Mawazo zaidi kuhusu maadili na nidhamu

Mawazo zaidi kuhusu maadili na nidhamu

Mimi nafikiri serikali inawajibika kutoa elimu ambayo itakayowafanya watu wetu wajitegemee na wasiwe tegemezi kwa serikali. Kama elimu yetu ikiwa bora ambayo itawafanya watu wetu wawe wenye kuweza kujitegemea kimawazo na kubuni mbinu mbali mbali za kuzalishaji mali na kujiongezea kipato tutapunguza tatizo la ajira. Kwahiyo elimu ya kujitegemea lilikuwa wazo zuri sana. Nadhani serikali inawajibika kuajiri watu wachache sana lakini wote wanaobaki wanawajibika kujiajiri na kutengeneza maisha yao wenyewe. Baada ya kuwapa elimu inawapasa kujitegemea. Kama elimu yetu haitowapa uwezo huo kwa kuwafanya waweze kusimama peke yao itakuwa tatizo. Hili sio suala la kuajiri watu wengi tu bali watu watakaokuwa na skills na uwezo wa kutumikia vizuri zaidi katika serikali. Watu wenye maadili, nidhamu na uwezo wa kuwa watumishi wa umma. Kwa mfano jambo rahisi sana la kupunguza ajira ni kwenye kilimo ni watu wangapi wanashiriki katika kilimo na tuna ardhi ya kutosha? nadhani hii pia inahitaji nia ya dhati ya watu kutoka katika umaskini.Katika post yangu nilisema sio kweli serikali haina pesa inaweza kuwalipa vizuri wafanyakazi wa serikali kama ikibana matumizi yasiyo ya lazima na kukusanya kodi ipasavyo. Ikiwemo jamii yenyewe kuzingatia uzazi wa mpango kwakuwa kama hatutazingatia uzazi wa mpango huduma za jamii hazitotosheleza daima au pengine kuwa bora.Kwahiyo suala la kujiuliza hapa ni tufanye nini ili kuengeneza elimu itakayo wafanya watu wetu wawe na uwezo wa kuzazlisha na kujitegemea? Nadhani tukiwapa skills za kazi hasa kazi za uzalishaji tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira. Tutakuwa na uwezo wa ku regulate uchumi wetu vyema kama watu wetu wakizalisha vya kutosha.

hakika uko sahihi kuwa serikali ndio yenye kuwajibika kutoa elimu ya kujitegemea kwa raia. lakini serikali yetu haina viongozi wenye muono huo kwa sababu wanaikosa nidhamu yenye kuwaongoza kulijua hilo. na hiyo inasababishwa na kutokuwa na msingi bora wa maadili juu kipi kinastahili kufanywa km kitu kizuri kwa taifa na kipi kibaya.
 
Mimi nafikiri serikali inawajibika kutoa elimu ambayo itakayowafanya watu wetu wajitegemee na wasiwe tegemezi kwa serikali. Kama elimu yetu ikiwa bora ambayo itawafanya watu wetu wawe wenye kuweza kujitegemea kimawazo na kubuni mbinu mbali mbali za kuzalishaji mali na kujiongezea kipato tutapunguza tatizo la ajira. Kwahiyo elimu ya kujitegemea lilikuwa wazo zuri sana. Nadhani serikali inawajibika kuajiri watu wachache sana lakini wote wanaobaki wanawajibika kujiajiri na kutengeneza maisha yao wenyewe. Baada ya kuwapa elimu inawapasa kujitegemea. Kama elimu yetu haitowapa uwezo huo kwa kuwafanya waweze kusimama peke yao itakuwa tatizo. Hili sio suala la kuajiri watu wengi tu bali watu watakaokuwa na skills na uwezo wa kutumikia vizuri zaidi katika serikali. Watu wenye maadili, nidhamu na uwezo wa kuwa watumishi wa umma. Kwa mfano jambo rahisi sana la kupunguza ajira ni kwenye kilimo ni watu wangapi wanashiriki katika kilimo na tuna ardhi ya kutosha? nadhani hii pia inahitaji nia ya dhati ya watu kutoka katika umaskini.Katika post yangu nilisema sio kweli serikali haina pesa inaweza kuwalipa vizuri wafanyakazi wa serikali kama ikibana matumizi yasiyo ya lazima na kukusanya kodi ipasavyo. Ikiwemo jamii yenyewe kuzingatia uzazi wa mpango kwakuwa kama hatutazingatia uzazi wa mpango huduma za jamii hazitotosheleza daima au pengine kuwa bora.Kwahiyo suala la kujiuliza hapa ni tufanye nini ili kuengeneza elimu itakayo wafanya watu wetu wawe na uwezo wa kuzazlisha na kujitegemea? Nadhani tukiwapa skills za kazi hasa kazi za uzalishaji tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira. Tutakuwa na uwezo wa ku regulate uchumi wetu vyema kama watu wetu wakizalisha vya kutosha.


