Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
''..ulianza lini kutoamini…”
“nilipoanza kusomasoma na kusitasita”
Nagona
Kezilahabi, ni mtu anayeona umuhimu wa kujisomea vitabu, katika kila kitabu chake lazima akupe picha ya mtu kusoma kitabu. Na namna mtu husika anavyobadili fikra zake kupitia usomaji wa vitabu.
Katika hii dunia, watu wanaoishi katika ndoto (In Kezilahabi’s voice) ni wale ambao misingi ya fahamu zao imejengwa katika ujinga, hili swala amelielezea katika Nagona kuwataja wale watu ambao hawali chakula (knowledge), watu ambao hula matumaini yanayotokana na ndoto zao.
Hili ndio swala ambalo hata sasa linaendelea kwa tulio wengi, tunaishi kwa kula matumaini, na tunayatafuta matumaini ambayo misingi yake ni wishful thinking (Visima vya ndoto). Ni wachache wanaovuka na kuingia kwenye ukurasa mwingine wa kuiona dunia, ni kama hivi sasa watu husoma Zaidi vitabu vya how to be rich, how to start a business, how to be successful, how to, how to… matumaini, ni baada ya kuchoshwa na uwepo.
Mtu hubadilika kwa sababu tofauti tofauti lakini kupata msimamo na kitu mtu anachoweza kukisimamia ni kupitia kufundishwa vitu kiundani. Kuvifahamu vitu kiundani ni kwa njia kahdaa moja wapo ni kupata mwalimu “Mentor” njia nyingine ni kujitupa maktaba kusoma vitabu vya mada husika.
Kwenye Dunia uwanja wa fujo, utamuona kijana Tumaini alivyobadili fikra zake juu ya maisha baada ya kubadilisha aina ya vitabu anavyovisoma.
Sio kila kitau kinaweza kujenga mtazamo chanya kwa mtu, lakini vitabu vina athari kubwa kwa asomaye. Tumaini ameonyeshwa kama mtu aliyekuwa anapenda Zaidi kusoma kuhus mapenzi, vitabu kama the garden nk. Kuwa na picha za wanawake waliokuwa uchi chumbani kwake nk. Lakini baadae alianza kusoma vitabu tofauti na vya mapenzi ndipo akaanza kupenda fikra na kweli alibadilika.
Tabia ya usomaji imeonyesha kwenye Nagona, wakati ameenda kuungama kwa Paroko (Ni kawaida kwa Kezilahabi kuzifanyia istazahi dini) sababu aliyoitoa kama mwanzo wa kutoamini kwake, ni kusoma soma na kusitasita (Doubt). Hiyo yote ni katika juhudi za Kezilahabi kuelezea athari za usomaji kwa msomaji.
Kwenye Kichwamaji kinaonyesha athari za usomaji kwa Kazimoto, ambaye amekuwa akisoma kitabu chake cha maisha kama alivyosema. Kitu kilimfanya awe anafikiria sana na kuwa tofauti na watu na kuiona dunia kivingine. Kitabu kilichokuwa na falsafa,…tusiwe na haraka katika kuamua, tamaa imemuongoza mwanadamu katika mambo mengi mazuri, na fikra imemuongoza mwanadamu katika mambo mengi mabaya…”
Kwenye Mzingile amemtaja kichaa anayesoma Das Capital na vitabu vingine ambavyo hakuvitaja, yote ni kuonyesha usomaji una athari fulani kwa wasomaji wake. Na msomaji huwa na matokeo ya vitabu asomavyo.
Usisitizaji aliofanya Kezilahabi katika vitabu vyake ni sawa na wanaofanya mataifa ya magharibi kupitia movies zao, ambazo zimekuwa na sera ya kuweka scenes za usomaji wa vitabu aidha kwa mtu kusoma, au walau kuonyesha shelves za vitabu.
Vitabu ni msingi wa fikra, haswa katika hii dunia ambayo sasa taarifa na maarifa yanasimama katika uchumi, knowledge economy. Lakini alihitaji nguvu Zaidi kuelezea usomaji kama ambavyo Marcus Garvey aliezea kwenye The message to the people.
KUHUSU ULEVI
Humu Kezilahabi hakutaka kuzipinga falsafa za kiafrika ambazo katika jamii zetu baada ya ngono starehe huwa ni pombe, utaona kawaelezea wanywaji tangu kwenye kitabu cha rosa mistika, na vinginevyo.
Mzingile na Nagona pia zimetaja unywaji wa pombe. Ila kwenye vitabu hivi wametumia neno mvinyo
Kwenye mzingile mzee alimuuliza, mbona kila ukirudi unakuwa umelewa mvinyo unapata wapi, akajibu kanisani
KEZILAHABI sio mtu anayeipinga pombe, anajua ufupi wa maisha na mtu anaweza fanya chochote ambacho anaweza akafurahia katika kipindi hiki kifupi cha maisha yake.
#Kezilahabian