Mawaziri Jenister Mhagama na Damas Ndumbaro hawana upendo kwa wafanyakazi kabisa

Mawaziri Jenister Mhagama na Damas Ndumbaro hawana upendo kwa wafanyakazi kabisa

Tuendelee kula mtori nyama zipo chini, Kimsingi hawa wakubwa hawapo kwa ajili ya kupigania maslahi ya watu wenye vipato vidogo badala yke wapo kwa ajili ya familia zao. ACHA MUNGU AENDELEE KUTUSIMAMIA. Tuzidi kumuomba na kumtumainia.
Yaani unamaanisha atawaondoa mmoja haya mabwenyenye?
 
kwa mgogoro alio usababisha Mei Mosi, waziri na naibu wake walipaswa waachie ngazi mara moja.
kwa kiasi kikubwa hawa ndio wamesababisha uchonganishi.
 
Kw Taarifa tu ni kua Huyo Jenista Mhagama ni mmoja ya watu incompetent kuwahi kua nao, ni wale hoyahoya ukijumlisha na elimu yake ya msondo, simply ni team vigelegele na hajawahi kusimamia issue yoyote technical, recall issue ya kikokotoo alivyomnawisha yule director irene Isaka wa regulatory ya social security.

Upstairs kwake panamtosha yeye!
 
Ndiyo maana mikoa ya kusini imejaa watu maskini sn sababu ya aina ya watu wanaotoka kusini
 
Kwa miaka 6 Jensiter na Ndumbaro wamekuwa wakishikilia portfolios muhimu sana za kuangalia maslahi ya wafanyakazi. Hata hivyo mpaka sasa hamna chcochote cha kujivunia wanachoweza ongea kuhusu wafanyakazi. Jesnister tangu akute ile Wage Order ya mishahara ya watu wa sekta binafsi ya Mwaka 2013 hajawahi hata kuiongelea mahali.

Huyu mama na mwenzake Ndumbaro hawa-reflect kabisa roho nzuri za watu wa Ruvuma walizonazo. Sijui wamekuwaje hawa? Yaani bure kabisa! Na Mwenyezi Mungu awaangalie pamoja na nafasi zao zinazowapata kiburi wasije pata amani kamwe kwa matendo yao mabaya wakimaliza utumishi wa umma.

Ndumbaro mpaka ameingia Samia leo ndiyo anaona umihumu wa kuwalipa wa darasa la saba. Yaani wewe ni bendera fuata upepo tu - hufai pale utumishi. Na siku ukiondolewa ni lazima watumishi watapiga vigelegele! Ndumbaro ni msomi mzuri tu lakini hujali hata wale waliokumbwa na sakata la vyeti feki pia walihitaji kulipwa fedha zao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hawa watu walifanya kazi na Katiba ya Nchi inawapa haki ya kulipwa ujira wao. Serikali yenyewe ilikuwa dhaifu kuajiri wa vyeti feki lakini yenyewe imeshindwa kujiwajibisha kwa makosa iliyofanya. Nchi hii mjenga chuki sana sana. Ndiyo maana Kiongozi mkubwa wa nchi anafariki wananchi wanashangilia.

Hata kama mnafikiri walioshangilia ni wachache bado pia wana impact. Hamjiulizi mbona Nyere na Mkapa walipofariki hamna hata mtu mmoja alionekana kushangilia?

Acheni roho mbaya - madaraka ni ya kupita tu! Mngemshauri vema Rais leo wafanyakazi wangekuwa wanafurahi na familia zao!
Rekebisha kwenye kichwa cha habari!!

Ndumbaro anaeshughulika na maslai ya wafanyakazi ni Dr. Laurean Ndumbaro ambae ndie Katibu Mkuu wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na SIO Dr. Damas Ndumbaro ambae ni Waziri wa Utalii.

Rekebisha hilo jina hapo juu!!!!
 
Jenista anabebwa tu ila hana leadership potential yoyote ile yaani legacy yake ni kuwa kofia kwa kobe anakwenda kila anakokwenda Rais aliyepo madarakani yaani hana jipya kabisa.

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom