Wakuu,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene (Mb), amesema Mawaziri Watatu, akiwemo yeye, Waziri wa TAMISEMI, na Waziri wa Elimu wanatarajia kukutana na Umoja wa Walimu Wasio na ajira Tanzania (NETO) Machi 10, mwaka huu.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi 3, 2025 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Waziri na Wakuu wa Taasisi za Umma.
Amesema lengo la kukutana na umoja huo ni Kuwasikiliza, Kushauriana namna bora yakupata majawabu sahihi ya kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao
Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibu Umoja huo uliibuka na madai ya uwepo wa vitendo vya upendeleo na rushwa katika usaili wa nafasi za ajira za kada ya Ualimu Serikalini.
Hata hivyo pamoja na Waziri Simbachawene kutangaza kutaka kukutana nao kwa mara ya kwanza viongozi wa umoja huo akiwemo Mwenyekiti na Katibu walikamatwa na jeshi la polisi.