Mawakili msipojitathimini taaluma yenu inakwenda kufa kifo cha kisiasa

Wewe kweli Naïve. Unakumbuka ishu ya Dk. Masumbuko Lamwai? Kwa kuwa tu alikuwa mwanasiasa wa upinzani, chuo UDSM walimtimua kisa haja publish. Sawa, usipopublish kweli unatimuliwa chuo, lakini wengi hawapublish, ika kama utaonekana unakera wakubwa, vigezo na masharti yanazingatiwa sana tu.
Lamwai akasimamishwa na uwakili, mambo magumu!! Wadau wakamtonya, unga mkono juhudi!! Alikabidhiwa kadi ya CCM na Mkapa, enzi hizo. Uwakili ukarejeshwa, naamini hata angetaka kurudi UDSM wangempokea tu. Ila ndio akapewa mafaili ya kesi za CCM na kwa kweli amerudisha 'value for money' kabla hajafariki.

Kama mtu ni kero kwa serikali, hata bangi atachomekewa. Lengo avurugwe. Hata kama hana kosa
 
Kosa lake aliita mahakama ya kisutu "kisutu revenue authority", huu ni utoto ambao unafanywa na wapuuzi wachache. Wakili msomi unaidharau mahakama sababu tu upate likes na comments nyingi.
 
Mahakama zikianza kiswahili sasa tutajikuta hata mawakili ni wapiga porojo tu
 
Nani alikwambia kukosoa mienendo mibaya ya serikali sio kuwa professional? Hujawaona chama cha madaktari walivyosimamia profession yao huu wakati wa corona? Je msimamo wao unaweza kuita kuwa sio professional?

Wanasheria wanalinda katiba ya nchi ambayo watawala wanataka kuifinyanga finyanga; watu wanaojua kuitafsiri Katiba ni hao wanasheria, ambao wanajaribu kuiweka serikali katika mstari wa kuiheshimu katiba!!! Wasipofanya hivyo nchi itatawaliwa kama nyumba ya mtu binafsi ambapo watawala watafanya kila wanalotaka bila pingamizi lolote na hapo nchi itakuwa ya kiimla!!!
 
Ukiondoa vyama vingne hiki ndyo walau kimebaki ktk kupaza sauti ktk zama hizi za kusifu na kuabudu
 
Baada ya Jiwe kuwa anapumulia mashine ni wazi sasa Tanzania inakuwa "reset to factory".

Dikteta Meko aliyehodhi Uhuru wa Mahakama na Uongozi wa Bunge anasubiri kuingia kwenye futi 6 chini ya ardhi.

Mawakili watarudisha heshima yao kama ilivyokuwa zamani.
 
Learned brothers and sisters...
The sun will rise tomorrow
For now Aluta continua
 
Jebra amekuwa mwanasiasa na mwanaharakati siyo mwanasheria tena!
Mnachoshindwa kuelewa wewe na washenzi wenzio mnazani siasa ipo kwaajili ya watu fulani na wengine wakifanya ni makosa!! Mwanasiasa wote wanafan zao hata wale wenye PhD zenye mashaka
 
Mnachoshindwa kuelewa wewe na washenzi wenzio mnazani siasa ipo kwaajili ya watu fulani na wengine wakifanya ni makosa!! Mwanasiasa wote wanafan zao hata wale wenye PhD zenye mashaka
Toa hoja acha kutukana ukiwa umejificha nyuma ya keyboard.
 
Ni divide and rule ndiyo inayotembea kwenye tasnia nyingi...hata waandishi nao wapo wapo tu wakati haki zao zinapokwa !!
Ni mkakati endelevu wa Serikali awamu ya tano. Kuminya kila wenye kiherehere ya kujaribu kudai haki.
 
Jebra amekuwa mwanasiasa na mwanaharakati siyo mwanasheria tena!

Ni kama ilivyo kwa Bashiru Ali kuwa katibu Mkuu Kiongozi, na wakati huo huo kuwa katibu Mkuu wa ccm ama?
 
Kamanda, mswalie Mtume. Chama cha Wanasheria kilipata liana, nuksi, walakin, pale walipomchagua tundulissu awe rais wao. Ukichagua rais, mathalani Magufuli au George Bush au Daniel arap Moi, ujue hiyo ndiyo picha yako wewe kwenye kioo. Walipatwa na shetani gani hadi wampigie kura zao tundulissu? What did they gave in mind?

As if hiyo haitoshi, muda wake ulipopita wakapata nafasi ya kujirekebisha - wahenga waluisema kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa, can you believe it - wakampa kura zao zote fatmakarume, a princess of the land, Babu yake mgombozi wetu, akarithi mikoba ya tundulissu anatukana Mapinduzi matukufu, anapinga Muungano ulioasisiwa na Babu yake, Ni laana hiyo iliwaangukua, Mwalimu alisema haikuachi sawa na kula nyama ya mtu.

Huyu waliyemchagua majuzi anawasingizia wenzie eti 60 wamekufa Covid: ni lawyer, si nurse, wapi na wap? Laana ya TLS hii, wacha iwatafune hadi kizazi cha 5 kama ilivyoandika Tayrati ya Mussa.
 
JEBRA KAMBOLE ni ripota wa DW, kumbe pia ni Wakili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…