Shayu:
Governments are the most inefficient enterprises in the world. Even in Scandinavian countries where people enjoy the highest quality of life on the planet, people there think that their governments are inefficient entities. So why do you think that the Tanzanian government with all its problems will be able to educate people who are capable of solving our problems?

The point I want to make is schools cannot teach students everything. In particular, they can’t instill entrepreneurship skills in those individuals who want to employee themselves and create opportunities for others. I am not downplaying the role of schools, but I think there’s a limit where formal education can take you when it comes to entrepreneurship.

Many professionals in academia have decided to become teachers, instructors, or professors, not because they have wanted too but because their professions have given them job security. For example if you are teacher in Tanzania, you might not get paid well, but you have a job for life. So tell me how these individuals who are afraid to take risks will teach young minds the values of business ownership?

As a society, Tanzanians shouldn’t downplay the roles of their own environments. For example, Tanzanian Indians, arabs, chaggas or wapemba are most likely to be involved in self-employment because their parents prepare them to think so. So instead of asking the government to be involved in every aspect of your child’s life, you should change your mindset.

If we go back to the original theme of this thread, you will find out that maadili and nidhamu are problems because people don’t see the relationship between their contribution to the well-being of the nation and what they get in return from their government.
 
Shayu:
Governments are the most inefficient enterprises in the world. Even in Scandinavian countries where people enjoy the highest quality of life on the planet, people there think that their governments are inefficient entities. So why do you think that the Tanzanian government with all its problems will be able to educate people who are capable of solving our problems?

The point I want to make is schools cannot teach students everything. In particular, they can't instill entrepreneurship skills in those individuals who want to employee themselves and create opportunities for others. I am not downplaying the role of schools, but I think there's a limit where formal education can take you when it comes to entrepreneurship.

Many professionals in academia have decided to become teachers, instructors, or professors, not because they have wanted too but because their professions have given them job security. For example if you are teacher in Tanzania, you might not get paid well, but you have a job for life. So tell me how these individuals who are afraid to take risks will teach young minds the values of business ownership?

As a society, Tanzanians shouldn't downplay the roles of their own environments. For example, Tanzanian Indians, arabs, chaggas or wapemba are most likely to be involved in self-employment because their parents prepare them to think so. So instead of asking the government to be involved in every aspect of your child's life, you should change your mindset.

If we go back to the original theme of this thread, you will find out that maadili and nidhamu are problems because people don't see the relationship between their contribution to the well-being of the nation and what they get in return from their government.


Miongoni mwa mambo ambayo sipendi ni kwa watumishi wa umma kwa wakati mmoja kuwa wafanyabiashara na watumishi wa umma. Umeliongelea hili jambo sidhani kama ni sahihi. Nadhani ni muhimu kwa wafanyakazi wa umma kutengenezewa mazingira mazuri ili wajitoe wote katika kazi walizoajiriwa. Hili ni muhimu sana. Ili kuongeza tija katika utumishi wa umma ama sivyo tutakuwa tunacheza. Ni muhimu kwa wao kupewa mahitaji yao muhimu, na wanaweza kupatiwa kama serikali ikijipanga. Ya kuwa na nyumba bora, elimu bora kwa watoto wao kwa kuimarisha elimu yetu na pia kuimarisha mifuko yetu ya jamii. Ili wafanyakazi wa umma wawe na imani na maisha yao baada ya kustaafu waishi maisha ya adili na yenye kumfariji. Hatuwezi kuwa na wanajeshi ambao kwa wakati mmoja anafanya ujasiriamali dukani na wakati huo huo kufikiria ulinzi hivyo hivyo kwa walimu hatutaweza kuzalisha kitu bora. Tuwaache wajasiliamali wawe wajasilaimali na watumishi wa umma wawe watumishi wa umma. Tuboreshe maslahi yao waishi maisha ambayo ya wastani ambayo yatamwezesha mfanyakazi wa umma kusomesha watoto wake katika shule za umma zilizoboreshwa, kupata huduma za afya, kuwa na makazi bora na gurantee kwa maisha yake ya ustaafu. Kwahiyo ni lazima tujenge kuridhika huku kwa watumishi wa umma. Tutenganishe kati ya utumishi wa umma na biashara. Ni sawa kwa mtumishi wa umma mke wake au mume wake ambae sio mtumishi wa umma kufanya biashara lakini sio kinyume chake. Jambo hili lina madhara yake katika utendaji wa utumishi wa umma.
 
