Mawazo ya Kezilahabi kuhusu maisha

Mawazo ya Kezilahabi kuhusu maisha

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
“Maisha ni kama mkufu, unachukua kipande hiki na hiki unaviunganisha, kipande kikikataa kiache kitamfaa mtu mwingine...” Mzingile.

Falsafa ya maisha kwa muono wa Kezilahabi, hauna tofauti na wanafalsafa walio wengi, lakini muono wake upo kwenye kujifunza, take that which works for you! Kwa kuwa kiundani(Intrinsically life is meaningless) Kama kitu hakikufai achana nacho. Ndio maana alifananisha maisha na mkufu ambao unapaswa kuuunda wewe mwenyewe.

Katika kuliona hilo Kezilahabi anaona vitu vya kipuuzi tunavyovifanya maishani na anavitukana kwa kumuona binadamu si kiumbe anayeweza kufikiri. Sio tu kuifanyia istizahi dini, sala na tamaduni na Imani, Kezilahabi ameona upuuzi kwenye mengi tunayoyaishi kwakuwa tumeyakuta yako hivyo.

Katika misingi mipya ya kuvunja yaliyotangulia yanayotuumiza ili kuja na maana inayofaa kizazi cha sasa Kezilahabi anaona umuhimu wa upendo kwenye maisha, na nafasi ya sayansi, ili huu mzaha (Kuishi) uwe mwepesi na wenye kuvutia.

Hapa moja kwa moja anaponda Schoolism, ndio sababu kwenye Nagona alijiuliza kama fikra zingalipo au tumebaki kuswaga kwenye madukagati ya wanafalsafa vichaa?

Mmoja kati ya msingi anaouweka mbele Kezilahabi ni kuwa hamuoni kiumbe mtu kama mwenye thamani kuliko viumbe wengine wowote, maisha yamekuwa mabaya kwa sababu kwanza hatujakielewa kifo, tumekuwa waoga kufa, woga wa kufa unatufanya tupoteze namna ya kuishi, na badala ya kuwa matajiri wa upendo tumebaki kuwa mabarakala, wanafiki na waasi.

“…maisha yenyewe ni mzaha ndio maana yanaweza kuishika”
 
Ametutoka!
 
Maana ya madukagati ni nini? Tafadhali naomba unijulishe.
 
Back
Top Bottom