Mawakili ni watetezi wa wanyonge au ni waporaji wa wanyonge?

Mawakili ni watetezi wa wanyonge au ni waporaji wa wanyonge?

Uwakili wa leo ni kula na mafisadi tu, kuwa mwangalifu na yeyote anayejiita wakili kwani unamlipa fedha halafu mdaiwa wako naye anamlipa! hapo utakuwa umeliwa, sasa cha ajabu zaidi na kushangaza wakili anayefanya hivyo unakuta Rais anamchagua kuwa Jaji

Mmeona eehhh?

Kite umeshindwa kujificha kuwa ni wakili na kama sio,basi baba yako alikuwa wakili-ahaaah!
WomenofSubstanc kasema Ukweli mtupu. na ni vyema mkajua siku hizi TZ ukipata case kama ya zaidi ya 500M,ma advocate wanapishana mlangoni kuja kuomba kukutea na sio wewe kuwafuata?Na wanafanya upepelezi kwanza kujua kama umeiba kweli na bado unazo au umesingiziwa,wakiona hizo pesa huna basi wanajua you are not hotcake.Kite ninayo evidence-what next?Hivi mtu anashikwa na kiungo cha Albino anakwenda mahakamani kushinda case -hii inataka mtu kusomea sheria?Mafisadi kina Yona,Mramba etc baba zao hakuwahi hata kufanya biashara ya karanga leo hii wana pesa ambayo hata kama tangu waanze kazi jumlisha posho zao,mishahara yao yote,bila kutumia hata senti 5,hazifiki na wanazitangaza hadharani? Mimi siku nchi hii ikiwa ya sheria mkononi sitoshangaa!Maana vitabu vya sheria havifanyi kazi!

Hapo sasa! Je hii ndio noble profession? Katika moja ya maswali waliyokuwa wanauliza panel ya kutahini wakili watarajiwa ilikuwa hili.."Endapo mteja wako ataungama kwako na kusema ni kweli katenda kosa ila anataka umtetee utafanya nini"Jibu sahihi lilikuwa ( sijui kama ni sahihi sic!) unatikiwa utunze siri ya mteja lakini wakati huohuo uhakikishe haki inatendeka.Hivyo unamshauri akubali umsaidie kufanya mitigation ili apate adhabu ndogo kwani amejifunza na kuona vibaya kuwa kakosa.Hii inategemea hasa lwenye ksei z mauaji.Siku hizi nadhani mambo yamegeuka. Ieleweke kazi ya wakili siyo kusaidia kuimarisha uhalifu bali ni kuhakikisha haki inatendeka kwa mshtakiwa kuwakilishwa kisheria.

Mimi nafikiri kuna haja ya serkali kuanzisha sheria na kanuni mpya kuhusiana na masuala ya 'malpractice' ya hawa mawakili. Mfano mzuri ni hapa Marekani wakili inabidi akate insurance kujilinda kabisa kama akichemka anaweza kushtakiwa na kutakiwa kulipa mapesa mengi sana. Hili suala kwa sasa hipo haja kuwepo Tanzania ili kulinda haki za hasa wanyonge.

Shadow.

Sijui hili limefikia wapi..Shadow na wengine pls update us.




Ukisoma Report ya chama cha mawakili ya mwaka 2008 utaona kuwa huu mchakakto unaendelea. Kutakuwa na compulsory insurance soon. Ila kwa ufahamu tu makampuni mengi ya uwakili yameshachukua hizo insurance. (Sisi lawfirm yetu tunayo). Ila kama mtu anataka kupata legal services cheaply kutoka kwa cheap lawyer asitegemee kupata best of legal services standards. (Rules za economics haziruhusu).

What is cheap?..small fee?
 
Chaumbeya,
Points noted.Ila ukweli bado utabakia palepale kuwa kadri siku zinavyoenda, heshima kwa mawakili na hata wanasheria inapungua kwa kasi ya ajabu.
Unayosema yapo na yatakuwepo ila hayaondoi ukweli.

Ripoti mbalimbali za hali ya rushwa na ufisadi nchini zinataja, pamoja na maeneo mengine kuwa sekta ya utoaji wa haki ie. mahakama,
polisi, and the related ni vinara wa rushwa na ufisadi kwa vile inaathiriwa sana na tatizo la kuporomoka kwa maadili 'moral decay'. Sababu ni debatable; lakini miongoni mwake ni kudorora kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi, na taifa, fani ya uongozi wa kisiasa kugeuzwa kuwa ni ya kujitajirisha badala ya kujitolea, na kwa bahati mbaya taifa kuingizwa katika mtego wa kutoa marupurupu lukuki na yasiyolipishwa kodi kwa viongozi wa siasa, bila kuzingatia uwiano na maslahi ya watumishi wa umma na sekta binafsi. Kwa mazingira hayo kinachowasukuma watoa haki ambao ni pamoja na wanasheria wakiwemo mawakili wa kujitegemea, ni kutafuta mwanya wa kuwakamua kwa kadri inavyowezekana wateja wao, hata kama kwa kufanya hivyo hakumhakikishi mteja kuwa atapata the best of his services....wakili kula huku na kule si jambo geni hizi sasa ili kukidhi mahitaji ya ulafi wao....
 
Una-evidence yoyote ile juu ya swala hili?????

Ushahidi ni daily experience. Nadhani wewe haijakutokea ndio maana unaleta law technicalities kwenye realities of life.
Mfano: Rais anawateua majaji kwa mkupuo, wengine tunasoma kesi walizoziamua quite controversial judgements!!!!
UJAJU ni kama udaktari bingwa. Upungufu wa madakitari bingwa hauwezi kumfanya Medical assistant aende theatre kufanya open heart surgery. nadhani UJAJI ni rank moja na udaktari bingwa in terms of the requirement of high level of profesionalism maana kuna kusave rights za mtu ambazo zina-determin maisha yake hapa duniani sawa na daktari bingwa kusave maisha ya mgonjwa.
 
Back
Top Bottom