Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna wa Magereza na Mkuu wa Gereza kuu la Ukonga

Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna wa Magereza na Mkuu wa Gereza kuu la Ukonga

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
HEVkxjnaUAA5CBo.jpg
Sisi mawakili Maduhu William, Nashon Nkungu na Paul Kisabo tumefungua shauri la Kikatiba ambalo ni Shauri No. 7300dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Shauri hili limefunguliwa katika mahakama kuu masijala kuu ya Dodoma. Tumefungua shauri hili kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea, vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu.

Soma Pia:

Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Aprili 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu ambao ni Mruma, Dr. Rumisha na Dr. Longopa, JJJ's.

Tutaipigania Heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana na bila kuchoka.

Wakili Maduhu
 
Je, mamlaka ya magereza yanaweza kuweka vikwazo kwa mawakili wanapokutana na wateja wao?
🤔🤔🤔
 
Hii nchi imeoza kila mahali, Ngoja tuone itakuaje na hii kesi
 
Nikuwapelekea moto tu makatili yote huku Israel anaruka nao mmoja baada ya mwengine hadi watubu
 
Hii imekuja kwa kuchelewa sana. Hii ilibidi ifanyike kitambo sana. Ilitakiwa pawe na kesi nyingi dhidhi ya hawa jamaa, kwa lengo tuu la kuwafanya waogope kupindisha taratibu.
Hongereni Mawakili, japo mmestuka kumekucha.
 
Kesi kama hii ni ile ya
Mchmchum marwa vs musson prisoner officers
Deportation ordinance act
 
Sisi mawakili Maduhu William,, Nashon Nkungu na Paul Kisabo tumefungua shauri la Kikatiba ambalo ni Shauri No. 7300dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Shauri hili limefunguliwa katika mahakama kuu masijala kuu ya Dodoma.
Tumefungua shauri hili kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea,,,vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu.

Soma Pia:

Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Aprili 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu ambao ni Mruma,, Dr. Rumisha na Dr. Longopa, JJJ's.Tutaipigania Heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana na bila kuchoka. Wakili Maduhu
Huyo 4th Respondent, ameunganishwa hapa kwa makosa au vipi?
 
Dawa ya wapumbavu wanaoshindwa kusimamia matakwa ya kisheria ya kazi zao, na badala yake wanafanya kazi zao kwa kuwafurahisha wanasiasa vilaza, ndiyo hii sasa.
 
Sema hawa mawakili wa CHADEMA wamejua 'kuwahangaisha' majaji

At this point ni wazi kuwa hata mahakama/ majaji pia watakuwa wanataka Lissu atoke Gerezani maana kila siku kesi zinafunguliwa

===================


Mawakili watatu, Maduhu William, Nashon Nkungu na Paul Kisabo, wamefungua shauri la kikatiba kupinga kile walichodai kuwa ni vikwazo vinavyowekwa na Jeshi la Magereza kwa mawakili wanapowatembelea wateja wao walioko magerezani.

Shauri hilo, lenye namba 7300, limewasilishwa katika Mahakama Kuu, Masijala Kuu ya Dodoma, likiwataja Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama wadaiwa.

Kwa mujibu wa mawakili hao, hatua ya Jeshi la Magereza kuzuia au kuweka vizingiti kwa mawakili wakati wa kufanya mashauriano ya kisheria na wateja wao—wakiwemo wafungwa na mahabusu—ni kinyume na misingi ya kikatiba na inakiuka haki ya kupata uwakilishi wa kisheria.

Wamedai kuwa vikwazo hivyo vinadhoofisha ufanisi wa huduma za kisheria na kuhatarisha haki za msingi za watuhumiwa na wafungwa, hususan haki ya kusikilizwa na kupata msaada wa kisheria kwa uhuru na faragha.

Shauri hilo linatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Aprili 14, 2026 mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, ambao ni Jaji Mruma, Dk. Rumisha na Dk. Longopa.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Wakili Maduhu amesema wako tayari kupigania heshima na hadhi ya taaluma ya uwakili bila kuchoka.

“Tutaipigania heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana bila kuchoka,” amesema Wakili Maduhu.

Source: IPP Media
 
Mawakili watatu, Maduhu William wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Nashon Nkungu na Paul Kisabo wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), wamefungua shauri la kikatiba kupinga kile wanachodai kuwa ni vikwazo vinavyowekwa na Jeshi la Magereza wanapowatembelea wateja wao waliokomagerezani.

Shauri hilo namba 7300 la mwaka 2026 limewasilishwa katika Mahakama Kuu, Masijala Kuu ya Dodoma, likiwataja Kamishna Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama wadaiwa.

Kwa mujibu wa mawakili hao, hatua ya kuzuia au kuweka masharti kwa mawakili wakati wa kufanya mashauriano ya kisheria na wateja wao wakiwemo wafungwa na mahabusu ni kinyume na Katiba na inakiuka haki ya kupata uwakilishi wa kisheria.

Wamedai kuwa vikwazo hivyo vinadhoofisha utoaji wa huduma za kisheria na kuhatarisha haki za msingi za watuhumiwa na wafungwa, hususan haki ya kusikilizwa pamoja na kupata msaada wa kisheria kwa uhuru na faragha.

Shauri hilo linatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Aprili 14, 2026 mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, akiwemo Jaji Mruma, Dk. Rumisha na Dk. Longopa.

Wakizungumza kuhusu shauri hilo, mawakili hao wamesema wako tayari kupigania heshima na hadhi ya taaluma ya uwakili bila kuchoka.

"Tutapigania heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana bila kuchoka," amesema wakili Maduhu kwa niaba ya mawakili wenzake.
 
Hizi sasa ndio khabari ...kudos kwao Wakili msomi Maduhu et al...kila silaha hata kama ni ndogo itumike, pia itasaidia kuweka kumbukumbu vizuri
 
Back
Top Bottom