We mkoloni kweli, au sijui ndo siasa! Kulikuwa na kona kona gani wakati ilikuwa inasaidia kurahisha ufanyaji wa malipo?! Ina maana umesahau zamani kabla ya huduma za namna hii watu walikuwa wanalazimika kwenda ofisi za TANESCO na kukaa masaa kibao kununua umeme wa sh. 5000 tu?!
Kwanini sekta binafsi hawaitumii, kwa mfano sekta ipi?!
Moja ya mambo yanayoonesha ni namna gani Magufuli amefeli kwenye sekta binafsi ni hili la MaxMalipo! MaxMalipo walikuwa very aggressive with high desire to expansion beyond the borders! Magufuli angekuwa ni mtu mwenye maono, mosi angeanza kuangalia tatizo la MaxMalipo hasa lipo wapi! Kama MaxMalipo walikuwa wanafanya biashara kwa ujanja ujanja, basi wangeanza ku-deal na huo ujanja ujanja! Na kwavile serikali ilishakuwa na mpango wa kutumia system yao wenyewe; basi wangeanza kwenda nao taratibu kwenye kipindi cha mpito, huku wakifanya attempt ya kuwaunganisha na masoko ya nje!
Serikali isiyolinda local innovation and services ni serikali ya hovyo!! Look at China ilivyosimama na Huawei dhidi ya figisu figisu za Donald Trump!! Matokeo yake, badala ya Huawei kutetereka, ndo kwanza inazidi ku-shine na kutishia brands kubwa Apple na Samsung!! Apple pumzi zimewabana hadi wanafikiria kupunguza bei bidhaa zao kwenye soko la China kwa mamilioni ya Wachina wanazipa kisogo Apple!!
Wabongo mkisikia Wabongo wenzenu wanakatwa lose, mnafurahia!!