Miongoni mwa mambo ambayo sipendi ni kwa watumishi wa umma kwa wakati mmoja kuwa wafanyabiashara na watumishi wa umma. Umeliongelea hili jambo sidhani kama ni sahihi. Nadhani ni muhimu kwa wafanyakazi wa umma kutengenezewa mazingira mazuri ili wajitoe wote katika kazi walizoajiriwa. Hili ni muhimu sana. Ili kuongeza tija katika utumishi wa umma ama sivyo tutakuwa tunacheza. Ni muhimu kwa wao kupewa mahitaji yao muhimu, na wanaweza kupatiwa kama serikali ikijipanga. Ya kuwa na nyumba bora, elimu bora kwa watoto wao kwa kuimarisha elimu yetu na pia kuimarisha mifuko yetu ya jamii. Ili wafanyakazi wa umma wawe na imani na maisha yao baada ya kustaafu waishi maisha ya adili na yenye kumfariji. Hatuwezi kuwa na wanajeshi ambao kwa wakati mmoja anafanya ujasiriamali dukani na wakati huo huo kufikiria ulinzi hivyo hivyo kwa walimu hatutaweza kuzalisha kitu bora. Tuwaache wajasiliamali wawe wajasilaimali na watumishi wa umma wawe watumishi wa umma. Tuboreshe maslahi yao waishi maisha ambayo ya wastani ambayo yatamwezesha mfanyakazi wa umma kusomesha watoto wake katika shule za umma zilizoboreshwa, kupata huduma za afya, kuwa na makazi bora na gurantee kwa maisha yake ya ustaafu. Kwahiyo ni lazima tujenge kuridhika huku kwa watumishi wa umma. Tutenganishe kati ya utumishi wa umma na biashara. Ni sawa kwa mtumishi wa umma mke wake au mume wake ambae sio mtumishi wa umma kufanya biashara lakini sio kinyume chake. Jambo hili lina madhara yake katika utendaji wa utumishi wa umma.



You are misguided. Can you tell me who is mfanyabiashara and who isn’t? When you go to work, what do you think you do? You sell your employer your expertise, skills, or manual labor. So in essence you aren’t different from the person who operates bus services, owns a TV station, or a commercial farm. So stop looking at businessman as a person who’s incapable of working for the government.

Second, your ideas stiffed social mobility, exchange of ideas and innovation. Take for example professors at the UDSM. According to you, they are public servants and shouldn’t participate in the market place as a business people. The question is can they write books for profits? According to you, they shouldn’t because they are public servants. For your information, writing a book is a business endeavor as teaching in another school or performing consulting assignments?

The advance in technology makes some professions in public arena obsolete. If you don’t allow people to venture outside their professions, how are you going to help individuals that the government has decided to reduce them from the workforce? Or do you think the government job is a life entitlement? Once you are in, you will stay there indefinitely.

Why should public servants be satisfied with what they have got? Why do you think that a public servant can’t be a millionaire? And why do you thing that it’s the duty of the government to provide houses for its workers?
So your ideas don’t solve the root cause of nidhamu and maadili mabaya. As a matter of fact, rather than helping, you exaggerate the problem because you think government is a solution of every social predicament.
 
You are misguided. Can you tell me who is mfanyabiashara and who isn't? When you go to work, what do you think you do? You sell your employer your expertise, skills, or manual labor. So in essence you aren't different from the person who operates bus services, owns a TV station, or a commercial farm. So stop looking at businessman as a person who's incapable of working for the government.

Second, your ideas stiffed social mobility, exchange of ideas and innovation. Take for example professors at the UDSM. According to you, they are public servants and shouldn't participate in the market place as a business people. The question is can they write books for profits? According to you, they shouldn't because they are public servants. For your information, writing a book is a business endeavor as teaching in another school or performing consulting assignments?

