Ibrahim Quan
Member
- Jul 24, 2020
- 6
- 0
Wazo la kibiashara ni nini?
Mawazo ya kibiashara ni mawazo aliyo nayo mfanyabiashara au mtu yoyote kunilngana na mtazamo wake juu ya biashara na biashara anayotaka kuifanya. Mawazo ya kibiashara ni mawazo alio nayo mtu kuhusu ni aina gani ya biashara anataka kuifanya wapi na ni kwa nini. Wazo la kibiashara ni hatua ya kwanza katika biashara, pasipo wazo au mawazo ya kibiashara hakuna mfanyabiashara ambaye anaweza akaanzisha biashara au kufanya biashara. Itambulike kuwa "biashara huanzia katika mawazo na kuelekea katika utendaji na utekelezaji" na baada ya mawazo hayo kwenda katika utekelezaji mtu huyo tutamwiita mfanyabiashara na kitu atakachokuwa anakifanya tutakiita biashara. Mtu anaweza asiwe na mawazo ya kibiashara na akafanya biashara! Mtu huyo anaweza kupata wazo la kibiashara kutokana na moja ya sababu zifuatazo
Familia ndugu au marafiki, mtu anaweza asiwe na mawazo ya kibiashara na kupata mawazo ya kibiashara, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamefanya biashara kutokana na mawazo walio pewa na familia zao, ndugu ama marafiki. Biashara haichagui ni wapi umetia wazo lako la kibiashara, unaweza ukafanikiwa kibiashara hata kama wazo la biashara yako umelipata kutoka kwa mtu.
Intaneti au mitandao ya kijamii, mtu au mfanya biashara anaweza akapata wazo la kibiashara kutoka katika tovuti mbalimbali na kulitekeleza. Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa anapenda sana kujifunza vitu vipya kutoka katika tovuti mbalimbali kama Google na aliweza kutafuta biashara au tovuti ambazo zinatumika sana hapa tanzania na alikuta ya kwanza ni YouTube na yapili ilikuwa ni Google na hiyo ikampelekea yeye kufungua YouTube akaunti yake ambayo inaitwa fazanation. Ninacho jaribu kukionyesha hapo au kukielezea ni kuwa mtu yoyote anaweza akapata wazo la kibiashara kwa kupitia intaneti na kuweza kupata elimu juu ya biashara hiyo.
Ubunifu - ubunifu ni kitendo cha kuvumbua au kugundua kitu kipya. Katika biashara ubunifu wa kibiashara ni kitendo cha kugundua bidhaa au huduma mpya ambayo haijawahi kuwapo hapo kabla. Hawa ndio wafanyabiashara ambao hufanikiwa sana haswa endapo wanaweza wakakifanya kitu walicho kigundua kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kipaji au kipawa alichonacho mtu - kipaji ni uwezo wa kipekee alio nao mtu, kipaji kinaweza kikamtofautisha mtu mmoja na mtu mwingine. Mfano wachoraji - wachoraji ni mfano wa baadhi ya watu waliojaliwa vipaji na kipawa, mchoraji ana uwezo wa kuchora mchoro tofauti tofauti au picha na kuziuza, watu hununua picha hicho kutokana na fumbo la picha hiyo au wanaweza waka nunua picha hizo kwa ajili ya mapambo.
Matamanio au ndoto alizo nazo mtu - mtu anaweza akawa mfanyabiashara kutokana na mtazamo na matamanio aliyo nayo mtu, toka nilipo kuwa mdogo nilikuwa anapenda sana kuwa mfanya biashara matamanio yangu yote kuanzia kipindi kile nipokua mdogo hadi leo nilikwisha kufanya biashara za aina nyingi maana nilikuwa napenda sana biashara na nilitamani sikumoja nije kuwa mfanyabiashara mkubwa, kutokana na matamanio yangu ilinibini mimi kufikiria na kutafuta wazo la kibiashara ambalo naweza nikalitekeleza ili kutimiza ndoto zangu. Hivyo basi hata wewe unaesoma kitabu hichi jaribu kuangalia matamanio yako, jaribu kufikiria kuwa baada ya miaka miwili au mitatu leo utakuwa wapi?
