SoC04 Mawazo yetu tanzania yetu

SoC04 Mawazo yetu tanzania yetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Juma jaibu kuhanga

New Member
Joined
May 18, 2024
Posts
4
Reaction score
5
Bungeni; Katika bunge la tanzania ni muhimu watu wenye mahitaji maalimu wangejumuishwa katika nafasi ya wabunge wa viti maalum hii itasaidia kuwepo kwa uhalisia wa mambo yao wanayowakabili katika jamii ingepeteza kama walemavu wa viongo, wasiona, viziwi, bubu na albino kila watu apo wangekuwa na wawakilishi wao.

Elimu; Katika ngazi ya sekondari kila mwaka katika somo husika iwekwe mada inayoelekeza suala la mbinu za ujifunzaji la hilo somo katika mwaka husika hii itasaidia mwanafunzi kujiandaa kiakili juu ya somo husika

- Pia ni vyema jamii ipewe elimu juu ya dhana ya elimu bure ili iweze kutambua elimu bure inagusa nyanja zipi katika elimu, Baadhi ya wazazi wanashindwa kushiriki kwenye masuala ya kielimu kwa kuwa wanaamini elimu bure ni kila kitu pasi kujua mipaka ya sera ya elimu bure

- Vilevile suala la Boom kwa wanafaika wa mikopo yaani chakula na malazi bodi inabidi iwe inatoa ndani ya siku 30 na kuacha siku 60 hii itasaidia wanafunzi wengi kwa kuwa inaonekana wanafunzi wengi wanashindwa kutunza hizo pesa na kukaa ndani ya wiki nane na kujikuta wanahali mbaya sana kabla ya wiki nane kutimia.

- Pia vyuo vyote nchi viwevinaandaa makala, semina na mijadala mbali kuhusu suala la mahusiano wanapokua chuoni hii itasaidia wanafunzi kujua mipaka ya mahusiano chuoni na kupunguza vitendo hatarishi kwa waathirika wanapoachana na wenza wao.

Maji na umeme Taasisi hizi ziandae mipango madhubuti ya kusambaza huduma kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kulipa gharama kwa wakati mmoja. Hivyo wanaweza kuwapa huduma hizo na kujumlisha gharama au kuziweka katika malipo ya kila mwezi mfano kila mwezi au kila huduma itapoisha muda wake ili aweze kulipa bili wanaweka 5000 kama malipo ya gharama za kuwekewa huduma na kiasi kingene kwa huduma anayoihitaji kama mtu anataka kununua umeme wa 2000 itamlazimu alipe 7000. Hii itasaidia kuwepo kwa umeme na maji kwa watu wengi.

Ajira, Somo la kodi liwekwe katika elimu hususani kuanzia ngazi ya sekondari hii hitasaidia wanafunzi kujua umuhimu wa kodi katika suala la ajira kwani nchi ili iweze kuajiri inategemea na mapato ya taifa na mwajiri mkuu na serikali hivyo suala la elimu ya juu ya kodi ni muhimi kupandikiza kupandikiza katika damu za vijana na kukwepa ule ushirikiano wa mfanyabiashara na mteja katika ukwepaji wa kodi.

- Pia suala la ukosefu wa ajira liwekwe wazi kwa vijana na kueleza sababu zake katika jamii pia serikali iweke njia mbadala ya kujiajiri yaani kufundisha hatua za kufuata ili vijana waweze kujiajiri na kuachana na neno la vijana hawataki kujajiri bila kuwapa mbinu za kujiajiri.

- Pia serikali iandae taasisi ya kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vitendo bure kwa vijana yaani utengenezaji wa sabuni, keki, mapambo n.k katika maeneo mbalimbali hii itasaidia kukuza na kuchochea ujasiramali kwa vijana. Huduma zote za kjamii ambazo zinahitaji utambulisho wa kadi za mhusika kama vile Hospitali na Benki ni vyema ungeweka utaratibu wa matumizi ya alama ya vidole yaani finger print kwani sio kila muda wananchi wanaweza kutembea na kadi mfukoni kwake pia itasaidia kupunguza wizi na udanganyifu kwa watumiaji.

Viongozi wote nchini ni kuanzia ngazi ya ubunge ni vyema kuweka wazi notes ya mali wanazomiliki mwanzoni na mwishoni mwa uongozi wao. Hii itasaidia kupunguza nguza ubadhilifu wa mali za umma kwa viongozi ambao sio wazalendo.

Rushwa; Serikali iweke adhabu madhubuti juu ya hakumu ya mtu anayekutwa na tuhuma za rushwa ingependeza suala la rushwa hukumu yake iwe kama ya ubakaji maana inanyima haki raia wengi na kikwazo kwa taifa kwa ujumla.

- Pia wanaotoa rushwa nao waandaliwe hukumu inayofanana au kukalibiana na hii.
 
Upvote 4
Pia ni vyema jamii ipewe elimu juu ya dhana ya elimu bure ili iweze kutambua elimu bure inagusa nyanja zipi katika elimu, Baadhi ya wazazi wanashindwa kushiriki kwenye masuala ya kielimu kwa kuwa wanaamini elimu bure ni kila kitu pasi kujua mipaka ya sera ya elimu bure
Kweli bro, maana kiuhalisia elimu ni gharama. Cha thamani chochote ni lazima kiwe na gharama.

Boom kwa wanafaika wa mikopo yaani chakula na malazi bodi inabidi iwe inatoa ndani ya siku 30 na kuacha siku 60 hii itasaidia wanafunzi wengi kwa kuwa inaonekana wanafunzi wengi wanashindwa kutunza hizo pesa na kukaa ndani ya wiki nane na kujikuta wanahali mbaya sana kabla ya wiki nane kutimia
Kwa hili unaonaje kama wakiachwa hivyohivyo ili wajifunze pia kujipangia bajeti. Mradi tu boom lao wapewe. Kuwalealea ndio kutazalisha wateja wengi zaidi wa kausha damu tu mbeleni. Maoni tu lakini.

Pia wanaotoa rushwa nao waandaliwe hukumu inayofanana au kukalibiana na hii.
Safi, maana halisi ya haki.
Viongozi wote nchini ni kuanzia ngazi ya ubunge ni vyema kuweka wazi notes ya mali wanazomiliki mwanzoni na mwishoni mwa uongozi wao. Hii itasaidia kupunguza nguza ubadhilifu wa mali za umma kwa viongozi ambao sio wazalendo.
Kuhusu hili tukiimarisha vizuri tu masuala ya kodi tutatoboa, maana historia ya kodi ya mtu itaoneaha maendeleo ameyapata kihalali ama la?
 
Back
Top Bottom