Maxence Melo, amewaomba Watanzania kuepuka kununua simu zilizotumika 'Used' kutoka katika mataifa mbalimbali

Maxence Melo, amewaomba Watanzania kuepuka kununua simu zilizotumika 'Used' kutoka katika mataifa mbalimbali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mkuu Maxence Melo, Mshauri wa Masuala ya Mtandao yupo Mubashara akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu utapeli wa kimtandao.

Msikilize upate kufahamu mambo mengi kuhusu jambo hili, ikiwamo na matumizi sahihi ya mtandao kwa ujumla.

Mkurugenzi wa JamiiForums na Mtaalam wa Mawasiliano ya Teknolojia, Maxence Melo, amewaomba Watanzania kuepuka kununua simu zilizotumika 'Used' kutoka katika mataifa mbalimbali na hata ndani ya nchi kwa kuwa wanakuwa hawajui historia ya mtumiaji wa hiyo simu.

Melo ameyabainisha hayo leo Mei 29, 2020, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na kuongeza kuwa mtu anaweza kununua simu ambayo ilitumika kwenye uhalifu na hata kwenye mitandao mikubwa ya kigaidi na hivyo endapo simu hiyo itaanzwa kuchunguzwa, basi atakayekamatwa nayo ndiye atakayehusishwa na matukio hayo moja kwa moja.

"Kununua simu iliyotumika si vibaya sana, kama uko tayari kuyachukua yale yote yaliyoambatana na hiyo simu, maana hiyo simu unakuwa nayo karibu kuliko hata mpenzi wako au mtu wako wa karibu, kwahiyo unakuwa umezikubali athari zote zitakazotokea, lakini epuka kununua simu zilizotumika, kwa sababu inakuwa ina historia ambayo hauijui, huenda mwenye hiyo simu alishawahi kuifanyia uhalifu" amesema Melo.

Aidha Melo ameshauri umuhimu wa kila mtu kuwepa nywira 'Password' ambayo siyo rahisi mtu kuipatia na isiwe ile ya mwaka wako wa kuzaliwa.
 
Anashauri tusinunue simu used kutoka nje kwa sababu iwapo mtumiaji wa kwanza alikuwa gaidi, na wewe utaingia kwenye rekodi na mpaka upate haki yako utakuwa umeshapoteza muda mwingi sana.

Unaponunua simu used maana yake umekubali kuchukua madhara yake. Atakuwepo kesho tena kujibu maswala mbalimbali ya kimtandao.
 
Anashauri tusinunue simu used kutoka nje kwa sababu iwapo mtumiaji wa kwanza alikuwa gaidi, na wewe utaingia kwenye rekodi na mpaka upate haki yako utakuwa umeshapoteza muda mwingi sana. Unaponunua simu used maana yake umekubali kuchukua madhara yake. Atakuwepo kesho tena kujibu maswala mbalimbali ya kimtandao.

Hii ni kweli kabsa kaongea la maana mno. Watu tunajisahau sana kisa umeona kitu cha bei cheee unakikimbilia bila kujua madhara yake.
 
Mkuu Maxence Melo, Mshauri wa Masuala ya Mtandao yupo Mubashara akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu utapeli wa kimtandao.

Msikilize upate kufahamu mambo mengi kuhusu jambo hili, ikiwamo na matumizi sahihi ya mtandao kwa ujumla.
Yuko vizuri sana kwenye hiyo taaluma

Jr[emoji769]
 
Mkuu Maxence Melo, Mshauri wa Masuala ya Mtandao yupo Mubashara akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu utapeli wa kimtandao.

Msikilize upate kufahamu mambo mengi kuhusu jambo hili, ikiwamo na matumizi sahihi ya mtandao kwa ujumla.

May 29, 2020
Mada : Udukuzi na utapeli mitandaoni
Maswali mengi yanajibiwa kwa faida yako ulinzi wa data, miamala, utakashikaji pesa bila kujua, udukuzi , utapeli , sheria za Tanzania kulinda customers, sheria za mitandao n.k

Source: EastAfricaRadio
 
Back
Top Bottom