Mawakili wetu kuvizia 'technicalities'

Mawakili wetu kuvizia 'technicalities'

Uwepo wa technicalities kwenye sheria ndio unaofanya ma layman washauriwe kuwahire mawakili. Vyenginevo,layman atatoka na hamna huku anaiyona kabisa haki yke.
 
hii fani ya wasanii yani mawakili wa bongo hawana tofauti na wasanii wa bongo
 
Kiukweli hii taaluma ya Sheria hususani fani ya Uwakili imekuwa mzigo kwa jamii
1. Kuna baadhi ya Mawakili hawatoi ushauri wa kweli kwa Wateja unakuta mtu/Mteja kafungua Kesi ambayo haina kichwa wala miguu mbele ya Sheria cha ajabu utasikia hata Makarani Wanamshangaa Wakili lakini anakomaa huku akijua hatima ya Kesi ya Mteja wake
Mapendekezo;
Mamlaka husika ya usimamizi wa Mawakili isiishie kuwasajiri na kuwapa Semina elekezi bali kila Wakili atakiwe kuwa anapelekea Register/ vyovyote utakavopenda kuuita Idadi ya Kesi za Wateja wake kwa mchanganuo
(a) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyoshinda na sababu za ushindi wake
(b) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyoshindwa na sababu za kushindwa kwake
(c) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyojitoa/kutolewa na sababu zake
(d) Kesi au Mashauri yanayo endelea na sababu zake pia muda tangu alipopewa kazi ya Uwakilishi.

2. Uwepo mfumo uliowazi ambao Wananchi tunawea kulalamikia Mawakili Wasiotekeleza Wajibu wao nachelea kuwaita " "******" au Wababaishaji

3. Uwepo mfumo au utaratibu wa mchanganuo wa malipo ya Kesi ili ifahamike mathalani kama Kesi yangu nina dai Milioni 10 na haina gharama za Wakili kusafiri mfano Wakili kutoka Mtaa wa Samora kwenda Kisutu siku hizi wanachanja Mbuga tu, tena wengine "Wababe" wanapanda Bodaboda bila Helmet. Gharama hizi si sawa na Wakili Msomi anaepanda Easyjet kwenda Mwanza.

4. Kampuni za Uwakili ziweke bayana weledi wake mathalani kama wao wamebobea kwenye Ndoa/Mirathi/Talaka/Kodi/Madini/Mikataba/Jinai sio kila Wakili anabeba kila Kesi utadhani fani iko kwenye uwanja wa majaribio.
Mkuu umetiririka vizuri sana.
Hii fani bado inamapungufu sana,na chanzo ni weledi na tamaa.
Na ndio maana hata Madaktari kuna kila mmoja ana fani yake ndani ya fani kuu,au Mchezaji wa Mpira ni kwamba kila mchezaji ana position yake.
Ina kibongobongo,unakuta kila Wakili anafanya kazi zoote peke yake.Kuna Ofisi humu ukienda kuna Wakili Mmoja tu,na Secretary wake labda na trainee mmoja.Maana sijui hata sheria ya kufungua Ofisi kwa hawa Mawakili ina vigezo vipi
 
Po's ndio zinatufanya tutofautiane na layman of laws then kuna kitu kinaitwa general rule and exception to the general rule!!wakili mjanja huwa anacheza na haya maeneo.
 
Back
Top Bottom