Utafiti, mtu anaweza akawa mfanyabiashara kutokana na utafiti alioufanya au takwimu za kiutafiti ambazo zilishawahi kufanywa, kutokana na changamoto zinazoikumba jamii kila siku na uhitaji wa jamii unaweza ukafanya utafiti na kutafuta ni njia gani ambayo unaweza kuitumia ili kuyatatua matatizo yanayo ikumba jamii na ukiweza kuyatatua matatizo hayo na hapo unaweza ukawa mfanyabiashara.
NI KWA NAMNA GANI MFANYA BIASHARA AU MJASIRIA MALI ANA WEZA KUPATA WAZO BORA LA KIBIASHARA
Mchujo wa kibiashara ni kitendo cha kuchagua biashara bora au nzuri zaidi kwa ajili ya utekelezaji kutoka katika mawazo ulio nayo, mara nyingi mchujo wa kibiashara hufanyika pale ambapo mtu ana mawazo ya kibiashara zaidi ya moja. Mchujo wa mawazo ya kibiashara ni kitendo cha mtu au mfanyabiashara kuchuja wazo la kibiashara kutoka katika mawazo mengi aliyo nayo kwa ajili ya utekelezaji.
Kama nilivyokwisha kutangulia kusema katika mawazo ya kibiashara kuwa mfanyabiashara anaweza akawa na mawazo ya kibiashara zaidi ya moja lakini akashindwa kutambua ni lipi sahihi ambalo litafaa au ambalo ataweza kulifanya kwa wakati sahihi na kumletea faida. Mtu anaposhindwa kufanya uchaguzi sahihi kwa wazo la kibiashara anaweza asije akafanikiwa.
Hatua za kufanya mchujo wa mawazo ya kibiashara.
Zipo hatua ambazo mfanyabiashara anapaswa kuzifuata ili kupata biashara iliyo bora kwa ajili ya utekelezaji, katika mchujo huu mfanyabiashara anapaswa kuchuja wazo moja moja.
Tambua na orodhesha mawazo yote ya kibiashara uliyo nayo, hii ni hatua ya kwanza katika mchujo wa mawazo ya kibiashara ambapo mfanyabiashara anapaswa kuyaorodhesha mawazo yote ya kibiashara ili aweze kutambua ataanza na wazo lipi na kumalizia na wazo lipi.

- Tadhimini na anza kutadhimini wazo moja moja la kibiashara kulingana na aina ya biashara ambayo uataka kuianzisha. Mfano wa vigezo vya kuzingatia unapokua unafanya tadhimini - wazo ulilo nalo kunauwezekano wa kutimia, au lina uhalisi?
- -faida utakayo ipata kutokana na biashara hiyo.
- -je watu (wateja wako) watakuwa tayari kununua bidhaa au huduma yako?
- -watu au jamii itanufaidika vipi kutokana na biashara yako?
- - usalama wa bidhaa yako au huduma ambayo unataka kuanzisha pamoja na usalama wa wateja wako ukoje?
- - Vipi uhalali wa biashara yako nikimaanisha uhalali wa kisheria.
- Fanya uchaguzi au utafiti juu ya biashara. Fanya utafiti juu ya wazo la kibiashara ulilo nalo kwa kutafuta taarifa muhimu kuhusu wazo hilo la kibiashara kwa kuwafuata wazoefu wa biashara. -Kama wazo ulilo nalo ni la uzalishaji wa bidhaa unapaswa kuwafyata wasafirishaji na kutambua kama kutakua na upatikanaji wa malighafi.
- -tafuta taarifa muhimu kuhusu masoko kwa kuwatafuta maafisa masoko ili kutambua kama bidhaa unayotaka kuizalisha inaweza ikapata soko. Hii itakusaidia kupata soko la uhakika pindi utakapoanza shughuli za uzalishaji.
- -Tafuta mwanasheria ili uweze kutambua uhalali wa kisheria na kutambua wajibu wako wa kisheria, mfanyabiashara anapofuata taratibu zote za kisheria ana uhuru mkubwa wa kufanya biashara zake pasipo usumbufu. Kumbuka katika hatua zote hizi unapaswa kupitisha wazo moja moja la kibiashara na kunahitaji umakini wa hali ya juu katika ukusanyaji wa taarifa.
- Angalia upatikanaji wa nafasi za kibiashara
- Fanya maamuzi
- Fuata hatua za kuanzisha biashara
- Tekeleza wazolako la kibiashara.
Upvote
0