Maxence Melo: Nashukuru kuwa mtu huru kutembea nje ya Dar bila kuomba ruhusa

Maxence Melo: Nashukuru kuwa mtu huru kutembea nje ya Dar bila kuomba ruhusa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkurugenzi mtendaji wa JamiiForums amesema anashukuru sana kwa kuwa sasa ni mtu huru kutembea nje ya Dar-es-Salaam bila kizuizi chochote cha kisheria.

Awali alikuwa na zuio, ambalo lilikuwa linamtaka apate ruhusa maalumu ya kutoka nje ya Dar kutokana na kesi zilizokuwa zinaikabili JamiiForums ambazo zimeisha rasmi leo, Novemba 17, 2020.

Aidha amesema kauli ya Rais wa Tanzania ilionesha kuwa wanahabari wanakwenda kupata uhuru wa kufichua maovu mbalimbali lakini namna ya utekelezaji wa hilo ni shida kwa kuwawatu wataogopa kuwa huru kufichua uovu.

Amesema hayo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni kutotoa taarifa ya mwanachama wa JamiiForums ambaye alifichuo uovu wa baadhi ya watendaji wa CRDB.



PIA SOMA:
https://www.jamiiforums.com/threads...otoa-ushirikiano-kwa-jeshi-la-polisi.1810712/
 
Uhuru na Haki ni mojawapo ya vitu muhimu kwa binadamu yoyote, na kwa hilo la leo Maxence Melo kuwa mtu-huru tena ni furaha kwetu sote wanaJF.
 
Hahaha conditional discharge sio uhuru jamani.

Hanafurahia kwamba anaweza kusafiri kwenda Bukoba bila kuomba ruhusa hajasema, humu mko huru.
 
Huyu Meko na mazabania wake wamesoma kweli Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu?
 
Pole na shukran kumaliza ''kifungo cha nje na kuanza kingine cha nje cha mwka 1''
 
Madai ya Wakili wa serikali: soma kwa urefu hapa chini:

MKURUGENZI JAMII FORUM AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA.
..

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja, Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzuia Askari Polisi kutekeleza majukumu yake.

Mahakama hiyo pia imemuachia huru mshitakiwa Mike Mushi kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake, huku ikimuonya Melo kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Faraji Ngukah. Katika hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema mahakama inamuhukumu Melo kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kutiwa hatia kwa kosa la kuzuia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu, pia inamuachia huru Mushi ambaye alionekana kama msindikizaji katika kesi hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya Upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao kwa kuleta mashahidi sita huku Melo akijitetea mwenyewe bila kuwa na shahidi mwingine.

Awali kabla ya kusomwa hukumu hiyo Wakili toka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, wakili Faraja Ngukah ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwani kitendo alichokifanya cha kuzuia askari kutekeleza majukumu yao ni hatari kwa Taifa.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi
, Bernedict Ishabakaki ameiomba mahakama itoe hukumu ya faini kwa sababu washitakiwa ni vijana ambao wameajiri na wanategemewa. Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Shaidi alisema mshtakiwa alionekana kuwa na makosa katika kesi ambazo zilifunguliwa awali ambazo zote zilikuwa na makosa yanayofanana.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Melo na Mushi walidaiwa kuendesha mtandao ambao haujasajiwa kwa kikoa (domain) cha .tz na katika shtaka jingine walidaiwa kuzuia askari Polisi kutekeleza majukumu yao, makosa wanayodaiwa kuyatenda kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

Habari na video kwa hisani ya
Source : Global TV Online
 
Sometimes unakosa hata cha kuandika. Max pole kwa safari hii ndefu na naamini hakuna wa kubomoa fikra zako.
 
Back
Top Bottom