Mawe kwenye figo

Aongezee kupunguza ama kutotumia kabisa 'Carbonated Drinks'.
 
MREJESHO
Nilibahatika kuonana na daktari wangu, baada ya kusoma ripoti ya Ct scan na kuiangalia CD ya hali ya figo zangu alisema yafuatayo:
1. Mawe yapo matatu
2. Ni madogo sana
3. Mrija mmoja wa kutolea maji na mkojo kweny figo umesinyaa.
Baada ya hapo alinielekeza kunywa maji lita tano kila siku na akanipatia dawa tatu ambazo ni Febuxostat 1x1 kwa siku30, Cetrizine tabs 1x2 kwa siku 7, na Xasix tabs 2x1 kwa siku 7. Baadaye akasema nirudi Kupima tena baada ya mwezi.

Kwa sasa sijisikii maumivu yoyote, ni kukojoa tu kila baada ya dakika 30 . Nawashukuru sana mlionitia moyo, nilipata hofu kubwa maana magonjwa ya figo yanatisha, niliwaza sana kuhusu wanangu wadogo hivi sasa uambiwe figo zimefeli - Nawashukuru sana na nitawapa mrejesho zaidi .
 
Nenda pharmacy kuna dawa inaitwa Tamsulosin hii dawa inatanua mrija wa mkojo na jiwe kama limeingia ktk njia ya mkoja linatembea kirahisi kutoka nje kupitia tundu la mkojo.Mara nyingi maumivu hutokea jiwe linapoingia ktk njia ya mkojo.Hapo hakuna kulala kila upande utaogeukia hauna nafuu.Lakini hiyo dawa ni kiboko.Huwezi kuipata ktk pharmacy ndogondogo.Ukianza kuitumia tu na nafuu utaiskia maumivu yatapungua.Angalizo:Ukishafikia ktk hali hiyo ili uweze kuthibitisha kuwa kweli ni mawe basi wakati unajisaidia haja ndogo hakikisha unakuwa na chujio kama la chai ule mkojo uaoutoa upitie ktk chujio hapo ndipo utafanikiwa kuna jiwe au mawe yaliyopita ktk tundu la mkojo.Na jiwe likishatoka tu basi unapata nafuu kubwa sana
 
Ahsante ila tayari nimepewa dawa na daktari. Alisema dawa alizonipa zinayeyusha mawe na hivyo hayatatoka mazima mazima yatatoka kwenye mkojo
 
Kula matango sana na nenda soko la ilala a soko lolote kubwa ulizia mboga za majan nanaa unaku unatengeneza kama juice kwa brenda ni nzuri sana hata kama ulikua unapata maumivu ama hupati mkojo kwa wakati utashangaa unapata ...nanaa +tango

mkuu unatia na maji kiwango gani?
 
je una mtu anapitia hiyo hali ?

hapana, ila nataka niwe natumia kila baada ya muda kama kinga, dawa za kienyeji za huwa ni jiwe moja ndege wa tatu mkuu, na nyingi ambazo hazina side effect kubwa, ukiwa na kawaida kutumia mara kwa mara ni kinga nzuri na vile vile unaweza yawahi matatizo katika hatua ya mapema sana
 
Shida yangu sasa ni kupunguza uzito, Mazoezi nafanya lakini matokeo ni madogo sana. Naomba I ushauri wa njia mbadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…