SoC02 Mawazo ya biashara hapa(hasa kwa wajasiliamali)

Stories of Change - 2022 Competition

GoJeVa

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
41
Reaction score
60
PATA MAWAZO YA BIASHARA HAPA(HASA KWA WAJASILIAMALI).

Andiko la leo, nitaongelea kuhusu biashara mbalimbali ambazo mtu mwenye mtaji uwe mkubwa au mdogo anaweza kuwekeza. Hivyo jongea katika huu ukurasa upate au uongeze maarifa juu ya biashara mbalimbali. Nitaanza kwa kuorodhesha biashara hizo huku nikitoa maelezo mafupi kwa kila biashara…..karibuni..!!!!!

1. Biashara ya miamala ya kifedha, kama vile M-pesa, Halopesa, Airtel money, Tigo pesa na uwakala wa kibenki kama NMB wakala au CRDB wakala.

Ili uanzishe biashara hii, ni lazima uwe na laini za mitandao ya simu ambazo zitakuwezesha kufanya miamala ya kifedha kama wakala wao. Ili upate laini hizo kuna njia mbili ambazo unaweza kuzitumia, njia ya kwanza ambayo ndio inashauriwa ni kuwa na TIN namba na leseni ya biashara ambazo ukipeleka kwenye maduka ya hayo makampuni ya simu utapata laini hizo(TILL) ambazo zitasoma jina lako na hivyo itakuwa na usalama mkubwa.

Njia ya pili ya kupata laini hizo ni kununua kwa mtu, njia hii sio salama sana na haishauriwi kwa sababu mtu mwenye hizo laini baada ya kukuuzia bado zitaendelea kusoma jina lake na pia mtu huyo anaweza kwenda KUSWAPU na kuzifanya ziendelee kuwa zake. Hivyo ni vizuri uwe na TIN namba na leseni ya biashara ili upate TILL zenye jina lako.

Katika hii biashara, faida hupatikana pale unapofanya miamala na hiyo faida unapewa kila mwisho wa mwezi. Hivyo unapofanya miamala mingi faida pia huwa kubwa, cha kuzingatia katika hii biashara kuwa sehemu nzuri ambayo utaweka biashara yako, angalau pawe na watu wengi.

NCC.png

Chanzo cha picha: mtandaoni.

2. Kilimo na ufugaji.
Kilimo na ufugaji pia ni biashara nzuri ambayo mtu unaweza kufanya. Unaweza kufuga mifugo mbalimbali kama vile; Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata, Samaki na mingineyo. Vilevile, katika kilimo mtu unaweza kulima mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

nc.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

3. Kufungua banda la chakula(Chipsi au Mgahawa).
Uzuri wa biashara hizi za vyakula, ni kuwa mpishi mzuri na kutafuta eneo zuri kibiashara. Mara nyingi chakula kikiwa na muonekano mzuri na radha nzuri ni rahisi kupata wateja wengi. Hivyo kwa wajasiliamali hili pia ni wazo zuri ambalo unaweza kulitumia.

n.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

4. Kufungua bucha au duka la kuuza samaki wabichi.
Katika biashara ya kuwa na duka la kuuza samaki wabichi kitu cha muhimu sana ni kuwa friza ambalo litasaidia samaki kukaa kwa muda mrefu.

n.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

5. Kufungua saluni ya kike, kupamba maharusi au kufungua saluni ya kiume.
Biashara hii pia ni nzuri, ila kitu cha msingi kama unataka kufanya mwenyewe bila msimamizi inabidi ujifunze hii stadi. Yaani namaanisha ujifunze ufundi wa kwenye saluni iwe ya kike au kiume. Kuna baadhi ya saluni za kike ili ujifunze unaambiwa utoe shilingi elfu hamsini kwa kila mwezi ambapo utakaribishwa hapo saluni na kufundishwa kila kitu yaani kupamba mtu, kusuka na ufundi wote wa kwenye saluni za kike.

n.png

Chanzo cha picha: mtandaoni.

6. Kufungua sehemu kwa ajili ya kuosha magari au pikipiki.

n.png

Chanzo cha picha: mtandaoni.

