Maximo.......je unamkumbuka kwa lipi?

An example to be emulated by Tanzanian Coaches.

I can not agree more. It is sad that yeye ameonekana kushindwa, lakini i can assure you baada ya miaka miwili yote aliyoyajenga yatabomoka, utaanza kusikia wachezaji walevi, nidhamu zero, magoli 5 -0 ndipo tutakapoanza kumkumbuka.
 
Ni Maximo huyuhuyu aliyeifanya Stars ifuatiliwe na Watanzania na kuinua Uzalendo,maana angekuwa Kayuni wala tusingefikia hatua hiyo!
 
Ni Maximo huyuhuyu aliyeifanya Stars ifuatiliwe na Watanzania na kuinua Uzalendo,maana angekuwa Kayuni wala tusingefikia hatua hiyo!

well wabongo wameifuatilia lakini je hiyo Stars imefanya lipi?
Na huyo mchoma chapati wa Brazil atajivunia katufanyia na katuachia kikombe gani au ngao gani?

Aende zake huko.
 
Tutamkumbuka kwa kutewezesha Watanzania kupenda kuvaa fulana zenye bendera ya Tanzania badala ya fulana za CCM
 
well wabongo wameifuatilia lakini je hiyo Stars imefanya lipi?
Na huyo mchoma chapati wa Brazil atajivunia katufanyia na katuachia kikombe gani au ngao gani?

Aende zake huko.

Sawa! Sasa hebu niambie kama huyu mpya akishindwa kufikia rekodi ya Maximo utaniambiaje? hata kutupeleka Mataifa ya Afrika ya ndani hakuna, utasemaje?
 
kwa wale wasiojua soka na walikua wakimkandia kocha aliyeipa nchi hii mafanikio makubwa(mafanikio ni relative term mjue) sasa watajifunza kwa njia ngumu kua nchi yetu ndio haina wachezaji sasa tulitaka maximo afanye miujiza gani? wachezaji hatuna na kaseja ndio huyo kafungwa goal la kijinga kabisa ( he was bitten at his near post what a pathetic goalkeeper).

tuliweza kucheza mpira mzuri, tuliwabana senegal hadi wakawa wanaomba mpira uishe wakatoa sare kwa goli la kubabatiza, tuliwabana cameroon etoo hakufurukuta sasa tumefungwa na morocco nchi iliyochoka kimpira kwa sasa, hata algeria tuliotoa nao droo ilikua kibahati tu maana tulizuia mwanzo mwisho, chini ya maximo tulienda hadi kucheza chan na tukawafunga wenyeji sidhan kama mafanikio hayo kwa sasa yatawezekana!
 
Huyu kocha mpya amesimamia mechi ngapi na Maximo alikaa muda gani? Kaseja bado ni best goalie TZ, Pepe Reina alifungwa la kizembe na Chamakh, na yule ni kipa wa kimataifa na yupo PL; unakumbuka Seaman na goli la Ronaldinho? Unakumbuka goli la kijinga la Petr Czec? Umesahau goli la kipa wa England thidi ya USA (SA 2010)? Unamkumbuka yule Taibi wa Man Utd alivyofungwa goli la mita 45 mechi ya kwanza akiwa Man Utd? Kama uliangalia mechi utagundua tatizo aliloliacha Maximo bado lipo...kuna kipindi timu inacheza mpira, inakaba (kwa sytem ya kukamia) lakini hatuna "UFUNDI" wa kupenetrate na kumalizia!! Huyu kocha mimi naomba apewe muda, tusianze kutafutana uchawi asubuhi! Ukweli ni kwamba vipaji vya kweli siku hizi vimefichika....tunahitaji wachezaji wenye killing instincts wakiwa golini......Tunajitaji type zile za kina Mogella (Golden Boy), Malota Soma (Ball Juggler), Makumbi Juma, Omary Hussein, Hamis Gaga, Athuman China, Ntenze John etc....
Vuta subira
 

pumzi tafadhari,dkika 30 tstaz hoi.
 
all that i am saying marximo was treated unfairly considering alipotukuta na alipotuacha, kwa mfano tulitaka maximo afanye nini zaidi, wachezaji hamna hata mmoja anayecheza ligi kubwa duniani alafu mnataka twende caf, naweza tajiwa timu yoyote iliyocheza mataifa huru bila kuwa na wachezaji wanaocheza ulaya sasa tulitaka maximo afanye miujiza kwa mitumba tuliyonayo, wachezaji hata africa hawana sifa then tunataka twende caf, chan was the best we could get and its gonna still be that way for quite some time mpaka tuki get rid na wachezaji kizazi hichi ambacho maximo alijitaidi kukiondoa ila wasiojua soka wachache wakawa wanamuona kakosea kwa mfano utovu wa nidhamu wa chuji nani asiyeujua, utovu wa nidhamu wa boban nani asiyeujua, mapaka alipoenda ulaya na kufanya yake madudu ndio muamini, kaseja kafanya nini ktk soka la africa hadi aonekane kua irreprecable? he got no statue, no technic, fitina tu! nasisitiza tena kua tutamkumbuka maximo!
 
Malawi CAN 2010

acha uongo wewe,
1. Russell Mwafulirwa (born 24 February 1983 in Zomba) is a Malawian football (soccer) player who currently plays for IFK Norrköping in sweden.
2. Chiukepo Msowoya (born September 23, 1988) is a Malawian footballer, who currently plays for Orlando Pirates in the South African Premier Soccer League
3.Esau Boxer Kanyenda (born September 27, 1982 in Dedza, Malawi) is a Malawian football (soccer) striker, he is a football striker for Russia's First Division FC Rotor Volgograd.
4. Robert Ng'ambi (born September 11, 1986) is a Malawian football (soccer) player who currently plays for Black Leopards in South Africa. His position is midfielder.
5.Chiukepo Msowoya (born September 23, 1988) is a Malawian footballer, who currently plays for Orlando Pirates in the South African Premier Soccer League
 


Ujerumani kwenye world cup south africa iliundwa na wachezaji wanaocheza ligi za ndani karibu wote, mbona walifanya vyema, Maximo alifanya mambo madogo sana ukilinganisha na support aliyoipata toka kwa wadau mbalimbali tulistahili kuwa mbali zaidi kama angekuwa ni kocha bora wa kiwango-kama ni kukumbukwa labda utamkumbuka wewe na wenzio wachache-hana jipya and thanks God its a good riddance!
 
watu oooh sijui kaseja kaachwa ndo maana stars inafungwa haya sasa naona tumeshinda.
 
ni Russell Mwafulirwa na Boxer Kanyenda wanaocheza ulaya,sasa hawa wanaocheza South Africa tusiseme ulaya,au ndio ulaya ndogo,au labda alieuliza alimaanisha wanaocheza palepale Malawi?sijui
 
Namkumbuka jinsi alivyoiendesha Taifa star kibabe!kudharau ushauri wa watanzania wapenda michezo,na kumsikiliza zaidi JK aliyempa kibarua cha kuganga njaa!
 
Unamkumbuka kwa jema lipi ambalo linapaswa kuendelezwa au kwa baya lipi ambalo halitakiwi kurudiwa tena?

Namkumbaka maximo kwa kuitoa tanzania kimasomaso. Miaka mingi imepita kabla ya tanzania kujulikana katika ulimwengu wa soka na sasa tz inajulikana angalau kidogo. Watanzania tusiwe wezi wa fadhila na wachoyo wa shukrani. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tusiposhukuru kwa kile kidogo alichotupa maximo kamwe hatutaweza kushukuru kwa kikubwa kutoka kokote duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…