Mawaziri Aisha Kigoda na Seif Khatibu watangaza penzi lao Bungeni

Mawaziri Aisha Kigoda na Seif Khatibu watangaza penzi lao Bungeni

mie nawatakia kila la heri na mola awajaalie ndoa yao idumu

kuhusu upotoshaji wa habari ndio watanzania tunavyoamini ili habari ipate wasomaji lazima uipooshe hiki ni kilema maana watza wadaku sasa stori za udaku ndio zipendwaZo
 
Hakuna lolote hao wanaendekeza sana ngono hapo mjengoni badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi. Kwanini maisha Dom yanapanda maradufu wakati wa Bunge? Na kwa nini kunakuwa na machangu wengi kipindi cha bunge? Hawafanyi kazi zao sawa sawa. Leo unasikia wanataka mfuko wa Jimbo pesa ambayo wewe na mimi unatozwa kodi tena bila huruma halafu hawa jamaa wanaitafuna wakidai ni haki yao na ukihoji unaambiwa una wivu wa kitoto au wivu wa kike ama wao wanasema wanafanya kazi kubwa . Wengine wakiona wamezidiwa wanaomba ulinzi wa ziada. Nakwambia iko siku hata hao wanaowakimbilia watawatosa sijui watakimbilia wapi?
 
Mchango huu unawahusu hawa walio kwenye ndoa au ?? maana wanandoa wana licence kisheria kushughulika.
 
hawa nao wafanye kazi mambo ya kutangaza mapenzi na mashukrani yasiyo ya lazima wakati muda wa bunge ni finyu ni ufisadi tu! Wabunge wanakosa muda wa kuchangia kutokana na dakika zinazotumiwa kwa mambo ya binafsi kama haya, kodi zetu ndo za kutangazia ngono zao??
 
RA naye na sister Z...KIA wangesimama
 
By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!
Aisha ana Advanced Diploma ya Clinical Medicine, na kwa mujibu wa Muundo wa Utumishi wa Kada za Afya anatambuliwa kama Daktari Msaidizi (Assistant Medical Officer). MDs na AMOs wote wanatambuliwa kama madaktari.
 
hii imetulia, hawa ndio haswaaa wanadumisha MUUNGANO wa tanganyika na unguja, safi sana, wengine nao waige mfano!.
 
hongera zenu wapendanao.
lol sijui wote wamenunua nyumba za serikali
manake itabidi moja irudi lol
 
mi naomba kuuliza, hivi huyo kigoda hakuwa ameolewa tu? na huyo seif hatibu hakuwa ameoa naye?
naombeni muongozo please!
 
Nawapa Hongera zao

Naomba kuuliza hawa wabunge/mawaziri walioko bungeni (couples) ni kwa nini kusiwe na sheria ya kutokuwa na mke na mume humo- kama mke ni mbunge au waziri mume asiruhusiwe kuwa mmoja wa wabunge/ waziri?

Maana naona kama ni kuendekeza matabaka ya masikini na matajiri kama both mama na baba ni wabunge ina maana wanalipwa kila mtu haki yake (maposho na marupurupu) au wangekuwa wanalipwa portion moja bwana ah
 
Hongera Dr Aisha Kigoda na Mhe Seif Khatibu kwa kudumisha muungano wa Tanzania bara na Tanzania visiwani (Zanzibar)

Wanajamvi naomba kuelimishwa kuhusiana na penzi la hawa waheshimiwa.

[1] Mheshimiwa seif kwa umri alionao lazima atakuwa ana mke/wake na watoto.Je Dr kigoda atakuwa mke wa ngapi ?.

[2]Dr Kigoda ukimwangalia usoni hakosi watoto na pengine aliwahikuolewa au alizaa tu watoto nje ya ndoa.naelewa kuwa na watoto hakuzuii kuolewa au kuoa lakini si vibaya tukapata historia fupi ya hawa waheshimiwa kwasababu ni viongozi wetu.

[3]Waheshimiwa tayari wameshafunga ndoa au wako kwenye matayarisho ya kufunga ndoa ?.
 
Pamoja na kuwapongeza kwa hatua hiyo ila inaonekana muda mwingi unatumika Bungeni kukidhi haja binafsi hususan mshawasha wa kumpata mwenzake. Je yale ambayo hayajawekwa wazi tuite ufisadi fulani au??????????????????????????????
 
By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!

respect kwako kaka..tupo ukurasa mmoja...
 
Nawapa Hongera zao

Naomba kuuliza hawa wabunge/mawaziri walioko bungeni (couples) ni kwa nini kusiwe na sheria ya kutokuwa na mke na mume humo- kama mke ni mbunge au waziri mume asiruhusiwe kuwa mmoja wa wabunge/ waziri?

Maana naona kama ni kuendekeza matabaka ya masikini na matajiri kama both mama na baba ni wabunge ina maana wanalipwa kila mtu haki yake (maposho na marupurupu) au wangekuwa wanalipwa portion moja bwana ah

kwa kweli mkuu wazo lako ni zuri sana.angekuwa mmoja tu ndo anakamata allowance hiyo ingenoga sana.maana nadikiria kama itatokea baba ,na mama wote wabunge na mtoto mbunge wa viti maalum.duuhh si itakuwa balaaa
 
Kama ni kweli ni aibu mijitu mizima kuleta mambo ya mahabu bungeni,sasa bunge limekuwa bunge la mapenzi teh tehhhhh.Ah lazima nihamie sayari ya mars kama mwendo ndo huu
 
hii imetulia, hawa ndio haswaaa wanadumisha MUUNGANO wa tanganyika na unguja, safi sana, wengine nao waige mfano!.
tuko pamoja mkuu katika hili,kwa mwendo huu muungano utadumu milele..
 
Back
Top Bottom