Mawakili wa Chadema wajitoe tu kwenye kesi ya Mbowe!

Lissu alishawaambia kuwa wasimtete mtu yeyote wamuache mbowe serekali iamue wenyewe
 

..wajitoe, Jaji awahukumu, halafu wakakate rufaa ktk mahakama ya rufani.
 
No...kwa sasa hivi wasijitoe.Jinsi wanavyoendelea na kesi ndivyo wanavyo wavua nguo.
Kibatala ni mtu mwenye akili saana.atazitumia case study zilizotolewa na Jaji wa hii kesi kumuachia Mbowe

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Ni kweli lakini kumbuka wanazid kupoteza muda,na mbowe anaendelea kusota gerezani..Ni Bora hicho kilichopangwa na Serikali kitimie mapema badala ya kuzunguka sana.
 
..wajitoe, Jaji awahukumu, halafu wakakate rufaa ktk mahakama ya rufani.
Sababu za kujitoa zitakuwa zipi labda?

Zitajengwa katika msingi upi wa kisheria?

Kuna kesi katika kumbukumbu ambayo wakili/mawakili walijitoa na hukumu kutolewa na aliyehukumiwa akakata rufaa na kwenda kushinda ktk mahakama y juu...?

Je, kwanini wasiendelee kesi na kuweka kila kumbukumbu ya makosa ya Jaji kisheria na huko mbeleni wakijua na kutumia hizo "hila" za Jaji wakakata rufaa...?

Mimi nadhani kuendelea na kesi hadi mwisho ni option nzuri zaidi kuliko kujitoa kwa staili anayopendekeza mtoa mada...

Na kama ni lazima, na wana sababu za msingi na za kisheria, washitakiwa wao ndiyo wamkatae Jaji kwa kusema hawana imani naye huku wakitoa sababu za kisheria na zinazoungwa mkono na ushahidi wenye nguvu...
 

..mawakili wajitoe

..na washtakiwa wasiweke mawakili wengine.

..utetezi wao ubakie kuwa ni kutokana mashtaka yote.

..mahakama iendelee na ushahidi wa upande mmoja mpaka itakapotoa hukumu.

..watakapopata rufaa watapata nafasi ya kupinga ushahidi wote mbele ya majaji wa mahakama ya rufani.

..hoja yao ni kuwa hawana imani na Jaji anayesimamia kesi hii, na hawana imani na Jaji Kiongozi ambaye ana mamlaka ya kum-replace Jaji wa sasa hivi.
 
Mkipigwa kwenye sheria mnajifanya mnaonewa,
Mlizoea kuhonga mahakimu na majaji kisha mkajifanya maarufu huku mkitumia rushwa.
Pambaneni kwa uwezo wenu mkishinda basi na mkishindwa tulieni.
Do you have any knowledge about law and judiciary? Kama huna hiyo knowledge basi tulia usome TU comments za wenye kujua!
Na siku nyingine usijaribu hii mbinu ya kuijaribu bunduki kwenye kichwa chako utajijeruhi! Ni nani anayeihonga idara ya mahakama na watendaji wake zaidi ya serikali Yako ya ccm? Rejea uteuzi wa majaji wote ukatae Kwa evidence Kama hawajahongwa vyeo walivyonavyo Sasa!
Mwajiri akikupandisha cheo ni rushwa hiyo na hutoweza kutenda nje ya matakwa yake! Unalitambua hilo au upoupo TU?
 
Mkipigwa kwenye sheria mnajifanya mnaonewa,
Mlizoea kuhonga mahakimu na majaji kisha mkajifanya maarufu huku mkitumia rushwa.
Pambaneni kwa uwezo wenu mkishinda basi na mkishindwa tulieni.
Sawa Mkuu hata Polepole alikuwa na mawazo kama yako.
 
Naunga mkono hoja, utetezi uendelee hadi mwisho ili tushuhudie kwa macho na masikio yetu matatizo ya mahakama zetu pamoja na udhaifu wa Majaji na Jeshi letu la Police.
 

Bahati mbaya sana pana kigugumizi:

https://www.jamiiforums.com/threads...u.1939760/[url] Kigugumizi hiki hakuna afya.
 
Mahakamani si mahala pa siasa. Kuna sheria, kanuni na taratibu za kuwa wakili. Hao mawakili wakifanya hicho ambacho akili yako inafikiri (cha kususia kesi) watafutiwa uwakili wao kama alivyofutwa Fatuma Karume. Hawatakuwa mawakili tena nchini hapa.
Kwa akili yako unafikiri kwamba hawa ni mawakili wa Mbowe. Yaani wameajiriwa na kusajiriwa kama mawakili wa Mbowe. You are very wrong bwana mdogo. Hawa ni mawakili wa mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala si mawakili wa mbowe! Wako pale kuisaidia mahakama.
 
Mkipigwa kwenye sheria mnajifanya mnaonewa,
Mlizoea kuhonga mahakimu na majaji kisha mkajifanya maarufu huku mkitumia rushwa.
Pambaneni kwa uwezo wenu mkishinda basi na mkishindwa tulieni.
In short kichwa chako kimejaa taka tupu,akili/ubongo hauna
 
Jaji anataka aweke historia kwa kumfunga mbowe. Ila tatizo ana bichwa bovu ambalo linashindwa kupambanua na kutambua anajiwekea historia mbovu mpaka anakwenda kaburini itamtafuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…