Taarifa za Hivi Punde, leo Januari 10, 2026
Clemence Mwandambo mkazi wa Mbeya aliyekamatwa tarehe 29.12.2025 amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke Jana tarehe 9 Januari 2026 na Jeshi la Polisi bila ndugu zake au sisi Mawakili wake kujua!
Pamoja na Juhudi za kutafuta alipokuwa amehifadhiwa tangu tarehe 29.12.2025, taarifa za kuhifadhiwa kwake hatukuweza kuzipata kwa sababu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kutokuwa wakweli juu ya sehemu anayoshikiliwa Clemence Mwandambo.
Jana kapelekwa Mahakama ya Temeke na Kusomewa maombi yanaitwa “Binding over” (Maombi ya Kuwa Chini ya Uangalizi) ambayo upande wa Jamuhuri wameomba Mahakama itoe Amri zifuatazo:
1. Kutofanya kosa lolote ndani ya Mwaka mmoja.
2. Kila ijumaa ya Mwisho wa Mwezi kuripoti Polisi Mbeya ndani ya Mwaka Mmoja kuanzia Jana.
3. Kutoa akaunti zake zote za Mitandao ya Kijamii kwa Jeshi la Polisi.
Baada ya kusikilizwa kwa Maombi hayo Mahakama ikakubaliana na maombi ya upande wa Jamuhuri na kutoa Amri hizo!
Kwa kuwa hakuwa na Wakili wala ndugu na ukizingatia hakuna aliyekuwa anajua alipohifadhiwa baada ya kutoka Mahakamani akapelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe na leo saa sita Mchana ndugu wakapigiwa simu ili wakamdhamini!
Hivyo basi Clemence Mwandambo Yupo chini ya Uangalizi baada ya Amri za Mahakama kutolewa hiyo Jana!
Hekima Mwasipu na Philipo Mwakilima
Mawakili