Mawaziri Jenister Mhagama na Damas Ndumbaro hawana upendo kwa wafanyakazi kabisa

Kitendo kilichofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani ni cha kizalendo hatuwezi kulipana mishahara wakati kuna miradi mingi ya maendeleo haijaisha.
Wewe nawe! Kujali mamiradi kuliko kujali hali ngumu za waTZ ndiyo uzalendo! Ulijifunza wapi hilo?
 
May be! Lakini wewe hujiulizi why tangu awe pale Utumishi mishahara haijapanda?
 
Hao akina ngumbaro ni watu waliojaa ubinafsi na roho mbaya kwa wengine kwa sababu wao wanakula mishahara minono na kuogelea kwenye miposho ya hapa na pale, nyumba bure, usafiri bure, umeme na maji bwerere.
 
Wanaoangusha wizara ya utumishi ni waandamizi hasa maafisa utumishi.Kwa mfano kwenye zoezi Hilo la kupandisha vyeo watumishi, baadhi ya maafisa utumishi hawajaweka wazi orodha ya watumishi wanaostahili kupandisha vyeo na madaraja, lengo kuu ni kutengeneza urasimu.

Ingependeza Sana katibu mkuu utumishi na waziri watoe amri kwa maafisa utumishi wote kuweka wazi majina yote ya wanaostahili kupandishwa ili wale wote wanaostahili wawepo.Nje ya hapo ni shida.
 
Mleta mada sijaelewa hebu nieleweshe hapa kidogo:-

"Kuna uhusiano gani kati ya watu wanaotoka Ruvuma NA kujali maslahi ya wafanyakazi?

Unless otherwise utuombe msamaha watu wa Ruvuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…