BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums amesema ukusanyaji holela na kuzagaa kwa taarifa binafsi za watu mitaani ikiwemo makaratasi yanayotumika kama vifungashio vya chakula au madawa ni madhara ya kutokuwa na sheria inayolinda taarifa binafsi za watu jambo ambalo linaiweka pia nchi kwenye hali isiyo salama.
Amesema kuwa Jamii Forums ikishirikiana na wadau wengine imeandaa muswada wa mfano ambao imeupeleka serikalini ili kutoa mapendekezo yatakayosaidia kutungwa kwa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi.
Pamoja na mambo mengine, muswada huo unatoa muongozo wa taarifa gani zikusanywe, zitatumikaje, zikusanywe kwa kiasi gani, mwisho wa matumizi ya taarifa hizo ni upi na lini pamoja na uwepo wa chombo huru kitakacho simamia zoezi hilo.
Aidha ametolea mfano jumbe za "tuma kwa namba hii" na "waganga wa kienyeji" kuwa ni uthibitisho kuwa mifumo ya ulinzi wa taarifa za faragha za wananchi na watumiaji wa mitandao haiko salama.
"Katiba ya nchi ibara ya 16 inataka taarifa zako binafsi zilindwe katika hali yoyote, kwa mfano mnaenda mitaani mnaona mandazi yanafungwa kwenye makaratasi mbalimbali kama mitihani, na magazeti, taarifa zetu zinapatikana kirahisi sana."
"Tunaitaka mamlaka ya nchi kuzingatia takwa la kisheria la katiba ibara ya 16 na ibara ya 18 inayotaka mawasiliano ya mtu yasiingiliwe na mtu yoyote, na kwangu huo ndio uzalendo wa kweli."
"Katiba ya nchi inalinda taarifa za mtu, ingawa katiba yenyewe imeelekeza mamlaka husika kuweka utaratibu wa kisheria, lakini kuwa na sheria rasmi ya ulinzi wa taarifa binafsi hatuna na majirani zetu wote wanayo."
"Umoja wa Afrika ulielekeza nchi wanachama kwamba, lazima mataifa yetu yatengeneze chombo huru kwa ajili ya uchakataji wa taarifa binafsi za watu wake, na ukiangalia Kenya wana chombo kama hicho ambacho kinawasaidia." - Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums.