Mkuu mimi nakupongeza kwa unachofanya si haba ila angalia upande huohuo wa kufuta nyuzi , Kuna kitu mimi inanitatiza hasahasa jukwaa la siasa ambapo waanzisha mada wanakuwa walewale siku zote Ina maana hamna wengine wenye mawazo mbadala was kuanzisha nyuzi ? Au ndio zinazofutwa ? Mimi namshauri kwa kuwa JF Kuna watu wa aina mbalimbali na weledi mbalimbali watu wengine pia mada zao ziachiliwe zisifutwe tupate , mawazo ,elimu ,teknolojia ,ujuzi , maarifa , mwelekeo kutoka kwa watu tofauti tofauti , sio kila siku mada za akina johnthebaptist , Mayala , ninachosema wadau wengi wapewe nafasi kuanzisha mada tupate maarifa mapya , sio kila siku walewale Tena wanna mwelekeo wa Lumumba , mimi mwenyewe mada zangu nyingi sana hufutwa sawa Kama Kuna mapungufu zifuatwe sikatai lakini inatia shaka , wakati wa Jiwe mada nyingi zilifutwa na Sasa pia pia , hivi na awamu bado ni tishio kwenu . Kuna siku nilioosti kuhusu ajira 6000+ nikaweka attachment ya ilani ya CCM kuzalisha ajira milioni saba ikafutwa shida nini? Mnatishwa vizuri na sisi members tujue , lakini naomba watu wengi wafunguke nyuzi nyingi ziachwe hewani ili tujue mengi, tujifunze mengi kutoka kwa wenzetu sio kila siku walewale . Mimi nimejifunza mengi sana hapa JF ndio napenda watu wengi wapate tupate mengi pia , mawazo yangu tu hayo samahani kama nitakuwa nimekukwaza .