Itakuwa kujidanganya kama taifa kudhani kuwa tuko vizuri.
Matumaini mapya yaliyoibuka baada ya SSH kuchukua nchi yamekwisha baada ya siku 100 ofisini.
Kama taifa tunayumba tokea kwenye corona hadi kwenye mustakabala kama taifa. Taifa limegawanyika hisia kali na munkari juu:
1. Kuhusiana na ugonjwa hatari wa Corona:
(a) Vinara wa misimamo ya awamu ile na Corona, chanjo yakiwamo mahusiano na WHO pia na mataifa mengine wangalipo serikalini.
(b) Kuna tofauti kubwa za kimtazamo kuhusiana na Corona baina ya watu, yakiwa ni madhara ya wazi yatokanayo na misimamo na propaganda za awamu ile.
(c) Athari za ugonjwa zinaendelea kuongezeka na watu wasio na hatia wanaendelea kufa.
(d) Tunapaswa sasa kama taifa kuzikumbatia tahadhari zote zilizokuwa zikibezwa katika awamu ile yakiwamo matumizi chanjo.
Ni wazi kuwa tunahitaji marubani wapya kama kweli tunayo nia ya dhati ya kuyaokoa maisha ya watu.
2. Mustakabala wetu kisiasa kama taifa:
(a) Umoja wetu uliokuwapo katika siku 100 za mwanzo za SSH haupo tena.
(b) Ukiukwaji wa wazi wa sheria na katiba wenye upendeleo, yakiwemo matumizi ya dola dhidi ya makundi mengine umeligawa tena taifa.
(c) Kubambikiziwa kesi kwa Freeman Mbowe kumeongeza mgawanyo chuki zaidi dhidi ya serikali.
Wasaidizi wasioweza kumsaidia rais kutuunganisha kama taifa, hawatufai.
3. Mustakabala wetu kiuchumi:
(a) Mwendelezo wa vigogo kutokulipa kodi, haukubaliki.
(b) Maongezeko ya kodi na tozo mbalimbali ndani ya kipindi cha ongezeko la UVIKO, hayakubaliki.
(c) Utaratibu wa gharama za matibabu ya UVIKO kuwa ni juu ya wahanga wa ugonjwa huu ambao ni janga la dunia, haukubaliki.
Manahodha wasioona umuhimu wa kila mtu kulipa kodi na kuwa ufumbuzi wenye wa haki kwenye majanga, hawatufai.
Mawaziri waliopo hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kumsaidia rais kutuunganisha.
Kama wao hawauoni umuhimu wa kuachia ngazi ili kumpa Mama SSH nafasi ya mwanzo mpya wa kuisafisha hali hii, na wafurushwe tu kwa maslahi ya taifa.
Ninawasilisha.