7. Kufungua ofisi kwa ajili ya kutengeneza vipindi vya televisheni au redio.
Hili wazo katika nchi yetu ya Tanzania kuna watu wamelifanyia kazi na wana ofisi hizo. Yaani hapa unaanzisha ofisi na kutengeneza vipindi hivyo vya televisheni au redio na kuwauzia wamiliki wa hivyo vyombo ukitengeneza vipindi vizuri na kwa ubunifu ni rahisi kuuza kazi zako.

8. Kufungua ukumbi wa kuonesha ligi mbalimbali za mpira wa miguu, kama vile ligi ya Tanzania bara, ligi ya uingereza, ligi ya hisipania na michezo mingine.

9.Kufungua duka la kuuza dawa za binadamu(pharmacy).

n.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

Biashara hii ina faida kubwa sana hasa ukiwa kwenye eneo zuri kibiashara. Ukiwa umesomea hii taaluma ya madawa inakuwa ni vizuri zaidi.

10.Kufungua sehemu za kupaki magari au pikipiki, hii inafaa zaidi sehemu za mijini.

MAWAZO YA BIASHARA YAPO MENGI SANA, HAPA CHINI NITAORODHESHA TU BILA KUTOA MAELEZO MAREFU.

11. Kuanzisha kampuni ya ulinzi.

12.Kuanzisha Kampuni ya kuzoa takataka au kuwa na kukodisha gari la kunyonya maji taka.

13.Uvuvi.
Hapa unanunua nyavu, boti, ngalawa au mitumbwi na kuajiri wavuvi ambao watakuwa wanavua na wewe unasubiri watoke majini na kuangalia wamepata samaki kiasi gani, baada ya hapo mnauza samaki na kufanya mgao kutokana na walivyopata.

14.Udalali wa vitu mbalimbali.

15. Kuwa na bustani ya kuuza maua au duka la kuuza maua.

16. Duka la kuuza mboga za majani Au genge la kuunza mahitaji ya nyumbani kama vile; nyanya,vitunguu,karoti,pilipili hoho na vinginevyo.

17. Duka la kuuza asali.

18.Kutengeneza kampuni ya kutengeneza matofali ya simenti(tofali za block).

19.Kuuza mbao.

20.Kukodisha viti, maturubai na kujenga majukwaa kwenye sherehe na matukio mbalimbali.

21.Kuwa fundi simu au kompyuta. Kumbuka ili uwe fundi lazima ujifunze.

22.Kuuza magodoro.

23.kuwa na duka la kuuza nguo.

24.Kuwa na bar. Kumbuka kreti moja ya bia faida yake ni zaidi ya elfu nne mia tano.

25. Kuwa na duka la nafaka, mfano; mchele,ngano, mahindi na nafaka zinginezo.

26.Kufungua duka la kuuza vifaa vya majumbani kama vile; sahani,vikombe,vijiko,chupa za chai na vinginevyo.

27.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi(gym).

n.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

28.Kununua magari yalitumika(used) na kuyauza tena baada ya kuyafanyia marekebisho.

29.Kuanzisha duka la mahitaji ya nyumbani kama vile; sabuni,sukari na vinginevyo.

30.Kuanzisha duka la kuuza spea za magari,pikipiki au baiskeli.

31.Kuanzisha duka la kuuza vipodozi,mafuta ya kupakaa na manukato.

31.Kufungua choo cha kulipia hasa sehemu za mijini.

32. Kujenga nyumba za kupangisha.

33.Kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha(mikopo).

34.Kuanzisha mini supermarket(supermarket ndogo).

n.jpg

Chanzo cha picha: mtandaoni.

35. Kuanzisha hardware.
36. Kuanzisha duka la kuuza vinywaji kama vile; pombe(K-vant,konyagi), mvinyo.

Hayo ni baadhi ya mawazo machache ya biashara ambayo kwa leo nimeyaleta kwenu.

AHSANTENI.
 
Upvote 5
HUDUMA : FASTA & PROFESIONAL
- KUSAJILI KAMPUNI 125,000/-
-KUSAJILI JINA LA BIASHARA 10,000/-

+HESABU ZA KAMPUNI & KODI - (AUDITED REPORT)
+TRA RETURN
+VAT RETURN
+SDL
+PAYE
=BRELA RETURN

PIGA/WATSUP SASA: 0788 104 228
 
Attachments

  • 20221102_102733.png
    20221102_102733.png
    300.1 KB · Views: 90
PATA MAWAZO YA BIASHARA HAPA(HASA KWA WAJASILIAMALI).

