Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
Hakuna lolote hao wanaendekeza sana ngono hapo mjengoni badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi. Kwanini maisha Dom yanapanda maradufu wakati wa Bunge? Na kwa nini kunakuwa na machangu wengi kipindi cha bunge? Hawafanyi kazi zao sawa sawa. Leo unasikia wanataka mfuko wa Jimbo pesa ambayo wewe na mimi unatozwa kodi tena bila huruma halafu hawa jamaa wanaitafuna wakidai ni haki yao na ukihoji unaambiwa una wivu wa kitoto au wivu wa kike ama wao wanasema wanafanya kazi kubwa . Wengine wakiona wamezidiwa wanaomba ulinzi wa ziada. Nakwambia iko siku hata hao wanaowakimbilia watawatosa sijui watakimbilia wapi?
Aisha ana Advanced Diploma ya Clinical Medicine, na kwa mujibu wa Muundo wa Utumishi wa Kada za Afya anatambuliwa kama Daktari Msaidizi (Assistant Medical Officer). MDs na AMOs wote wanatambuliwa kama madaktari.By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!
By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!
Nawapa Hongera zao
Naomba kuuliza hawa wabunge/mawaziri walioko bungeni (couples) ni kwa nini kusiwe na sheria ya kutokuwa na mke na mume humo- kama mke ni mbunge au waziri mume asiruhusiwe kuwa mmoja wa wabunge/ waziri?
Maana naona kama ni kuendekeza matabaka ya masikini na matajiri kama both mama na baba ni wabunge ina maana wanalipwa kila mtu haki yake (maposho na marupurupu) au wangekuwa wanalipwa portion moja bwana ah
tuko pamoja mkuu katika hili,kwa mwendo huu muungano utadumu milele..hii imetulia, hawa ndio haswaaa wanadumisha MUUNGANO wa tanganyika na unguja, safi sana, wengine nao waige mfano!.