mawazo tafadhali

mawazo tafadhali

mkia

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
582
Reaction score
508
story yangu inaaza hivi,
nakumbuka mnamo tarehe 09/06/2012 majira ya saa 10 jioni nilimpokea mchumba wangu kutoka Same na kuja huku nilipo Ruvuma. so tukawa tunaishi pamoja, nakumbuka siku ya tarehe 27/06/2012 yaani mwezi huo huo akanza kutapika tapika akawa anachagua chakula, dah mtu mzima nikagundua inaweza kuwa tayari, nikamuuliza mara ya mwisho siku zake alienda lini? akadai mwezi uliopita yaani ameanza tarehe 12/05/2012. sasa kiukweli nikawa sina imani isije katoka nayo huko aje kunibambikia. tarehe 30/06/ tukanunua kipimo na kujiridhisha kwamba tayari. tukalea mimba na mtoto akazaliwa, sasa ana miaka miwili ila kinachonishangaza mtoto hafanani na mimi kabisa kwa mfano mdogo tu ananywele ngumu kweli kweli ukilinganisha ukoo wetu wote tuna nywele laini. cha kushangaza ni kuwa baada ya kumtambulisha kwa ndugu, hasa mzee wangu akaniambia waswasi wake kuhusu mtoto kama ni damu yangu kiukweli naumia sana rohoni kuhusu hili.
nipo njia panda, kwa wenye kujua namna ya ku calculate tarehe za hatari za kupata mimba naombeni msaada kwa hili. je mtoto atakuwa wangu? na kuhusu DNA uwezo sina.
jioni njema na week end njema.
 
naombeni mawazo
 
Duh pole sana.
Yalishanikuta nikalea mimba na mtoto mpaka afafikisha mwaka na miezi mitatu ndipo nilipogjndua kuwa alikuwa anakula pesa zangu tu na za baba halisi wa mtoto. Ikawa mwisho wa story.
 
Mbona umechelewa sana kuomba ushauri? Mtoto ana miaka miwili, any way, huhitaji DNA, maelezo tu yanaonesha huyo si mtoto wako m-bane vizuri huyo 'mkeo' atakueleza tu baba wa mtoto!
 
kila nikiwaza juu ya hili naumia sana, some time nauchuna na sijawahi mwambia hii kitu, nahitaji nifanye uchunguzi wangu na kukusanya ushahidi ili maamuzi yawe sahihi. kwani muda tuliokaa nae ni mrefu na mtoto kanizoea sana mpaka muda mwingine nasikia faraja. naogopa kumwacha bila ushahidi pia isije nimempotezaea mda wake na heshima kwa wazazi wake kila kitu nimesha fanya barua ya posa na mahari kinachosubiriwa ni ndoa tu. naogopa kufunga ndoa tena ya kikristo halafu baadae tukaachana kisa mtoto si wangu nitapata shida kufunga nyingine kama mnavyojua ndoa za kikristo ukifunga ndo basi tena mpaka mwenzio ametangulia mbele za haki ndo ufunge tena.
 
Muulize vizuri....hakuna mimba za hivyo....ulipaswa kumuuliza dokta je mimba ilikuw ya mda gani?
na siku mtoto alizaliwa ni ipi?
dalili zote huyo mtoto si wako
 
Kuna wimbo wa Lucky Dube ngoja niiutafute nikuwekeeee hapa. Nimeumizwa sana sana na story yako
 
"You Got No Right"

[Woman:]
I got lonely sometime
You were gone and left
Like you always do
You were never there
When I needed some care
You were never there when I needed somebody to talk to
Somebody came and took your place.

[Man:]
Oh! Baby
Somebody took my place
In your heart I can say
I'm used to it
By now, 'cause it happens all the time
That is one test I always fail
But one thing my heart can't
Understand... who's gonna take
The place of this boy in my heart
We used to play together,
Do everything together,
But now what am I gonna say

[Chorus:]
You've got no right
To call me father
I've got no right
To call you son,
You got no right to talk to me
I've got no right to talk to you
Even though I try so hard
To be strong, but it hurts inside.

