Mayele alindwe na waamuzi wa ligi kuu, yeye ni nembo ya ligi yetu

Mayele alindwe na waamuzi wa ligi kuu, yeye ni nembo ya ligi yetu

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nimekuwa nikifuatilia namna wamuzi wa Ligi kuu namna wanavyoshindwa kabisa kumlinda Fiston MAYELE.

Fiston hapaswi kuchezewa rafu za kipuuzi puuzi. Inapaswa hata akiguswa kwa nguvu kidogo refa apige filimbi kuashiria faulo, hata kama sio faulo kamili. Hilo litasaidia kuwafanya wachezaji wengine kuwa waangalifu wanapo mkaba Mayele.

Naishukuru bodi ya ligi kwa kutoa adhabu kwa Yondani kwa kosa la kumkanyaga Mayele kwa kusudi kabisa.

Dhidi ya Namungu Mayele alikuwa akifanyiwa Vitendo vya uovu mno na wachezaji wa Namungo.

Mayele kwa sasa ni nembo ya LigiKUU ya Tanzania na pia ni nembo ya Taifa letu la Tanzania (Hata kama yeye si mtanzania).

Mayele akiumia na kukaa nje hata kwa mechi moja basi kuna hasara inapatikana kimapato katika vilabu vyote vya Ligi.

Akikaa nje kwa zaidi ya hata wiki mbili basi thamani na hadhi ya ligi yetu huporomoka katika viwango vya soka barani Afrika.

Taifa kama Taifa nalo linaathirika pakubwa kimapato.

Kumbukeni issue ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wangali bado La Liga.

Hawa jamaa walipewa special treatment kuanzia kwa waamuzi mpaka kwa wananchi wa kawaida.

Basi iwe ivyo kwa Fiston Mayele, tufanye ivyo kwa manufaa ya Mpira wa Bongo na Taifa kwa ujumla.
 
Wasipokuelewa wana lao jambo. Hilo suala liko wazi kabisa, Mayele anatakiwa kulindwa.

Anapaniwa sana, yani wakati wote anawindwa tena anawindwa vibaya.
 
Fiston hapaswi kuchezewa rafu za kipuuzi puuzi. Inapaswa hata akiguswa kwa nguvu kidogo refa apige filimbi kuashiria faulo, hata kama sio faulo kamili. Hilo litasaidia kuwafanya wachezaji wengine kuwa waangalifu wanapo mkaba Mayele.
Labda muanzishe ligi ya Yanga tu, ila sio hii ya NBC.
 
Back
Top Bottom