Andiko la leo, nitaongelea kuhusu biashara mbalimbali ambazo mtu mwenye mtaji uwe mkubwa au mdogo anaweza kuwekeza. Hivyo jongea katika huu ukurasa upate au uongeze maarifa juu ya biashara mbalimbali. Nitaanza kwa kuorodhesha biashara hizo huku nikitoa maelezo mafupi kwa kila biashara…..karibuni..!!!!!

1. Biashara ya miamala ya kifedha, kama vile M-pesa, Halopesa, Airtel money, Tigo pesa na uwakala wa kibenki kama NMB wakala au CRDB wakala.

Ili uanzishe biashara hii, ni lazima uwe na laini za mitandao ya simu ambazo zitakuwezesha kufanya miamala ya kifedha kama wakala wao. Ili upate laini hizo kuna njia mbili ambazo unaweza kuzitumia, njia ya kwanza ambayo ndio inashauriwa ni kuwa na TIN namba na leseni ya biashara ambazo ukipeleka kwenye maduka ya hayo makampuni ya simu utapata laini hizo(TILL) ambazo zitasoma jina lako na hivyo itakuwa na usalama mkubwa.

Njia ya pili ya kupata laini hizo ni kununua kwa mtu, njia hii sio salama sana na haishauriwi kwa sababu mtu mwenye hizo laini baada ya kukuuzia bado zitaendelea kusoma jina lake na pia mtu huyo anaweza kwenda KUSWAPU na kuzifanya ziendelee kuwa zake. Hivyo ni vizuri uwe na TIN namba na leseni ya biashara ili upate TILL zenye jina lako.

Katika hii biashara, faida hupatikana pale unapofanya miamala na hiyo faida unapewa kila mwisho wa mwezi. Hivyo unapofanya miamala mingi faida pia huwa kubwa, cha kuzingatia katika hii biashara kuwa sehemu nzuri ambayo utaweka biashara yako, angalau pawe na watu wengi.

View attachment 2338100
Chanzo cha picha: mtandaoni.

2. Kilimo na ufugaji.
Kilimo na ufugaji pia ni biashara nzuri ambayo mtu unaweza kufanya. Unaweza kufuga mifugo mbalimbali kama vile; Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata, Samaki na mingineyo. Vilevile, katika kilimo mtu unaweza kulima mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

View attachment 2338104
Chanzo cha picha: mtandaoni.

3. Kufungua banda la chakula(Chipsi au Mgahawa).
Uzuri wa biashara hizi za vyakula, ni kuwa mpishi mzuri na kutafuta eneo zuri kibiashara. Mara nyingi chakula kikiwa na muonekano mzuri na radha nzuri ni rahisi kupata wateja wengi. Hivyo kwa wajasiliamali hili pia ni wazo zuri ambalo unaweza kulitumia.

View attachment 2338106
Chanzo cha picha: mtandaoni.

4. Kufungua bucha au duka la kuuza samaki wabichi.
Katika biashara ya kuwa na duka la kuuza samaki wabichi kitu cha muhimu sana ni kuwa friza ambalo litasaidia samaki kukaa kwa muda mrefu.

View attachment 2338108
Chanzo cha picha: mtandaoni.

5. Kufungua saluni ya kike, kupamba maharusi au kufungua saluni ya kiume.
Biashara hii pia ni nzuri, ila kitu cha msingi kama unataka kufanya mwenyewe bila msimamizi inabidi ujifunze hii stadi. Yaani namaanisha ujifunze ufundi wa kwenye saluni iwe ya kike au kiume. Kuna baadhi ya saluni za kike ili ujifunze unaambiwa utoe shilingi elfu hamsini kwa kila mwezi ambapo utakaribishwa hapo saluni na kufundishwa kila kitu yaani kupamba mtu, kusuka na ufundi wote wa kwenye saluni za kike.

View attachment 2338117
Chanzo cha picha: mtandaoni.

