Mawifi inakuwaje? Kunakuwa na kutokuelewana na mke wa kaka yao

Dj lete mawifiiiii

Kuna wale mawifi kwenye harusi fulani MC alikuwa Garab ..walimpa tahadahari wifi yao kuwa kaka yao yuko romantic ni handsome anajua kupenda na ana mvuto hivyo ahakikishe ana mtunza vizuri!

Sasa just imagine hapa Mke na wifi zake watakuwa na uhusiano gani?
 
Naam naam big sisy..

Naomba nikuhakikishie kuwa huyo lastiboni akileta ukuda wake atachezea vitasa na nyundo nyingi nyingi za utosi[emoji2][emoji2][emoji2]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]



Mungu asaidie tu huyo mume asiwe ndio anategemewa kwa kila kitu huko kwao.
 
yaani jiandae tu


mie mmoja mamzooom tu....kamaliza vibweka vyote.
kakuta sina habari.

hao wifi zangu tu kwa kaka zangu ya kwao hayanihusu yeye alitaka yangu yamhusu ili avumbue nini sijui!!!!
 
wazaramo kazi unayo.

ila silaha kubwa ni kuweka mipaka na sheria, kanuji na taratibu za nyumba yako zinatakiwa kufuatwa, hutaki sepa!!!

epuka mazoea na ushosti usio wa lazima.

msaidie inapowezekana.

pia mengine unayapuuzia mpaka ashangae
 
hahahaha

yaani balaa limeanzia ukumbini....ndoa haijatimiza hata masaa 24!!!
 
Waeleze wanadhani kutubwba kitandani ndio inatosha kufanya tuwasahau dada zetu...mbususu zipo nyingi tuu na ukikubali kuolewa kaa ukijua kua huo ni muunganiko wa familia mbili sio watu wawili
Hawaelewi. Ndo maana nimekua nikieleimishwa kwamba, katika biashara ogopa sana mapenzi yakihusika. Utalia kilio cha panzi. Yaan mpenzio siyo nduguyo. Siku yakiharibika na biashara imekufa

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Kuna wanawake wanahuzunisha sana. Wanatafutaga shari zisizo na ulazima. Wanakuta family zina amani kabisa. Basi wataanza chokochoko. Sijui kwann hawatakagi kabisa bond ya mumewe na nduguze kuendelea tena. Sijui wana matatizo gani. Utafikiri dsda zao wanashare huo mkia na ndugu yao. Wale ni damu na nyama moja
Tukiolewa miji ya watu tuishi tuache kuleta sera zetu mpya. Or else iwe ni tamaduni mbaya ambazo hazimpendezi Mungu.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Binafsi huwa nipo busy na mambo yangu. Sina muda wa kufuatilia familia za kaka zangu wala kwa upande wa mwenza wangu.

Nawapenda sana wifi zangu na wanajua lakini kila mmoja ashinde mechi zake, hii inapunguza malumbano na vioja vya kila aina.
 
Duuh dada mtu anaingiaje chumba cha kaka yake na mkewe?😳😳 ajabu hii na uswahili kiwango cha lami
 
Nakuaminia kamanda[emoji23][emoji23]
Sitaki familia ambazo macho yote yapo kwa kaka yao
Familia ambazo kaka yao ni mtoto pekee wa kiume.
Familia ambazo zinampangia kaka yao maamuzi na hana sauti.
Familia ambazo mawifi ndio final say.

Mapema sana tutashindwana.
 
Asantee

Umepotelea wapi siku hizi sikuoni
Nipo sana ila huwa nakomenti kidogo kama hivi.

Si unajua tena nadumisha mawifi wasigombane na wifi yao[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…