Ni hivi mfano labda anataka kulima maharage...labda katika kulima kwake ametumia 5M..baada ya kuvuna mteja wa kwanza anakua yeye mwenyewe anajiuzia kwa bei halisi kama vile anavyotaka kuuza kwa wengine kwa bei ya jumla..hapo anakua ameaharudia pesa ya kulima na faida.
Baada ya hapo anayachukua yale mazao anapeleka kwenye duka lake la nafaka napo anauza kwa bei ya reja reja..akipata faida tayari anakua na msingi wa biashara mbili pasipo kuchanganya.
1.Anakua na msingi wa kulima na faida na soko la uhakika kwa sababu mteja wa kwanza wa mazao anayolima ni yeye mwenyewe.
2.Mbili akishajiuzia anakua anapeleka moja kwa moja dukani kwake kuuza kwa bei nafuu..
Hii system hata matajiri wakubwa wanaitumia sana,wanalima wenyewe na wajiuzia wenyewe kabla ya kumfikia mlaji
Nb:Mimi sio mfanya biashara najaribu kucreat idea tu hapo na Maharage ni kitu cha kwanza kukifanyia research Mungu akijaalia nitafanya hiyo biashara.
Sent using
Jamii Forums mobile app