The advance in technology makes some professions in public arena obsolete. If you don't allow people to venture outside their professions, how are you going to help individuals that the government has decided to reduce them from the workforce? Or do you think the government job is a life entitlement? Once you are in, you will stay there indefinitely.

Why should public servants be satisfied with what they have got? Why do you think that a public servant can't be a millionaire? And why do you thing that it's the duty of the government to provide houses for its workers?
So your ideas don't solve the root cause of nidhamu and maadili mabaya. As a matter of fact, rather than helping, you exaggerate the problem because you think government is a solution of every social predicament.


Hujanielewa vizuri concept niliyokuwa naongelea na falsafa yangu nzima.
 
Hujanielewa vizuri concept niliyokuwa naongelea na falsafa yangu nzima.

I understand you very well but there's a huge different between you and me. We live in two different and opposing political extremes. Based on your posts, it seems you favor highly regulated environments in which the government is a master of everything.
 
I understand you very well but there's a huge different between you and me. We live in two different and opposing political extremes. Based on your posts, it seems you favor highly regulated environments in which the government is a master of everything.

A Country is organism. ufanisi wa nchi utategemea sana ufanisi wa element zinazounda taifa eg watu na taasisi zao. ili taifa liendelee lazima kuwe na regulations katika baadhi ya mambo. Mimi nafikiri baadhi ya mambo ni misingi ya taifa imara. Hasa suala la national ethics.
 
Hoja yako ni nzuri sana na lengo lako lina mantiki sahihi na mimi ninakubaliana na hoja yako mhimiri. Ila ninakwenda kinyume kidogo na mbinu unayoipendekeza kuweza kulifikia lengo hilo. Kwa maelezo yako mengi yamejikita katika kulaumu na kusema kauli kama inpaswa, lazima….nk . Kauli kama hizi ni bora kwa wale unaowaambia kama wanatambua kile unachowasisitizia ila walikuwa wameteleza ila sio kwa watanzania.

Labda nizifafanue hoja zangu ili unielewe nachokimaanisha. Maadili, kwa neno la kingereza (morality) lina maana ya matendo yote yanayomhusu binadamu. Miendendo na taratibu zote zinazomhusu binadamu. Unapoongelea maadili unazungumzia kaida zote katika maisha ya binadamu anayeishi katika jumuiya fulani ya watu. Matendo hayo yote huwa yamegawanyika katika makundi mawili, yaani matendo mema na maovu.
Lakini umaadili au elimu maadili (ethics) ni taaluma ambayo hutoa misingi au kanuni ambazo ndizo hutumika kuyafasiri matendo yanayotendeka kama ama ni mema au maovu. Na hapo ndipo tunapobaini kuwa kitendo kile ama ni chema au kiovu. Bila misingi hiyo itolewayo na elimu maadili hakika hatuwezi kulitambua tendo lolote kama ni jema au baya hata kama ni jema na baya kwa lenyewe au zuri kwa lenyewe.

Lakini pia, katika taaluma hii ya umaadili, ipo mitazamo mbalimbali ya kuyatazama matendo au kuyafasiri matendo ya binadamu kama ni maovu au mema. Mtazamo wa kwanza ni ule unaopendekeza kuwa maadili ni dhana moja na sawa kwa kila mtu na kwa watu wote (moral objectivism). Mtazamo huu hupendekeza ya kuwa, ubaya au uzuri/wema wa tendo umo katika tendo lenyewe na binadamu wote hulitazama sawa kuwa ni baya au jema na ni kwa watu wote ulimwenguni. [Moral absolutism – state that, all human acts are evil or good to all people universally – everywhere and to any person] kwamba, kwa mfano kuua ni tendo baya kwa kila mtu kwani tendo lenyewe ni baya na kila mtu hakuna nayependa kufanyiwa hivyo. Wafuasi wa mtazamo huu ni wengi wakiwemo wanafalsafa wa zamani wa maadili.

