Mawazo na mbinu za biashara

Mkuu unamawazo ambayo nimeyatafiti ni jinsi tu wewe unaamua kuingia vipi na unahitaji faifa baada ya muda gani.....

1: Kunabiashara ya nguo za kike mwanza (mtumba) unakuwa unachagua nguo mojamoja dar saa 10 usiku kinakuwa na mzigo wa moto sana...kwakuchagua nguo mojamoja basi unakuwa na uhakika wa kupata nguo zenye quality nzuri

2: Kunabiashara ya kufuga Noah kama dini inaruhusu hawa ukilima na mahindi ukayatumia kama chakula chao pamoja na chako utatoboa

3: Kufungua frame ya nafaka hii fanya sana mtaani aiseh utapiga sana pesa maana kilasiku utauza..nafaka kama maharage, mchele, unga (unanijua mahindi unasafari mwenyewe).

4: Biashara ya dagaa wa mwanza wale kuna uzi niliupitia wakasema kwa kuwatoa mwanza kuwaleta hapohapo mbeya unaweza piga pesa vizuri tu.... Hii sijajua imekaaje ila hizo 3 ninauhakika nazo mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii No3 nimeielewa vizuri sana kwasababu ni biashara ya uhakika na inaweza nifanya ku survive wakati nazowea mazingira ya kitaani..Hii No2 sijaielewa.."Noah" ni ninii mkuu

By the way Nakushukuru sana kwa mawazo kwan naamin naanza kupata cha kukifanyia kazi..shukran
 
fanya biashara ya nafaka mkuu na mafuta ya alizeti yawepo hapo....

Noah ni nguruwe mkuu wanalipa sana tena san..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
week mbili zinatosha,tenga hata laki tano then nenda sehemu yoyote porini ukachukue mazao ya nafaka uje kuuza mjini,utakuwa umepata mwanga kuhusu biashara za mazao,faida na changamoto zake
Nimekuelewa vizuri mkuu japo huwa wana vigezo vya hiyo likizo, Ndo mana kwenye Mada yangu nimesema kuna vikwazo na kero zinazofanya niweze kujitegemea mwenyew hivyo kuna shida kidogo
 
but mkuu hiyo kazi mbona ni nzuri tu,unaweza kufanya biashara huku ukiendelea kuifanya...kwanini usianzishe biashara then umwachie hata wife awe anaisimamia
but mkuu hiyo kazi mbona ni nzuri tu,unaweza kufanya biashara huku ukiendelea kuifanya...kwanini usianzishe biashara then umwachie hata wife awe anaisimamia
Wazo zuri sana...Lakin mkuu lengo ni kufikia uchumi wa kati au juu kabisa kwani kubaki kazini siyo suluhisho la umaskini wangu. Nilitaman sana nitumie wazo kama lako lakin najua unaelewa watumishi wa umma vile huwa wanapata vikwazo vingi pale wanapokuwa wakijaribu kujikwamua.

Kiukweli hata kama ningelipwa M10 bado hili wazo la kujitegemea nimekuwa nikiishi nalo hivyo nadhani ili nafsi ilizike ni bore nipambane ili niweze kununua mda wa watu wengine..I mean kutoa ajira kwa watu wengine...Najua ni kazi ngumu lakin nimejitoa mwili na roho mkuu..
Asante kwa Ushauri
 
sawa mkuu nimekuelewa,kuna uzi nimekutag wa maswala ya mobile money...ukipitia ule uzi unaweza jifunza kitu...kama niliona umesema upo mbeya...ukipambana pale kabwe stendi ukapata chumba hii mitaa yenye mzunguko mkubwa wa watu or ukipata chumba huku mwanjelwa sehemu yenye mzunguko mkubwa wa watu utapiga hela...

Issue ni kupata chumba tu,and sehemu kama iyo unafungua duka kubwa sana la simu vikienda sambamba na hizo huduma..but hakikisha ofisi una i design inakuwa na muonekano classic wa pekee

JOKES...Hakikisha kwenye ilo duka kama utakuwa na wafanyakazi unaajiri vitoto vyakike vizuri but smart kichwani kwa ajili ya kukusaidia kwenye mauzo
 
kama upo kanda ya ziwa, kwa biashara ya nafaka inaweza kukulipa namtoa mfano hai uku kahama kw sasa bei ya mche per kilo 800-1200 kasababu ya msimu wa mavuno na gunia la mpunga ni sh 30000-35000 ukinunua gunia zako kadhaa ukaja kuuzia mwezi sept-january ni bei isiyo pungua 90000 na kilo ya mchele huwa inauzwa mpaka 1600 kwa huku.sasa unaweza ona ilivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi gani ambayo huwezi kumove kirahisi? Endelea kuweka pesa afu omba uhamisho tu. Nasema hivyo kwa maana.. kuna Milengo miwili.. mlengo ambao hauamini kwenye ajira na ule unaoamini kwenye Ajira. Hivyo basi ili kujidhatiti lazima uanze biashara ungali kazini.

Hii itakusaidia kupunguza usumbufu hasa kwenye ofisi kadhaa za umma as ww ni mtumishi pia. Mim nimeomba kuhamishiwa Mtwara au Lindi ili nijikite kwenye biashara hzo. Naamini nitahamishiwa kutoka hapa Dom nilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…