View attachment 2465387
Maisha ya Mwanadamu kiujumla yanatengenezwa na mawasiliano chanya ya kila siku katika mazingira yanayomzunguka.
Neno mazingira likijumuisha nyumbani, kazini, kwenye biashara, kanisani, msikitini, shuleni, vyuoni kwenye mikutano n.k
Kila Mwanadamu hapa Duniani anatamani kufikia malengo yake makubwa ya kimafanikio aliyojiwekea. Wengine wanatamani kuwa wafanyabiashara wakubwa, viongozi, wanasiasa wakubwa, madaktari, wanamichezo, walimu wakubwa ulimwenguni n.k
Mwanadamu ni kiumbe pekee aliyebarikiwa na Mungu
(The Ultimate Intelligence) akajazwa maarifa, karama, hekima, busara, uwezo mkubwa wa kufikiri, kubuni, na kutatua changamoto mbalimbali za maisha yake.
Lakini aya yote hayata wezekana kama una mawasiliano hasi na mahusiano hafifu na Mungu wako pamoja na mazingira yanayokuzunguka kwa ujumla.
Tutapeana mifano miwili, mitatu hili tuweze kwenda sawa:-
1. Hauwezi kupanda cheo kazini au kwenye Uongozi kama una mawasiliano hafifu na mahusiano mabaya na Kiongozi wako ama Boss wako.
2. Hauwezi kuwa Mfanyabiashara mkubwa kama una mawasiliano mabaya na wateja wako.
3. Mwanamichezo hauwezi kuwa kwenye kikosi cha kwanza kama una mawasiliano dhaifu na mahusiano mabaya na kocha wako. Mfano mzuri ni Greatest Football Player of all time
Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro vs
Erik Ten Hag (Manchester United Coach)
View attachment 2465161
Mwaka 2023 👏 ukawe mwaka wako bora kwa kuwa na mawasiliano chanya na mahusiano bora na Mungu wako.
Mwaka 2023👏 ukawe mwaka wako chanya na kuwa na mahusiano chanya na ndugu zako.
Mwaka 2023 👏 ukawe mwaka wa mawasiliano na mahusiano bora na wafanyakazi wenzako, mpenzi wako, wafanyabiashara wenzako, familia yako, wanamichezo wenzako, Viongozi wenzako pamoja na wanasiasa wenzako.
Hata Mitume na Manabii wa Mungu walikuwa na mawasiliano mazuri na Mungu wao ndio maana mahusiano yao, mission zao pamoja na vision zilienda kwa wakati na kwa mpangilio maalum.
Be the One, by "sweat on the small stuff to build the big one".
Tengeneza mawasiliano bora ya kiroho, kimwili na akili hili kujenga mahusiano imara katika maisha yako.
Basi hakika utafanikiwa.
No One know's Everything
No One Who Is Someone
View attachment 2465229