Mtazamo wa pili ni ule unaoyaangalia maadili au kuyafasiri kuwa matendo ya binadamu ni mabaya au mazuri kulingana na mtu au jamii yake mwenyewe ambapo kupitia jamii hiyo wanayo misingi na vigezo vyao vya kimaadili. Na hivyo, huwezi kuwa utamaduni wa watu fulani ni mzuri na wa watu fulani ni mbaya, kwani kila watu wanao utamaduni wao ambao ni mzuri kwa wao japo unaweza pia kwa wengine ukawa mzuri au mbaya pia. Hawa hudai kuwa hakuna kanuni maalumu na za kijumla kwa watu wote na mahala pote zenye kutumika kufasiria matendo fulani kuwa haya ni mema na haya ni maovu bali jamii yenyewe ndio kipimo cha ubaya na uzuri wa utamaduni wao. Hii ni (moral subjectivism approach). Wao hukanusha uwepo wa kanuni jumuishi zinzotambuliwa na wanadamu wote kuhusu maadili. Kwa hiyo kwao, huyaangalia maadili kwa mtazamo wa mtu, watu au jamii fulani. Baadhi ya wafuasi wa mitazamo hiyo ni wanaelimu jamii (sociologists).

Mtazamo wa tatu ni ule unaodai kuwa sio kila sehemu maadili au kanuni za maadili hufuatwa, mtazamo huu huitwa (amorality au amoral approach). Mtzamo huu hufuatwa zaidi na wanaelimu biashara au uchumi. Katika biashara, hudai kuwa biashara haina cha maadili au haifuati/kufungamana na kanuni za kijamii au za ulimwengu kuhusu maadili ya kawaida, bali biashara ina maadili yake ambayo ndio taratibu na msingi wa biashara. Na misingi hiy au kanuni hizo ni kukuza uchumi au kuongeza faida katika biashara kwa njia yoyote ile. Kwa maana hiyo, wafanya biashara na wanaelimu biashara hujali faida inayopatikana kwa biashara na kukuza uchumi na wala sio maadili. Hapo ndipo matendo kama ulaghai, wizi, uongo, kuuza bidhaa feki huhusika pia, lengo ni kuongeza faida kiuchumi. Kwa mfano, kampuni inaweza kuzalisha bidhaa ambayo inawezakuwa na madhara kwa watumiaji wake na ikagundulika kuwa kampuni ilishazalisha bidhaa hizo, lakini wakisitisha kuzipeleka sokoni, kampuni itapata hasara kubwa…na hivyo, inaamuliwa kuzipeleka bidhaa hizo sokoni haijalishi watu wataathirika au la. Ilmradi faida ipatikane…..katika msingi huo wafanya biashara hudai kuwa kitendo hicho ni kufanya biashara bila kuhusika na kanuni za kimaadili. na katika ulimwengu huu wengi hukimbilia kwenye biashara, hakika watakuwa na mtazamo huo.

Mtazamo mwingine wa kimaadili ni ule unaoitwa “utilitalianism approach of morality” ambao hudai kuwa tendo ni jema au baya kulingana na mtazamo wa walio wengi kuona kuwa kile kilicho na manufaa kwa wengi na maafa kwa wengi, hivyo wao huamua kuwa tendo hilo ni jema au ovu. Kumbe jamii ikiona hili suala sio zuri kwao basi linakuwa baya au ovu, ikiona zuri basi linakuwa zuri.

Mtazamo mwingine ni ule unaofuatwa na wale wanaodai kuwa hakuna tendo baya au zuri kwa lenyewe isipokuwa kila tendo ni zuri bali huja kuwa baya pale ambapo mtu humuumiza, na huja kuwa zuri pale linapokuwa na manufaa kwake. Kumbe, kwa mtazamo huu mtu akiiba au kufisadi lakini akanufaika kama yeye hakika hawezi kuacha matendo hayo na huwezi kumwambia kuwa hayo matendo ni maovu. Kwake ni mazuri, yaani yamemnufaisha.

Kwa maelezo haya mafupi kuhusu maadili, naomba niseme kuwa, mitazamo ya “moral subjectivism, utilitarianism, amorality, na ule unaosema tendo ni baya au zuri pale linaponufaisha au kuumiza” ndio mitazamo ambayo hufuatwa na watu wengi katika ulimwengu wa sasa, zikiwemo nchi tajiri ulimwenguni. Nchi hizi hufuata mitazamo hiyo na ndio maana wao hufanya kila njia iwe bora au mbaya kuzinyonya nchi masikini, kwao, matendo ya nchi masikini ndio mabaya, ila kwa wao yao ndiyo mazuri, ndio maana tunao uvamizi na vita kwa nchi zetu ilmradi wao wapate kile wanachotaka kutoka kwetu ili wakuwe kiuchumi.

