Mawaziri hawa ni mizigo au Wizara zimewazidi kitaaluma na uzoefu?

Mawaziri hawa ni mizigo au Wizara zimewazidi kitaaluma na uzoefu?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Dr. Faustine Ndugulile naamini amepwaya pale mawasiliano, kasi ya mabadiliko ya teknologia ukilinganisha na uwezo wake kiubunifu kwenye ili eneo amepwaya kabisa.

Waziri wa michezo Bashungwa wizara yake imemkalia vibaya. Hana hoja au maelekezo mapya yakimkakati kwenye sekta ya michezo. Ukiona DC anakuja kuweka mazingira ya uwanja yawe na hadhi yakimataifa na Waziri yupo tambua uwezo na ubunifu haupo. Lakini pia TFF na bazara la michezo vimekaa kama vyombo visivyo chini ya wizara yake. Basata nayo kifo Cha mende, magazeti na vyombo vya habari vinasubiri maelekezo ya Rais, je nafasi ya waziri Ni ipi wizarani Kama majukumu haya yanamsubiri DC au Mhe. Rais?

Palamagamba Kabudi, ni mbobezi wa sheria lakini si mtu sahihi kwenye wizara ya katiba na sheria. Msimamo na mambo aliyowaaminisha Watanzania for 5yrs si Yale anayopaswa kusimamia leo.

Anaona aibu na anashindwa atumie mbinu gani kuwaaminisha wananchi kwamba ubeberu ulitukwamisha. Atatumia mbinu gani kutuaminisha kwamba si muasisi wa sheria kandamizi.za nchi hii. Ni vigumu kufanikiwa Bora abaki mbunge wa kawaida Kama akina Bashiru.

Hawa ni baadhi ya Mawaziri ambao siwezi sema Ni mizigo ila wamekabidhiwa wizara ambazo zimegeuka mizigo kwao.
 
Kwa Ndugulile na Bashungwa naweza Kukubaliana na Wewe 99%, ila kwa Kabudi sikubaliani nawe kwani Kitaaluma hapo alipo ni mahali pake tofauti na hao Wenzake.
 
Yule Wa Utumishi nae anapwaya watu wengi sana hawajapanda madaraja ama kubadilishiwa figa za mshahara wakati Mh.Rais aliahidi kutotaka madeni yatokanayo na mishahara. Mfano ktk halmashauri ya wilaya ya Kwimba watumishi wote waliooandishwa vyeo itabidi waandike madai kwa kutobadilishiwa ngazi za mishahara Kwa mwezi Wa 6
 
Mwingulu Wizara ya miamala ni mahali pake kabisa, aachwe hapohapo.
Hana lolote kwani hiyo wizara ni mala yake ya kwanza kuwa hapo??nini cha zaidi alichokifanya? Ila kwa Afrika hatuna haja ya kuwalaumu sana kwani kwenye wizara zao unatakiwa utumie 10% ya uwezo wako, mengine ni maelekezo toka kwa aliyekuteua hata kama kitu hicho hana uelewa nacho.
 
Dr. Faustine Ndugulile naamini amepwaya pale mawasiliano, kasi ya mabadiliko ya teknologia ukilinganisha na uwezo wake kiubunifu kwenye ili eneo amepwaya kabisa.
AISEEE, wewe ungefanya nini kwa wakati huo aliokaa hapo?

Katika mawaziri ambao ukitazama tu hata wanavyoonyesha kujiamini, mmoja ni huyo Ndungulile. Hebu mfananishe na yule kichekesho aliyekuwa Utalii, nani yule..., Gwangwala?
Huyu Madilu ni waziri tena wizara nyeti kabisa, anajuwa nini yule? Ulishamsikia akisema kitu nawe ukaamini anajuwa anachoongelea?

Utalii yupo nani sasa, yule aliyetaka kuhamishia ofisi Chato? Hao ndio mawaziri unaodhani wana uwezo?

Uwekezaji, sijui nayo ni wizara siku hizi? Kuna waziri huko? Afya kuna waziri na naibu wake? Vichekesho vile nao unawaita mawaziri?

Ngoja nikwambie wizara zilizo na mawaziri: Kilimo, wote wawili, waziri na msaidizi wake, hao ni mawaziri.

Ardhi, waziri ni waziri mwenyewe, msaidizi, basi ni msaidizi tu

Kalemani ni waziri, hata bila kumhusisha na Mwenda zake

Tamisemi sasa hivi kuna waziri

Biashara..., Mkumbo? Anaelewa mambo, hata kama tabia nyingine ni za mashaka.
 
Back
Top Bottom