Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mkutano huo umeongozwa na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Musalia Mudavadi na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Mhe. Prof. Amon Murwira, umefayika Ikulu Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ngazi ya Mawaziri (Organ Troika) ya SADC Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mawaziri wa Ulinzi kutoka Nchi Wanachama wa EAC na SADC.
Mkutano huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC, utakaofanyika nchini tarehe 8 Februari 2025.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la EAC, Mhe. Musalia Mudavadi amesema mkutano huu wa pamoja umelenga kupata njia ya pamoja ya kutatua changamoto za usalama Mashariki mwa DRC, kwa manufaa ya DRC na Afrika kwa ujumla.
“Mkutano huu unaweza kupimwa kwa mtindo mzuri au mbaya kulingana na jinsi ulivyofanyika, lakini SADC na EAC zina sababu ya kufanya mkutano huu kwa pamoja, suala hili liko hapa mbele yetu ili liweze kutafutiwa namna bora ya kulitatua” alisisitiza Mhe. Mudavadi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC, Mhe. Prof. Amon Murwira amesema maono ya Waanzilishi wa SADC yalijikita katika kanuni za usawa na uhuru wa kila nchi, uadilifu na Umajumuhi wa Afrika. Na kuongeza kuwa Waasisi hao wa SADC walidhamiria kuwa na ukanda wenye amani na usalama ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa kanda.
Soma Pia: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo
Soma: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo
Attachments
-
publer-1738945466041.jpg80.9 KB · Views: 1 -
publer-1738945458159.jpg100.6 KB · Views: 1 -
publer-1738945463579.jpg37.5 KB · Views: 1 -
publer-1738945446989.jpg126.9 KB · Views: 1 -
publer-1738945449894.jpg79.3 KB · Views: 2 -
publer-1738945444533.jpg67.6 KB · Views: 1 -
publer-1738945441760.jpg96.6 KB · Views: 1 -
publer-1738945439081.jpg85.8 KB · Views: 2