Sanjali na hilo, viongozi wengi, katika jamii zetu na nchi kwa ujumla, ni wafanya niashara ambao hufuata mtazamo wa ‘amorality’, ambao kwao pesa na utajiri ndio kila kitu na hivyo wao wako tayari kufanya kila kitu ikiwa hata ni kuua, kuiba, kuhonga kupata uongozi, kufisadi mali za umma n.k ilmradi wapate kile wanachokitaka. Hawa watu hatuwezi kuwalaumu bali msingi ni kuwarudisha katika njia kwa kuwaelimisha japo ni jambo gumu sana, maan samaki mkunje angali mbichi. Vilevile katika suala la uongozi kuna falsafa ya siasa(uongozi) ambayo iliasisi wan a mwanafalsafa wa kiitaliano Nicollo Maciavelli, ambayo inaitwa “principle of double effects” ambayo aliijengea hoja madhubuti ya kuyakana maadili na kuzalisha falsafa ya utawala anayoieleza katika andiko la ‘the perice’, yaani utawala wa mwanamfale. Huyu yeye anakanusha kufuata misingi ya kimaadili katika kupata uongozia, bali kiongozi aanweza kuwa mlaghai, mwizi, meongo yaani (pretender) ilimradi aendane na kukamata miatazamo ya jamii anayotaka kuiongoza, na apate madaraka. Yeye, anasema kuwa kiongozi atumie njia au mbinu zozote zile hadi afanikishe kupata huo uongozi, ziwe mbinu mbaya au nzuri. Alafu baada ya hapo kiongozi atumia mbinu zozote zile kulinda nafasi hiyo. Kwanini, anasema hivyo, kwa muono wake alisema hivyo, kulingana machafuko ya maadili kwa ufalme wa Roma ambao ulienea hadi kwa makasisi wa makanisa hadi kiongozi mkuu, papa. Kwahyo, Machieavelli akahitimisha kuwa binadamu ni wabaya kwa wenyewe kwahiyo hahitaji mtu kuwahurumia na kuonesha upendo kwao, na ukifanya hivyo, wanakumaliza. Ndio maana akakanusha kiongozi kufuata maadili. Viongozi wengi wetu wan chi hii hasa walioenda shule wameiga falsafa hiyo kwa kulaghai wananchi na kufanya uovu huo unaouona lengo wanufaike wao na kulinda kwa njia yoyote ile uongozi huo. Hawna elimu ya maadilia na hawayajui maadili.

Nilitoa mfano mzuri kuhusu viongozi wetu wasiofuata sheria, kuwa kama jamii au kabila lina mwono wake wa kimaisha na matendo yake – ambapo, kuna matendo fulani wao ni mema, na ni mabaya na kwa jamii nyingine sio mazuri au mabaya. Mtu aliyezaliwa kwa familia yenye uchu wa vitu vya kiulimwengu, ukosefu wa fadhila kwa wengine, wezi, watusi, walaghai n.k, hakika na yeye atakuwe katika maisha hayo hadi anakuwa mtu mzima. Tabia hizo zitaendelea kwa kuwa katika makuzi yake tabia hizo amezizoea. Mfano, kama baba ni tajiri lakini ni mlaghai, na mdhulumaji watu madeni yao, na kufanya hivyo kuna mfanya awe na mali hizo, anasomesha watoto katika shule za matajiri, ana mali kibao….mwishowe huyu mwanae, atakuwa akiwa na mawazo ya kuwa ulaghai ni mzuri na ni njia ya kuendelea, hakika huyu akiwa kiongozi fulani hawezi kujua kuwa yale ni matendo maovu bali ataendelea na tabia hizo zilizomkuza ndio utasikia, kaiba pesa za umma, fisadi, hatojali watu wanapopata hadha za kimaisha. Huyo anapochaguliwa huwezi kumlaumu. Wengi wa viongozi wetu wameumbwa kwa maisha na mazingira kama hayo, ndio maana unasikia kashfa kama ESCROW, IPTL,RICHMOND, DOWANS MELEMETA,BOT, WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA, MAJANGILI n.k. alafu baada ya kashfa hizo wanajiuzulu na wanatembea makanisani na majukwaani wanaanza kujitamba na kutoa misaada na wanaonekana mashujaa kwao, hatimaye wanaomba kuwa viongozi tena alafu mnawarudisha madarakani tena, alafu ati utegemee hao hao utawaambia wabadilike wafuate maadili, au wajali pesa na mali za umma, wakuelewe. Wakifanya hivyo, huo utakuwa ni muujiza.

