Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Baadhi ya masuala aliyoongelea Mkurugenzi mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, katika warsha ya kukuza maudhui ya ndani yaliyofanyika TCRA.
Kukosoana si kubaya
Ukosoaji uwe wa pande mbili, kama kamati inavyokosoa watengeneza maudhui na wao pia wakubali kukosolewa, lakini kukosolewa huku kuwe ni kwa kujenga na kuongoza watu kuwa katika misingi na siyo kulazimisha vitu viwe wanavyovitaka, kamati isikilize na upande mwingine kujua shida iko wapi, kufanya maamuzi bila kusikiliza upande mwingine ni kuendeleza mpasuko kati ya watengeneza Maudhui na Kamati.
Sheria na Sera zilenge kuchochea Uchumi wa Kidigitali, ada zifutwe
Kamati itengeneze mazingira mazuri ikiwemo sheria na sera endelevu pamoja na mifumo ambayo inajulikana na kukubalika kimataifa ili kuchochea uchumi shindani wa kiditali na watanzania kuweza kufaidika kutokana nayo. Hii ni pamoja na kufuta ada kwa online TV ambayo itachangia watengeza maudhui wasikwepe kujisajili lakini pia kujikita katika kutengenaza vitu vyenye ubora
Kipeni Kiswahili kipaumbele, inalipa
Watengeneza maudhui wahamasike kutumia lugha ya Kiswahili kwenye kazi zao kwa kuwasilisha maudhui yenye tija, kwa kufanya hivi watafaidika na maudhui yao kwasababu tayari watakuwa na upekee pamoja na uzito ambao kampuni na taasisi mbalimbali zipo tayari kulipia ubunifu huo, ikiwemo Jamii Forums ambayo inawekeza sana kwenye uandishi wenye tija.