Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Wewe kweli Naïve. Unakumbuka ishu ya Dk. Masumbuko Lamwai? Kwa kuwa tu alikuwa mwanasiasa wa upinzani, chuo UDSM walimtimua kisa haja publish. Sawa, usipopublish kweli unatimuliwa chuo, lakini wengi hawapublish, ika kama utaonekana unakera wakubwa, vigezo na masharti yanazingatiwa sana tu.Watanzania sijui tuko vipi katika masuala yetu na hata katika kutoa mawazo flani kuhusu ishu flani.
Mfano kuhusu wakili jebra, sijaona mtu yeyote kazungumzia ishu ya kwa nini kapelekwa advocate committee, kosa Lake, halafu ndo watu tuanze hapo kuona kama ana tatizo au la.
Advocate committee anaweza pelekwa wakili kwa misconduct yoyote kati yake yeye na mteja, au attorney general, au jaji kutokana na aina ya misconduct ambayo huainishwa na yeye hupewa siku 14, kujibu, sijaona hyo charge sheet, na hata yeye majibu yake, ila hapa anaonyesha tu kuwa kama kuna sympathy flani anaitaka toka kwa wananchi.
Pia kumbuka tu kuwa hayo makosa anayotuhumiwa nayo japokuwa hayajulikani, bado ni tuhuma na hivyo anapewa Muda wa ku-defende all allegations na hivyo ni suala la Muda tu.
Ila niseme, kama kafanya kosa lolote, atahukumiwa tu kama watu wengine. Sheria ni msumemo. Kama hajafanya ataachiwa tu
Lamwai akasimamishwa na uwakili, mambo magumu!! Wadau wakamtonya, unga mkono juhudi!! Alikabidhiwa kadi ya CCM na Mkapa, enzi hizo. Uwakili ukarejeshwa, naamini hata angetaka kurudi UDSM wangempokea tu. Ila ndio akapewa mafaili ya kesi za CCM na kwa kweli amerudisha 'value for money' kabla hajafariki.
Kama mtu ni kero kwa serikali, hata bangi atachomekewa. Lengo avurugwe. Hata kama hana kosa