Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,051
- 462
- Thread starter
-
- #21
i see hongera malenga wetu
du jamaa anavo flow.... Amekuja kivingine
NaendeleaM bado nimekazana tuition kwa Lizzy, nakupa mstari mmoja nitamalizia kama home work...lol
Mvumilivu hula mbivu, ulimwengu wasasa hula mbovu... (To be cont...)
Kupendwa ni muhimu,hasa kwenye muhibu
hata nikiwa bubu,kamwe sitathubutu
magulumangu nibusu,nimekutegea shavu
hata kama ni safari,tutaishi tupendavyo?
Magulumangu mwenzio leo mistari haipandi kabisa....kila nikijaribu nagonga mwamba!!!Ila naona mwanafunzi wangu ananiwakilisha....
Naendelea
kama hutaki mbivu kula mbovu,ulimwengu ujao utakula mbivu
Magulumangu mwenzio leo mistari haipandi kabisa....kila nikijaribu nagonga mwamba!!!Ila naona mwanafunzi wangu ananiwakilisha....
Asante Shantel.... Kazi kubwa hii sijui huyu jamaa hukaa mda gani.....
hukaa ninapokaa,mistari isojaa,
sitamindi ukipaa,la malenga letu jukwaa,
njo hata kwetu kitaa,wote malenga hujaa,
Kazi ni kazi jamani,vina vishazi ni tunzi,
Busu umelitokea, nami nimelipokeaya mtende ni bahati,busu nishalitokea,
kamwe si msamiati, kuthubutu sitapotea,
nitende mi we wa ati,shanteli mwana hotea,
Tutaishi tupendavyo,mpaka mwisho wa safari,
Need I say mo.... Bravo M... Very impressive....
Busu umelitokea, nami nimelipokea
wengi walimezea, na mate kulitolea
tuendelee kulilia, jukwaa la kulengea
mwisho wa safari, tutafika tupendavyo?
mwanzo wa safari ni moja, haki nakuambiaavumaye baharini,papa kumbe wengi wapo,
acha denda watokeni,wameze kama wa mwipo,
tutafika umalengani,kwa vina vyetu simpo,
Tutafika tupendavyo,mwisho safari karibu,
umelipokea kwa mbembwe,bila mukini hiyana,
uko juu kama limbwe,uzuri wako bayana,
nipe nikupe na wewe,ujuzi wangu tisana,
Tutafika tupendavyo,mwisho safari karibu,
mwanzo wa safari ni moja, haki nakuambia
upige kelele kama chura, na ubweke kama mbwa
malenga tadumisha, na jukwaa kuanzishwa
ujuzi wako tisana,nani anabisha?
Bado nahema kwa nguvu, busu nalisikizia
papa wengi nao nyumbu, katu wanachungulia
siwezi kukupa ujuzu, busara u heshimika
mwisho wa safari karibu, safari moja huanzisha ingine
vigezo na masharti zingatia, kabla ujatia nangashanteli we uko juu,hata mimi nimekwisha,
walahi sina makuu,kwa hili utadumisha,
watasema kwa juzuu,ntabweka bila bisha,
njoo mama wewe njoo,nimeandaa sherehe,
tutamwita masanilo,kanisani unajua,
judithi dada kanilo,maombi kuyatatua,
siku uwe wangu hilo,wenye macho kuumbua,
Njoo mama wewe njoo, nimeandaa sherehe,
Yeah,ni shairi,..Duuh
Kumbe shairi
Haya bana . . . .
Tanzania Railway Stesheni, ilimtoa baba ako kijijiniYeah,ni shairi,..
ndo kazi zetu TRC siku hizi,si unajua tena treni zote zime kufa
mkuu,kipaji kinaokoa