SI KWELI Mayai ya Kuku kutoka nje ya Tanzania, yalisababisha kushuka kwa bei ya Mayai

SI KWELI Mayai ya Kuku kutoka nje ya Tanzania, yalisababisha kushuka kwa bei ya Mayai

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Juni 14, 2021 mitandao mbali mbali ya kijamii ilirindima kwa uvumi kuwa kuna mayai ya kuku kutoka nje ya Tanzania ambayo yamefanya mayai nchini yauzwe kwa Tsh. 4000 kwa trei la mayai 30, hali iliyoleta taharuki kwa wafugaji wa kuku nchini.

1668405721226.png
 
Tunachokijua
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilifanya uchunguzi kwenye masoko makuu katika miko yote ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu Taarifa kwamba kuna mayai ya kuku kutoka nje ya Tanzania yanayoliweka soko la mayai nchini katika kitendawili kigumu. Uchunguzi huo ulifanyika Juni 15, 2021 ili kubaini bei ya soko ya mayai.

Katika Uchunguzi uliofanywa na Wizara wafugaji wakubwa wa kuku wa mayai na wafanyabiashara waliulizwa kuhusu bei za bidhaa hiyo. Mbali na uhaba wa vifaranga uliokuwepo kutokana na COVID-19 uchunguzi ulibaini bei ya mayai ni kuanzia Tsh. 6500 kwa trei mpaka Tsh. 9,000 kwa trei. Huku yai moja likiuzwa kuanzia Tsh 250 hadi 500.

Hakukuwa na wingi wa Mayai yanayoingia kutoka nje ya Tanzania yanayoshusha bei ya mayai yanayozalisha nchini. Taarifa hizo zilikuwa uzushi. Hata hivyo, kumekuwa na matukio machache ya uingizaji wa mayai nchini kwa njia za panya lakini Wizara imekuwa ikidhibiti hali hiyo. Mwezi wa Aprili, chama cha wafugaji wa kuku kiliomba makampuni ya kuku yaruhusiwe kuingiza vifaranga wa kuku wa nyama, vifaranga wa kuku wa mayai na mayai ya kutotolesha kutokana na uhaba mkubwa wa vifaranga nchini na Serikali imeruhusu kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Juni mpaka Agosti 2021.
Back
Top Bottom