#COVID19 Mawaziri waachie Ngazi kutoa Nafasi kwa Mwanzo Mpya

Uko sahihi mkuu tunahitaji fresh faces kwa kweli, new faces,new vision,harmony

Haisaidii kuwafumbia macho watu hawa. Haisaidii kutokuwataja majina yao. Hawana mishipa ya aibu. Wanatuchukulia poa.

"Sitaona haya kumwonea haya mzembe" -- mwalimu Nyerere (rip).

Unajiuliza hivi Gwajima, Simbachawene, Sirro, Mwigulu na wenzao wanatuona je kweli?

Hatuna sababu ya kuona haya au kuogopa kuwataja kwa majina yao, kuwazodoa kwa unafiki wao, kuwazomea kwa njaa zao, kuwananga kwa ubinafsi wao uliopitiliza, kuwaonyesha kutokutufaa kwao nk.

Hii nchi ni yetu sote. Tunawajibika sote
kuona kuwa inaendeshwa kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia kwa mujibu wa katiba. Si kwa utashi wa mtu binafsi.

Hili si shamba binafsi la mtu yeyote!
 
Kwani unataka uteuliwe wewe? Achia mwenye kuwateua anajua cha kufanya

ID yako hii ya msa(h)ada ninaisoma vyema.



Hata hivyo nisiache kukupa makavu:

Nchi hii ni yetu sote wala si shamba binafsi la mtu.

"Sitaona haya kumwonea haya mzembe, mwizi, mbinafsi, asiyetufaa, mwongo, na wote namna hiyo" -- mwalimu Nyerere (rip).



Hawa hapa hawatufai na sababu zimeorodheshwa. Vipi, eewe ni mmoja wao au japo kuna jamaa yako?

1. Afya:



2. Mambo ya ndani:



3. Fedha na uchumi:



Au nasema uongo ndugu zangu?

Cc: BAK, Mwifwa imhotep
 

Braza j una vituko vingi sana...
 
Huku uko unazama huku tuko vizuri tutembee vifua mbere
 
Alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo, akaichezea. Sasa hawa jamaa wanamwadhibu. Na wameshaongeza mizizi yao kwenye system. Kwa sasa kuwatoa ni vigumu mno.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Beberu anasema "it's never too late." Waswahili nao hakubakia nyuma, "wajinga ndiyo waliwao." Kigugumizi cha nini?


Kimya chake kinafanya watu kuhitimisha kuwa labda yeye ndiye mwenye makando kanda zaidi. Anapoteza uungwaji mkono.

Siamimi kuwa kipo asichokijua. Itakuwa ni kutojitendea haki yeye mwenyewe.

Cc: Mshana Jr
 

Mkuu kwenye bandiko lako namba moja sioni waziri yoyote wa kuachia ngazi, ifahamike hapa kwetu uwaziri ni njia kuupata utajiri. Mfano Jenister Mhagama anaachia vipi uwaziri hata kama hana tija, yeye anapigania kipapai tu aendelee kukaa kwenye ulaji.

Mwigulu ndio huyo kumuelekeza mama wa kambo kibla, saa hii anatengeneza sinema za kuusaka urais akijifanya ana suluhu ya matatizo ya watanzania. Nakumbuka Magufuli alimfukuza uwaziri kwa kumtuhumu anafanya kampeni za kujijenga kisiasa kuusaka urais. Alichokifanya Mwigulu ni kwenda kuloga akarudishwa tena kwenye uwaziri. Sasa hivi wameshamshikia mama wa kambo chini, wanafanya watakavyo. Mama ameambiwa atulie pesa ikusanywe kwenye tozo, na Mwigulu ameanza matumizi kwa kuzunguka huko na huko kuendelea na kampeni zake za Urais.
 

Mkuu ninakubaliana na yote uliyoyaandika. Ila sina hakika kwa sehemu ya mwisho kwenye mada kama uliiona:




Suala la wao kutoka si kwa hiari yao peke yao. Bali hata kutoka kwa kufurushwa kama ikibidi, nayo ni sehemu ya mchezo vile vile.

Tunao wajibu uliotukuka wa kumsaidia SSH kuwaondosha watendaji kama hao. Yeye akiwa au hata asipokuwa sehemu ya uozo huo.


Nchi si kama shamba la mtu binafsi. Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba. Isitoshe kuna yaliyo mikononi mwetu kama wananchi:



Au nasema uongo ndugu yangu bwana Jumbe Brown?
 
Kwa huyu mama tayari kafail hana cha kubadili
 
Kwa huyu mama tayari kafail hana cha kubadili
Ila waswahili wanasema kawia ufike. It is never too late.

Mtu mzima akisema "samahani." Humaanisha fresh start. Hakuna cha kuongeza wala kupungua.
 
Kuna watu hawataki hilo

wao wanataka maandamano na drama tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…