Kiukweli hii taaluma ya Sheria hususani fani ya Uwakili imekuwa mzigo kwa jamii
1. Kuna baadhi ya Mawakili hawatoi ushauri wa kweli kwa Wateja unakuta mtu/Mteja kafungua Kesi ambayo haina kichwa wala miguu mbele ya Sheria cha ajabu utasikia hata Makarani Wanamshangaa Wakili lakini anakomaa huku akijua hatima ya Kesi ya Mteja wake
Mapendekezo;
Mamlaka husika ya usimamizi wa Mawakili isiishie kuwasajiri na kuwapa Semina elekezi bali kila Wakili atakiwe kuwa anapelekea Register/ vyovyote utakavopenda kuuita Idadi ya Kesi za Wateja wake kwa mchanganuo
(a) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyoshinda na sababu za ushindi wake
(b) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyoshindwa na sababu za kushindwa kwake
(c) Idadi ya Kesi/Mashauri aliyojitoa/kutolewa na sababu zake
(d) Kesi au Mashauri yanayo endelea na sababu zake pia muda tangu alipopewa kazi ya Uwakilishi.
2. Uwepo mfumo uliowazi ambao Wananchi tunawea kulalamikia Mawakili Wasiotekeleza Wajibu wao nachelea kuwaita " "******" au Wababaishaji
3. Uwepo mfumo au utaratibu wa mchanganuo wa malipo ya Kesi ili ifahamike mathalani kama Kesi yangu nina dai Milioni 10 na haina gharama za Wakili kusafiri mfano Wakili kutoka Mtaa wa Samora kwenda Kisutu siku hizi wanachanja Mbuga tu, tena wengine "Wababe" wanapanda Bodaboda bila Helmet. Gharama hizi si sawa na Wakili Msomi anaepanda Easyjet kwenda Mwanza.
4. Kampuni za Uwakili ziweke bayana weledi wake mathalani kama wao wamebobea kwenye Ndoa/Mirathi/Talaka/Kodi/Madini/Mikataba/Jinai sio kila Wakili anabeba kila Kesi utadhani fani iko kwenye uwanja wa majaribio.