6. Kufungua sehemu kwa ajili ya kuosha magari au pikipiki.

View attachment 2338120
Chanzo cha picha: mtandaoni.

7. Kufungua ofisi kwa ajili ya kutengeneza vipindi vya televisheni au redio.
Hili wazo katika nchi yetu ya Tanzania kuna watu wamelifanyia kazi na wana ofisi hizo. Yaani hapa unaanzisha ofisi na kutengeneza vipindi hivyo vya televisheni au redio na kuwauzia wamiliki wa hivyo vyombo ukitengeneza vipindi vizuri na kwa ubunifu ni rahisi kuuza kazi zako.

8. Kufungua ukumbi wa kuonesha ligi mbalimbali za mpira wa miguu, kama vile ligi ya Tanzania bara, ligi ya uingereza, ligi ya hisipania na michezo mingine.

9.Kufungua duka la kuuza dawa za binadamu(pharmacy).

View attachment 2338130
Chanzo cha picha: mtandaoni.

Biashara hii ina faida kubwa sana hasa ukiwa kwenye eneo zuri kibiashara. Ukiwa umesomea hii taaluma ya madawa inakuwa ni vizuri zaidi.

10.Kufungua sehemu za kupaki magari au pikipiki, hii inafaa zaidi sehemu za mijini.

MAWAZO YA BIASHARA YAPO MENGI SANA, HAPA CHINI NITAORODHESHA TU BILA KUTOA MAELEZO MAREFU.

11. Kuanzisha kampuni ya ulinzi.

12.Kuanzisha Kampuni ya kuzoa takataka au kuwa na kukodisha gari la kunyonya maji taka.

13.Uvuvi.
Hapa unanunua nyavu, boti, ngalawa au mitumbwi na kuajiri wavuvi ambao watakuwa wanavua na wewe unasubiri watoke majini na kuangalia wamepata samaki kiasi gani, baada ya hapo mnauza samaki na kufanya mgao kutokana na walivyopata.

14.Udalali wa vitu mbalimbali.

15. Kuwa na bustani ya kuuza maua au duka la kuuza maua.

16. Duka la kuuza mboga za majani Au genge la kuunza mahitaji ya nyumbani kama vile; nyanya,vitunguu,karoti,pilipili hoho na vinginevyo.

17. Duka la kuuza asali.

18.Kutengeneza kampuni ya kutengeneza matofali ya simenti(tofali za block).

19.Kuuza mbao.

20.Kukodisha viti, maturubai na kujenga majukwaa kwenye sherehe na matukio mbalimbali.

21.Kuwa fundi simu au kompyuta. Kumbuka ili uwe fundi lazima ujifunze.

22.Kuuza magodoro.

23.kuwa na duka la kuuza nguo.

24.Kuwa na bar. Kumbuka kreti moja ya bia faida yake ni zaidi ya elfu nne mia tano.

25. Kuwa na duka la nafaka, mfano; mchele,ngano, mahindi na nafaka zinginezo.

26.Kufungua duka la kuuza vifaa vya majumbani kama vile; sahani,vikombe,vijiko,chupa za chai na vinginevyo.

27.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi(gym).

View attachment 2338140
Chanzo cha picha: mtandaoni.

28.Kununua magari yalitumika(used) na kuyauza tena baada ya kuyafanyia marekebisho.

29.Kuanzisha duka la mahitaji ya nyumbani kama vile; sabuni,sukari na vinginevyo.

30.Kuanzisha duka la kuuza spea za magari,pikipiki au baiskeli.

31.Kuanzisha duka la kuuza vipodozi,mafuta ya kupakaa na manukato.

31.Kufungua choo cha kulipia hasa sehemu za mijini.

32. Kujenga nyumba za kupangisha.

33.Kuanzisha kampuni ya kukopesha fedha(mikopo).

34.Kuanzisha mini supermarket(supermarket ndogo).

View attachment 2338141
Chanzo cha picha: mtandaoni.

35. Kuanzisha hardware.
36. Kuanzisha duka la kuuza vinywaji kama vile; pombe(K-vant,konyagi), mvinyo.

Hayo ni baadhi ya mawazo machache ya biashara ambayo kwa leo nimeyaleta kwenu.

AHSANTENI.
Iko njema
 
Back
Top Bottom