Mayalla: Wapo kina "Yuda" wema wenye kukataa kushiriki uovu

Mayalla: Wapo kina "Yuda" wema wenye kukataa kushiriki uovu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwanahabari Mkongwe Nchini Tanzania Bw. Paschal Mayalla amesema kikawaida katika dhana ya usaliti kuonekana jambo baya, pale inapotokea watu wanapanga mambo mabaya na maovu, yeyote atakayejitokeza katikati yao na kusema kuhusu njama hizo dhana hiyo hugeuka na kuwa dhana nzuri na yenye tija kwa jamii husika.

Mayalla amebainisha hayo leo Jumamosi Juni 06, 2026 wakati akizungumza na chombo hiki cha habari Jijini Dar Es Salaam, akirejea mfululizo wa matukio ya watu kupotea na kutekwa, akisema upo uwezekano wa wapangaji wa matukio hayo kutokukubaliana pamoja katika kutekeleza matukio hayo, hivyo anapotokea mmoja wao kuzungumza hadharani kuhusu matukio hayo, huyo mtu hugeuka kuwa msaliti mwema.

"Katika dhana hii ya usaliti, japo usaliti unaonekana kama jambo baya, lakini inapotokea watu wanapanga mambo mabaya na mabovu na mmoja yeyote atakapojitokeza na kusema aliyepanga mambo hayo ni nani, huo nao unakuwa ni usaliti lakini usaliti mwema kwa jamii."

"Kuna hii ishu ya watu kupotea na hawa jamaa wanaoitwa wasiojulikana, japo hawajulikani, wenyewe wanajijua na hawajipotezei wenyewe, kuna mtu anawatuma kupoteza watu sasa kwavile wasiojulikana hawajulikani na anayewatuma hajulikani na hatujui wanaopotea kinawakuta nini kama ilivyokuwa kwa Humphrey Polepole, ninaamini kuna watu walipanga. Wale waliompoteza Polepole ni Watanzania wenzetu na kuna watu walipanga kumpoteza ila kuna uwezekano kwa wale waliopanga kuna mwingine hapendi kuona kile kinachotendeka kwahiyo mtu huyu ikitokea akaja kusema kuhusu kupotea huko kwa watu mtu huyo anakuwa msaliti kwa wenzake waliokuwa wakipanga nae lakini kwa upande wa usalama, mtu huyo anakuwa msaliti mkombozi." Amesema Mayalla.

Soma Pia: Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani

Si kila msaliti ni msaliti mbaya. Msaliti mbaya ni yule ambaye mnapanga mambo mazuri halafu yeye anapanga mambo maovu. Msaliti mzuri bado atakuwa ni Yuda vilevile lakini mnapanga mambo maovu kuwafanyia Watanzania lakini yeye anasema hapana, mimi sipo na ninyi." Ameongeza kusema Mayalla.

 
Back
Top Bottom