Hahahhaa!. Mkuu, umeenda too deep kwa layman. Ni kama unapiga pindi kabisa.
Nina uhakika hatakuelewa, yeye anachotaka ni Ushauri na kumuondoa hofu.
Kwanza, tumpongeze kwa hatua ya mwanzo kabisa ya kufika katika kituo cha afya na kupata huduma pamoja na vipimo. Na baadae kupata uvumbuzi wa tatizo linalomsibu.
Hata hivyo, nimeshindwa kuelewa ni kwa namna gani alipimwa na kuambiwa kinachomsumbua ni mawe kwenye figo, kisha aliyemhudumia akashindwa kumshauri na kumpa dawa.
Anyway, tuseme alimconsult na kumuelekeza akapige x-ray ama CT scan kisha akapata dharura na kuondoka kabla ya majibu hayajatoka.
Pili, usiwe na hofu Mkuu. Kidney stones zinapona na kuisha kabisa kwa njia kadha wa kadha. Hivyo huna haja ya kuogopa na kujitoa hofu isiyo na maana. Cha muhimu ni kuzingatia tiba na ushauri wa kitaalam.
Tatu, matibabu ya kidney stones hutegemea sana ukubwa, aina na pengine idadi ya mawe husika.
a)Kama mawe ni madogo (chini ya mm 5), mgonjwa unashauriwa kunywa maji mengi kila siku, ili kusaidia kuflash mawe hayo.
b)Kama ni mawe ya wastani (mm 6 mpaka mm 10) basi pamoja na unywaji wa maji mengi anaweza kutumia Citalka ama Nifedine, hizo humsaidia kuyeyusha kwa kiasi mawe hayo na pia kupunguza maumivu.
c)Kama stones ni kubwa (mm 11 na kuendelea) basi tambua hayawezi kutoka yenyewe na hivyo kuhitaji usaidizi wa wataalam katika kuyavunja vunja kwa njia ya ESWL, ureteroscopy na upasuaji.
Hivyo, ni muhimu sana kujua ukubwa wa mawe husika kabla ya kuanza matibabu. Mtaalam wako atakuelekeza yote.
Tatu, tambua mlo wako na ikiwezekana badilisha. Mkuu
DR Mambo Jambo ameeleza vema hapo huu, kwenye kipengele cha supersaturation (rejea kipengele namba 4 hapo juu). Punguza matumizi makubwa ya chumvi pamoja na proteins haswa zitokanazo kwa wanyama (nyama, mayai, nk).
Jijengee tabia ya kunywa maji mengi kila siku. Fanya mazoezi na kama una uzito mkubwa, tafadhali pungua Mkuu.
Nne, itakubidi ufanye follow up juu ya maendeleo ya afya yako, haswa juu ya tatizo linalokusibu. Kwa maelekezo ya Mtaalam wako, itakubidi urudi mara kadhaa kufanya check up kuona maendeleo ya mawe yako. Kama yanatoka ama la! Na hatua za kuchukua baada.
Nakutakia uponyaji mwema.
ephen_