Kwanza nakupa hongera kwa kuamua kujiajiri mwenyewe mkuu please nakuomba hilo la kuomba mkopo uliangalie kwa jicho lako mara mbili maana najua mkopo una manufaa zaidi na ni njia mojawapo ya kumsaidia mfanyabiashara kwa kumuongezea mtaji kabla hujafanya maamuzi yako ya kuitoa nyumba yako kwa kupata mkopo ingatia haya.
1. umeamua kuomba mkopo ka ajili ya kununua coaster je unakipato kingine cha kuendesha familia kuhusu matumizi madogo madogo ya kila siku hapo nyumbani?
Hili kosa hufanyika na watu wengi sana maana ukiamua kuomba mkopo wa hela jaribu kuitumia kwa makusudio ya huo mkopo maana vijana wengi huwa wakiomba mkopo mara utasikia katoa hela kidogo hapo kalipia sijui ada, kanunua mchele, na vitu vidogo vidogo asikuambie mtu ukitumia hata sh 2000 hapo umepunguza makusudio ya mkopo huo so ni vizuri ujitathimini kwanza uhakikishe kuhusu matumizi madogo madogo unayo angalau ya kukutosheleza ndani ya miezi nane au zaidi bila kugusa hata senti moja ya hiyo biashara yako. maana utakapoanza biashara yako ujue kuna return ambayo utakuwa unarudisha kil mwezi na inategemea utaomba kwa muda gani, hili ni muhimu sana
2. Pili uko tayari kuwa bandigu? hili lina maana sana unaweza kufikiri nakufundisha tabia mbaya ila ukweli kabisa tupo katika jamii ya kitanzania na tumelelewa hivyo nasema hivyo kwa sababu tunapoona mtu amenunua coaster au anakitu flani cha gharama tayari masikio yetu na fikra zetu tunafikiri ameshatajirika na wala hatujuia katoa wapi hiyo hela so unachotakiwa ndugu yangu funika masikio na macho ya watu maana watu watakuja kulilia matatizo ya shida zao usifikiri watakuja kukuomba mahela mengi hapana watakuja hata sh 1000, mara 5000 mwisho michango mara jirani anaumwa sisemi usiwe eti mkimya kabisa naomba uangalie pale kwenye ulazimu tu na uwe serious maana siku ukianguka hakuna atakayekusaidia zaidi ya kukucheka wakishangilia nyumba yako inapigwa mnada.
3. tatu je hiyo biashara ya daladala nani anakuwa dreva ni wewe au unaajiri mtu? mapendekezo nafikiri hujafikia hatua ya majukumu mengine mengi maana umesema ndio unataka kuanza hiyo biashara ninapendekeza wewe mwenye uwe driver maana wakati wa mwanzo ni muhimu sana ili kupata uzoefu angalau mwaka mzima ili ukija kumuajiri mtu hawezi kukudanganya maana utakuwa umepata uzoefu wa kutosha.
4. mwisho kabisa je mkopo huo na hiyo biashara inalingala na kiasi ambacho utakuwa unarudisha kwa mwezi hili ni muhimu sana ili usije ukawa unapigiwa na credit officer unazikimbia simu jaribu kufanya uchunguzi wako kwanza
nakutakia biashara njema na mafanikio katika hilo.
Asante