Maxence Melo: JamiiForums imefanikiwa kujenga Fikra Mbadala kwa watanzania wengi

Maxence Melo: JamiiForums imefanikiwa kujenga Fikra Mbadala kwa watanzania wengi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo mkurugenzi wa JamiiForums amefanya mahojiano kwenye kipindi cha Clouds 360. Pamoja na mambo mengine ameongelea suala la hofu ya kuingia matatani na kusema ameshaingia mara kadhaa na haijawahi kuwa hofu kwake pia ameongelea awamu ya sita ilivyoanza kwa kuwasikiliza.

========



SWALI: Kama nimukuelewa Vizuri, mtandao wa JamiiForums uliuanzisha watu wapate sehemu ya kuzungumza, kutoa maoni yao nk. Unafikiri mmefanikiwa kwa kiasi gani kufanikisha hilo?

Maxence: Ajenda ya kwanza kupigania vijana kuwa katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na maamuzi, tumefanikiwa. JF had to be a voice of a voiceless, sauti ya watu wasio na sehemu ya kusemea kwa kiwango kikubwa tumefanikiwa. Jamiiforums ndio mtandao unaoongoza hapa nchini kutembelewa na watu wengi, unapata watu laki sita, laki saba kwa siku ambapo hakuna mtandao kama huu kwa Tanzania unafanya kitu kama kile.

Nia ya pili kupambana na maswala ya ufisadi, maswala mengi ya kifisadi yaliibuliwa JamiiForums, ikiwa JamboForums mwanzoni ikaja kuwa JamiiForums na tulibadilika kuwa JamiiForums baada ya changamoto za mwaka 2008 pale nilipokamatwa nikadaiwa kuwa ni gaidi kutokana na kashfa ya Richmond lakini niseme kashfa kubwa zote nchini zilianzia JamiiForums na kwa kiwango kikubwa kwa upande wa kupambana na ufisadi mtandao wa JamiiForums umefanya kazi kubwa.

Social life, JamiiForums imewapa watu uwanja mpana wa watu kuweza kupata mawazo mbadala, watu kuweza kukutana na marafiki ingawa kuna wanaopata maadui, haikosekani katika jamii lakini imefanya watu kujenga fikra mbadala ambazo kwangu naziona ni fikra chanya.

Swali(PJ): Platform kama JamiiForums ambayo iko very strong na ukiangalia hata watu wanaochangia mle ndani pengine kuna watu wengine hawapendi kutaja majina yao lakini ukiangalia content ya michango unaona huyu mtu amebobea. Wewe ni mhandisi, katika suala zima la maadili inakuwaje maana ni free to access, kitaaluma unai-manage vipi?

Maxence Melo: Kama kuingia matatani nimeshaingia sio mara moja wala mbili, kwakweli hatujawahi kuogopa kuingia matatani na hilo sio tatizo kwetu.

JamiiForums ina watu wa aina mbalimbali, ina wasimamizi wa ubora wa maudhui, ina wasimamizi wa maudhui na ina watu wanaofanya kazi ya kujenga uelewa kwa wananchi, tunasema 'Amplification of citizen voices' kuzipeleka kwenye mitandao mingine ya kijamii.

JamiiForums haifanyi kazi kwasababu ya sheria za Tanzania, kuiogopa Serikali. JamiiForums inafanya kazi kwasababu ya matakwa ya wananchi lakini tuliweka taratibu tangu mwaka 2006 wakati inaanza kwamba taratibu hizi ndio zitaongoza namna ya kushiriki kwenye mijadala, sio kwasababu ya maadili ila kwasababu ndivyo wanachama wetu wanavyotaka.

Swali(PJ): Kuna mjadala gani unaokumbuka ambao umewahi kukaa platform ya JamiiForums na ikawa motomoto ambao pengine huwa ukilala unaikumbuka?

Maxence: Kwa context kwamba ulikuja kuleta vurugu kubwa ni mjadala wa Meremeta, najua kizazi cha sasa hawajui Meremeta ni nini! Kulikuwa na ufisadi uliokuwa unahusishwa na Jeshi na ulikuwa unaandikwa na baadhi ya vyombo vya habari pia uliibua mjadala mpana sana ndani ya JamiiForums.

Ilifikia mpaka waziri mkuu akaenda bungeni kwamba maswala ya Jeshi hayatakiwi kuongelewa kabisa. Baada ya mkwara ule, mainstream media ziliacha kuandika. Tuliendelea, mikwara iliyofata baada ya pale haikuwa mikwara ile ya kitoto. Pia mijadala ya Richmond na EPA.
 
Inatia moyo Jamiiforums kuendelea kuwa chombo namba moja cha kupashana habari nchini Tanzania ambacho huhoji zaidi kila taarifa kwa kufuata vigezo na taratibu za viwango vya juu iliyojiwekea katika upashanaji habari huku ikikidhi kulinda sheria kubwa ya nchi yaani katiba ya nchi.
 
Ni kweli, lakini kwanini kauli hii kaitoa wakati huu?
Je ndio kusema vijana wa JF wajiachie?
 
Back
Top Bottom