Kwa maoni yangu ni kuwa hatuwezi kulalama kuwa nchi haina maadili, nidhamu na watu wakajua na kuwa na tunu hizo, la hasha! Unahitajika msasa wa uhakika. Nchi nzima watu wake wamo katika dimbwi la kutokujua maadili ni nini, na mmomonyoko wake, kwa kuwa kila mtu anao mtazamo wake wa kimaadili uliomkuza. Ndio maana hata bunge letu wabunge wake hutunga sheria si chini ya msingi wa maadili ya taifa, bali kwa kuwa wao hujua kuwa kazi kuu ya bunge ni kutunga shria, pasi kujua sheria hizo zitatumika na kusimamiwa ipi na kwa misingi ipi. Bila kujua mantiki sahihi ya sheria hizo ni ipi itakayoiongoza nchi yetu katika kilele cha mafanikio. Hawawezi kutunga sheria zenye manufaa ya kitaifa kwa sababu, taifa kama taifa hatuna misingi yetu ya pamoja tulioibaini kama sisi na kuamua kuwa ni maadili ya taifa popote pale nchini. Ndio maana kila mbunge akiamka akawaza na wala sio kufikiri anakuja na hoja binafsi kwa ajili ya kutunga sheria anayodhani yeye ni sahihi kwake kumbe pengine in audhaifu ndani mwake na haikidhi haja kwa watanzania wote.

Mathalani, nilishawahi kujiuliza kuhusu sheria kusimamia haki au kutoa haki kwa wale walionyang’anywa hali hizo. Na hudai kuwa hakimu au wanasheria wao hufasiri sheria ili kutenda haki kwa watu, ila mimi hujiuliza swali moja kuwa haki hubainishwa na sheria au sheria hulinda na kusimamia haki? Vilevile, mwanasheria au hakimu yeye ndiye mtoa haki au yeye ni chanzo cha kuitambua na kumwonesha mdai haki yake? Kama sheria ni msumemo, inakuwaje mtuhumiwa nakuwa amefanya kosa kweli, ila mshitaki ameshinwa kudhibitisha, na mtuhumiwa anashinda kesi na tunasema haki imetendeka? Je, kushindwa kuwa na ushahidi wa kutosha au kushindwa kujieleza kwa mshitaki kunaondoa kosa liliotendwa? Wakati huo huo kuna watu wanashindwa kwa sababu mbalimbali kuthibitisha madai yao juu ya kesi lakini wametendewa visivyo, ila hukumu inatoka kuwa watuhumiwa wameshinda? Hizo ndizo sheria zetu zinazotungwa na watu ambao wametoka katika jamii zetu. Hakimu, kwa mfano, anaweza akaifasiri vibaya sheria na kutoa hukumu isiyo, mhusika akakata rufaa na kwenda mahakama za juu, na kweli ikabainika kuwa hakutendewa haki na hukumu ya mwanzo. Lakini hakimu aliyekiuka au kushindwa kuifasiri sheria vizuri ama kwa maksudi au bila kudhamiria hachukuliwi hatua yoyote ya kumwadhibu kwa kosa lile. Sheria inamlinda hakimu kuwa inategemea uwezo wa a hakimu wa kuifasiri sheria….alafu kwa sheria hiyo usema sheria ni msumeno. Hiyo ndio nchi yetu na watu wake. Sheria kimsingi ipo kulinda maadili na bila maadili hakuna sheria, lakini sheria zetu hazina misingi madhubuti ya kulinda maadili yetu bali ni matamko tu kwa sababu na sisi huwa tunashuhudia wenzetu wengine wakitoa matamko hayo.

