Tanzania Railway Stesheni, ilimtoa baba ako kijijini
ikamleta mjini, kwa senti ishirini
kuikashifu ya nini, kwani imetutoa mbali
tusidharau mbachao, kwa msala upitao
Duh! kwa kweli umenifurahisha sana mrembo, kumbe na wewe wamo ki hivi? keep it upKwa heri magulumangu, muda wa kinywaji umewadia
ninatoka nyumbani kwangu, kwenda kusalandia
sisahau kipochi changu, starehe kwenda lipia
maisha ni safari, ishi upendavyo nakwambia
Mkuu kumbe umo
Unaweza kumfunika Mpoto
Kaza buti bila kikomo
Safari bado nzito
Yeah,ni shairi,..
ndo kazi zetu TRC siku hizi,si unajua tena treni zote zime kufa
mkuu,kipaji kinaokoa
Mh,acha bhana,...yaani unataka kusema
hahaha,TRC oyeeee!
Wahindi noma,yaani wameua shirika wakafundisha wafanyakazi
mashairi duh
Duh! kwa kweli umenifurahisha sana mrembo, kumbe na wewe wamo ki hivi? keep it up
hhaaa,mi nashangaa sana, nilikuwa siipendi malenga..lakini hapa ni kiboko....magulumangu kama Andanenga vile..kila comment ina shairi lake..namie naomba unijbu kwa shairi, wewe na Shantel..mpo juu,na kilio chenu chasikika.
Hindi haiko jua shairi bebe...iko kura tambuu tu...kwenda wewe sako...
Bebenangho....hahaha Mpoto kijana sana hahahahha....
Sugu wetu malaria,Aspirini dawa yake,
Babukijana silia,unga mkono babake,
Quinine sijetupilia,Field masha iwe mwake,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,
soga mhemheBebe nkoyi, Mrisho Mpoto atale nyanda???
Taratibu na mbavu zangu oohoo!
Bebe nkoyi, Mrisho Mpoto atale nyanda???
mzee ushakua msanii, mashairi yametulia!
i can guess, magulumangu yuko likozo, manake akibanwa huptea kabisa humu.
hongera kwa kupata likizo mpendwa!
soga mhemhe
Magulumangu dimbani, hongera nakupatia,
Kwa kuniweka kundini, kuishinda malaria,
Ila huyu wa jamvini, Amelogwa atakua,
Klorokwini kamshinda, Aspirini nitaweza?
Labda kikombe cha babu, tena kwa kufakamia,
Asinyweshwe kwa adabu, hatapona malaria,
Tena afungwe bawabu, asije akakimbia
Huyu Malaria Sugu, Mimi ameshanishinda.