwa nini kapelekwa advocate committee, kosa Lake, halafu ndo watu tuanze hapo kuona kama ana tatizo au la.
Advocate committee anaweza pelekwa wakili kwa misconduct yoyote kati yake yeye na mteja, au attorney general, au jaji kutokana na aina ya misconduct ambayo huainishwa na yeye hupewa siku 14, kujibu, sijaona hyo charge sheet, na hata yeye majibu yake, ila hapa anaonyesha tu kuwa kama kuna sympathy flani anaitaka toka kwa wananchi.
Pia kumbuka tu kuwa hayo makosa anayotuhumiwa nayo japokuwa hayajulikani, bado ni tuhuma na hivyo anapewa Muda wa ku-defende all allegations na hivyo ni suala la Muda tu.
Ila niseme, kama kafanya kosa lolote, atahukumiwa tu kama watu wengine. Sheria ni msumemo. Kama hajafanya ataachiwa tu
Ili kupata huruma kambole ametoa wito,lakini hati ya mashitaka ameificha,hao ndio mawakili wetu waliolewa siasa
 
Jebra amekuwa mwanasiasa na mwanaharakati siyo mwanasheria tena!
Askofu au padre au mchungaji au hata shehe, kama anaunga mkono serikali, hata akitoa matamko ya kuunga mkono serikali, hakuna tatizo. Ole wake apingane au akosoe suala Fulani linaloshadidiwa na serikali, hasa serikali hii ya Magufuli, basi shida itaanzia hapo. Ataambiwa anachanganya dini na siasa, in mwanaharakati, nk.
Askofu Gwajima no Mbunge, lakini hatusikii kwamba kachanganya dini na siasa.
 
Back
Top Bottom