[Woman:]
As I pack my bags
To go now baby I thought
I could share this with you
The next time you fall In love
Treat your woman right
Remember that her place
Is not only in the Kitchen
All she needs is tender
Loving care.
 
Ukisachi huo wimbo utakuta mpangilio mzuri naona hapo nimekosea. Ni wimbo ambao huwa nikiwiimba unanikumbusha mbali sana
 
mtoto alizaliwa tarehe 01/03/2013.
 
asee kibao bomba sana
 
Kitu chochote ukishakitilia shaka lazima utakiona kina kasoro.
 
Kama si wako mbona alizaiwa karibia na miezi kumi anaweza kuwa wakwako huyi
 
tangu umempokea mlifanya mandingo lini?
yani tarehe ngapi?
na je mtoto alitimiza miezi tisa? maana hapo yote yanawezekana
 
Duh pole sana.
Yalishanikuta nikalea mimba na mtoto mpaka afafikisha mwaka na miezi mitatu ndipo nilipogjndua kuwa alikuwa anakula pesa zangu tu na za baba halisi wa mtoto. Ikawa mwisho wa story.

uligundua kwa njia gani ungetupa ujuzi ndugu tukajifunzia kwako
 
Roho isikuume mkuu hakuna kisichofa,mlee kwa mapenzi na matunda yake utakuja kuyaona,damu yako anaweza asikufae huyo wakulea akakufaa..
 
mandingo tulifanya siku hiyo hiyo
 
mandingo tulifanya siku hiyo hiyo

kama umzunguko wake upo sawa. kati ya tarehe 30/6 mpaka 6/7 ndio mimba ingekubali bila tatizo.
sasa tarehe 27/6 sio mbali sana na 30/6 japo inaleta mashaka kidogo.
 
uligundua kwa njia gani ungetupa ujuzi ndugu tukajifunzia kwako

Mtoto alipozaliwa alileta vielelezo kutoka hospitalini na kuniambia nitengeneze cheti cha mtoto. Sikuwa na haraka lamini yeye ndio akawa na msukumo kwamba nikatengeneze cheti. Tatizo likawa kwenye jina la mtoto. Yeye halitaki jina nililompa mtoto akawa anamwita jina lingine. Tuligombana sana juu ya hilo lakini nikasema basi mi cheti nitakitengeneza kwa jina lile la kwangu. Nikakitengeneza lakini alitaka kubaki na cheti nikamkatalia. Tukaendelea kuishi nikimpatia mahitaji ya mtoto mpaka mtoto alipofikia meize nane akanjambia kuwa kuna sindano mtoto anatakiwa kudungwa lakini mahitaji ni pamoja na cheti cha mtoto. Nikampati. Mtoto alipofikisha umri wa mwaka na miezi mitatu nilimtembelea nikamfanyia manunuzi makubwa ya mavazi. Siku ya tatu alinipigia simu akiwa njiani anampeleka mtoto hospitali. Sikuwa na imani na ile nikaamua kumfuatilia kwa nyuma hadi hospitalini bila yeye kujua. Nilipofika hospitali akanitumia sms kuwa anadaiwa pesa nyingi za matibabu ya mtoto. Nilisimama nikamtokea na kumaambia naomba vilelezo hivyo. Cha kushangaza alikataa kunipa chochote mpaka akaondoka. Baada ya hapo nikaenda kwenye dirisha la malipo kuhakiki madai hayo.
Hapo ndipo ugunduzi ulipotokea. Majina niliyouliza yote hayakuwepo kwenye watu aaliopatiwa huduma siku ile. Nikasema lile jina alilomwita nikalipata lakini nina la baba sj langu. Sikuamini.
Siku ya tatu nikaenda tena hospitalini maana anadai mtoto alilazwa, sikumkuta. Nilipoilizia kumbukumbu zake nikakuta jina la baba wa mtoto na sirname. Nikawa nimemaliza utafiti. Nimampigia nakuuliza kisa cha kunidanganya muda wote akawa hana jibu. Ukawa mwisho mawasiliano. Wala hapakuwa na haja ha DNA test.
 
naomba kuuliza, tupeane elimu kidogo, hivi mwanamke anapata kuona dalili kama kichefuchefu n.k ujauzito unapofikisha mda gani?
 
Back
Top Bottom