Kwa maoni yangu yenye kukubaliana na hoja yako, ni kwamba, nchi nzima imeoza, imekiuka maadili kama taifa ambayo angalau mwl Nyerere alikuwa ameanza kuiweka kwa mwono mmoja uliotokana na falsafa ya ujamaa, ambapo kumbe Nyerere ni mwanafalsafa mfalme aliyependekezwa na Plato, mwenye uwezo wa kuiongoza jamii kwa misingi ya haki na kuona ni kipi kinatakiwa. Ili nchi yetu irudi katika maadili ya kitaifa yaliyojengwa chini ya msimamo na mtazamo mmoja kama taifa, tunahitaji kufikiri upya na sio kuwaza kujua kuwa nchi yetu itakuwaje inavyotakiwa iwe. Na hili suala, linawahitaji watu waliobarikiwa kimaono hasa wanafalsafa na wenye uwezo wa kufikiri na kuufikia ukweli thabiti. Naamini wapo mmoja wapo ni wewe, na mimi ambao tunachangia mada kama hizi hapa. Tunapaswa kuendeleza elimu hii kwa watanzania wenzetu, kwa njia yoyote ile ila watu waweze kufunguka macho.

Kwa kuwa watanzania ni mchanganyiko na ni jamii tofautitofauti, hatuwezi kuegemea mtazamo wa kuwa kila mtu anafikiri ana akili hivyo anajua jema na baya. La hasha! Sio wote wanaojua hivyo, kumbe kama hawajui, inatupasa kuzunguka nchi nzima upya, kusoma na kuzichunguza jamii zetu na tabia zake ili tubaini ni matendo yapi kwao ni mabaya au mazuri kwa mitazamo na utamaduni wao, alafu tuunganishe, ufanano na utofauti huo kwa ujumla tuyaweke pamoja yale amabayo ni mema kwa kila upande, na kupitia elimu na taasisi na vyombo vya kiserikali – serikali kuu, bunge na mahakama, wajadili chini ya uongozi wa wataalamu waliochagulia kama wanafalsafa, na wasomi wenye ung’amuzi wa ajabu juu ya maadili ambao tayari watakuwa wameisoma mitazamo yote ya maadili na kuunganisha na kuja na matazamo mmoja ambao utayafasiri maadili kwa mwono mzuri wa kitanzania na kuitwa kuwa haya ndio maadili kwa mujibu wa mtazania. Na tutoe elimu ya kina kuhusu dhana ya kuyaangalia maadili kwa mwono mmoja kuwa maadili au matendo ya binadamu ni mazuri na mabaya kwa yenyewe (moral universal principle – moral objectivism/absolutism). Hayo ndiyo yatakayotufasiri na hata mtu akikosea atajua dhahiri kuwa kakiuka maadili ya kitanzani, na ama ataelimishwa au kuadhibiwa kwa misingi ya maadili ya kitanzania na hapo ndipo tutakuwa sahihi kusema nchi yetu ina maadili kwa kuwa sisi kama taifa tayari tulishakuabaini na yapo hadi katika vitabu na adidu rejea za taifa. Hata vyombo vya kutunga sera na sheria vitatunga sera/ sheria hizo chini ya misingi hiyo ya umaadili wa taifa letu na si kama wanavyofikiri wao.

Tukishakuyagundua hayo, ni jukumu pia hayo mambo kuingizwa katika mitaala ya elimu yetu, na kuanzisha somo la maadili kwa ngazi zote na somo hilo liwe la lazima na msingi kwa wanafunzi wetu wote na lihimizwe. Pili hilo liende sambamba na tafakuri kuu juu ya falsafa na mwono wa misingi ya kitaifa ambayo ndio hiyo itatuongoza katika kupanga kila jambo kwa maadili ya taifa letu, na hivyo kuwakuza vijana wetu katika misingi hiyo amabayo ndiyo hiyo itakuwa inawafasiri watanzania mahara popote. Kwa kipindi kirefu, elimu hii ya umaadili kwa watu wetu ikitolewa mwishowe watu watautambua mwelekeo wao na kulijua taifa lao na kuwa tayari kuipigania kwani wanao utambulisho wao wa taifa. Huwezi kusema maadili ya taifa bila taifa lenyewe kuwa na maadili hayo ambayo watu wake wamebaini wao.

Hili jambo aliliona mwl Nyerere ndio maana aliamua kuunda falsafa ya ujamaa na kujitegemea ambayo kila kitu kilichokuwa kikiibuliwa kiliaksi misingi ya ujamaa, na maadili yakiwemo. Lakini, baadaye uhuni uliliingilia taifa hili na kupoteza utambulisho wetu ambapo waliofanya hivyo, ndio hao hao wanaokiuka miongozo hiyo na kuliharibu taifa kulifanya lisiwe na mwelekeo.
YANGU NI HAYO
Nimekusoma vyema uchanganuzi wako.
 
Back
Top Bottom